SoC02 Nipe dili...

SoC02 Nipe dili...

Stories of Change - 2022 Competition

Actuality

Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
7
Reaction score
10
“NIPE DILI”

NYUMBANI

Ni saa tatu asubuhi naamka napiga miayo aaaaaaaahhhhh, naamka toka kwenye kitanda cha nyumbani kwa mzee Wamwise, kinachoniamsha ni kelele za kufoka za mzee Wamwise na mkewe wakilalamika wajukuu zake kulala sana, na kelele za wapangaji wakiwa na shughuli zao mbalimbali za nyumbani,


Mzee Wamwise: Mna lala tu, kuna siku mtakuja kuamka mkute dunia haipo

Bibi Wamwise: Acha walale labda wana uhakika wa kula leo maana hapa hakipikwi kitu leo kwa walalaji

Mpangaji 1: We lulu, lulu muone bichwa ka baba ako unaendaje shule hujapaka mafuta? Hebu njoo”

Mazungumzo hayo yanafanya nitabasamu tuu, huku ndo kwetu bana. Natoka nje najiandaa kwa kutoka japo kutafuta chochote cha kufungua kinywa maana imetangazwa hali ya hatari kwa bibi Wamwise kuwa leo hakipikwi kitu. Naondoka zangu nyumbani moja kwa moja mpaka kijiweni kwetu. Nawasalimu washikaji ambao nimewakuta kijiweni


KIJIWENI

Mimi
: Niaje?

Washikaji: Poa engineer wa mtaa. Leo umekuja na nini baba?

Mimi: Mnataka dili sio?

Washikaji: Imechuchumaa hiyo baba, mbona unauliza majibu.

Mimi: Nina mshikaji wangu yuko Chuga anataka mende, kila mende mmoja shilingi 200.

Mshikaji 1: Mende?!!!!

Mimi: Eehhh huelewi wapi baba.

Mshikaji 1: Upo seriouse engineer?!!!

Mimi: Baba meseji hizi hapa kanicheki jana watsup anataka mende, wanahitajika kenya huko na wenzetu

Mshikaji 2: Kwani anataka mende wangapi?!

Mimi: Uwezo wako wewe. Ila kila mende mmoja shilingi 200

Mshikaji 3: Mende hawa hawa wa chooni na kabatini wanauzwa 200???!!

Mimi: Baba hutaki au? Ndo dili la leo hilo

Mshikaji 2: Ila hizi kamba za engineer.

Mimi: Sio kamba baba hilo ndo dili la haraka baba kama unaweza kuwakusanya kazi kwako, we kusanya niletee wakala wa mende hapa upate mzigo wako

Mshikaji 3: Ila mdogo angu engineer, we ni msomi japo huna ajira tupe mchongo ambao utatubariki kwa muda mrefu hizi mishe za chap chap sio, huwa hazina uhakika sana.

Mshikaji 2: Kweli maana ushatupa dili kibao na tumeambulia kula tuu na bado hatuna mchongo wa kudumu.

Mshikaji 1: Tupe dili engineer tuishi sio tule tu baba.

Mimi: Kweli mnahitaji dili la kudumu??

Mshikaji 3: Unauliza Mende chooni.

Mimi: Asa kumbe unapajua pa kuwapata mende (akacheka)

Washikaji: (Wanacheka)

Mimi: Sasa sikiliza, si unajua mafuta ya kupikia saivi adimu sana bongo hapa

Washikaji: Eeehhh!!!!!!

Mimi: Hilo ndo tundu lenyewe, tunatokea hapo

Mshikaji 2: kivipi baba?

Mimi: Hapa kwetu watu wanalima sana karanga, ufuta, alizeti na tuna parachichi si ndio.

Washikaji: Enheee!!!

Mimi: hivyo vyote ni vyanzo vya mafuta ya kupikia.

Washikaji: kweli

Mshikaji 1: Nakubali

Mimi: Tunanunua mashine 2 za kukamua mafuta ya karanga,ufuta na alizeti na mashine ya kuyachuja, kisha tunafanya upakiaji kwenye makopo safi kisha tunaenda sokoni wazee.

Mshikaji 3: Hapo manake tumefungua kiwanda si ndio?

Mshikaji 1: na kama ni hivo ni kiwanda basi kinatakiwa kusajiliwa na SIDO au?

Mshikaji 2: Maana yake inakuwa kama kampuni tunaisajili TRA na BRELA pia.

Mimi: Asa walimu mnafeli wapi mmekaa mtaani mkajisahau kutumia elimu yenu kumbe tukiamua tunaweza kuwa wawekezaji wakubwa tu.

Mshikaji 1: Huu mchongo ukitiki hata ajira za ualimu siombi tena nafanya yangu

Mshikaji 2: Kweli

Mshikaji 3: Tunaweza kama tukiamua

Mimi: Sasa ili tuweze fanikisha mchongo mkubwa lazima tupambanae michongo midogo midogo itupe mtaji wa kupata hizo mashine na kuanzisha kiwanda, tukijiwekeza kidogo kidogo kwa pamoja na kwa malengo kuna siku kijiwe chetu kitahama na kuwa ndani ya nyumba na sio chini ya mti tena

Washikaji : Kweli

Mshikaji 3: Kwani hizo mashine bei gani na zina ukubwa gani

Mimi: Zipo ndogo ambazo ni rahisi kutumia na bei huanzia milioni 1 mpaka 2

Mshikaji 2: Aaahhh inawezekana kumbe

Washikaji: Inawezekana

Mimi: Kwa kiwango cha chini tuwe na kama milioni 5 hivi tunaweza kuanza

Mshikaji 1: kabisa

Mshikaji 3: Mbinu ya masoko mtaniachia mimi

Mimi: Mwalimu na masoko wapi na wapi?

Mshikaji 2: Labda tumuulize anafanyaje?

Mshikaji 3: Mbona rahisi tuu, tunatumia mbinu ya mitandao ya simu tunatembeza bidhaa nyumba kwa nyumba na kutoa elimu pia kama tunasajili line hivi.

Mimi: Duuuh nakubali. Sasa kila mwezi tunaweka laki moja kwenye akaunti ya kikundi chetu, ili kuanza kujipanga.

Mshikaji 3: Tufanye laki na nusu wazee

Washikaji: Kweli

Mimi: Poa maana nilikuwa nawahurumia nyie wenye watoto na ajira hamna

Mshikaji 1: Hhahhhahh we ajira unayo???

Mimi: Oya poa wanangu tukahangaike sasa sio muda wa kukaa hapa tena tayari tuna malengo makubwa

Washikaji: Poa tusambae tukapambane

Mimi na washikaji: Poa

Mshikaji 3: Tukutane kesho hapa hapa kuandaa mkataba wa makubaliano

Washikaji na Mimi: Sawa Mzee wetu wa kijiwe

Mimi: Halafu kabla ya kuondoka tumeongea mengi sana ila mshaurini mwalimu mwenzenu aache gongo na sigara atakufa.

Mshikaji 1: Achana na mimi wewe

Mimi: Nakuachaje sasa wakati tumepanga wote mambo ya maana hapa ukilewa utafanya kazi kweli baba?

Mshikaji 2: Kweli jamaa huitaji kuwa na msongo wa mawazo tena tupambane tutoke achana na pombe kali na sigara kali ankali

Mshikaji 3: Mwana tusikilize na tutakusaidia kuacha. Kwa kifupi tuwe nae karibu ataacha tu.

Mimi: Sawa hakikisheni anaacha pombe kali huyu na sigara zake sivyo hatuwei fanya kazi na mlevi sisi, japo tunampenda ila aache tuwe sawa

Mshikaji 1: Poa washikaji nimewaelewa nitajitahidi niache, siunajua tena nimesoma ila mwaka wa nane huu sina ajira na maisha magumu ila nitaacha tu, tupambane.

Washikaji: Nani hajasoma sasa?

Mimi: Haya nakupa dili nenda mnadani kalete viazi tupige mzigo leo nguna ya mchana utakuja kupiga hapa kijiweni

Mshikaji 1: Kweli engineer?

Mimi: Hutaki au?

Washikaji: Oya poa basi pamoja badae jamaa.

Mimi: Poa walimu

Hivi ndivyo tulivyo mimi na washikaji zangu kila siku ni mapambano hatuna wa kumlaumu na kila siku tunapanga dili jipya ili tuu mdomo uende kinywani sisi na familia zetu wale wanaotutegemea maana hatuwezi tu kusuburi ajira ili maisha yaendelee lazima tuishi. Sasa tumepata mchongo mpya huenda ndio tundu letu la kutokea ngoja tupambane tuone. KARIBU KIJIWENI NIKUPE DILI.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom