SI KWELI PreGE2025 Nipashe wamechapisha taarifa kuwa 'Halima Mdee kuwaongoza wabunge 19 wa CHADEMA kuhamia CHAUMMA'

SI KWELI PreGE2025 Nipashe wamechapisha taarifa kuwa 'Halima Mdee kuwaongoza wabunge 19 wa CHADEMA kuhamia CHAUMMA'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
1748412439074.png
 
Tunachokijua
Halima Mdee aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Kawe mwaka 2010 hadi 2020 alipoachia nafasi hiyo baada ya kushindwa na Jesephat Gwajima katika uchaguzi mkuu wa 2020. Baadaye aliteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mdee alifanya mahojiano na Shirika la utangazaji la Uingereza idhaa ya kiswahili, BBC Swahili ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia hali ya kisiasa nchini na uelekeo wake kuuendea Uchaguzi mkuu.

Katika mtandao wa Facebook ilichapishwa taarifa iliyotumia utambulisho wa machapisho ya Nipashe ikiwa na kichwa cha habari 'Halima Mdee kuwaongoza wabunge 19 wa CHADEMA kuhamia CHAUMMA'


Je, upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao uliotumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) pamoja na marejeo ya video mahojiano ya Mdee na BBC Swahili yaliyochapishwa YouTube Mei 28, 2025, JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Aidha Chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo si la kweli, ni la kutengeneza na wapotoshaji kwani halijachapishwa katika kurasa rasmi za Nipashe.

Aidha katika mahojiano aliyofanya na BBC Swahili Mdee alieleza, kuwa akiwa sehemu ya watu walioijenga taasisi (CHADEMA) kwa miaka zaidi ya 20 hafurahii kuona mgawanyiko mkubwa huku akisema ataweka wazi kama atagombea ubunge na atagombeaje baada ya kuvunjwa kwa bunge.​
Back
Top Bottom