Nipe jina na maana ake

King Rabbit

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2015
Posts
1,145
Reaction score
4,293
Baada ya kuwa baba kijacho kwa miezi 9 sasa hatimae muda si mrefu mungu akijalia mkono wake wa neema natarajia kuitwa baba fulani....

Kwangu mimi mtoto ni mtoto haijalishi awe wa kike/kiume wote ni watoto.

Jina kwa upande wa mtoto wa kiume ninalo tayari,lakini kwa upande kike sijalipata bado.

Kwa kuzingatia mambo tajwa hapo juu naomba msaada wa wadau kupekua library za bongo zenu na kila mmoja apendekeze jina analohisi ni sahihi kwa mtoto wa kike.

Nakaribisha majina na maana zake kwa jinsia ya kike.

#Karibuni nyote.
 
Shekh kwakuwa kazaliwa awamu ya 6 na mama ndio kashika nchi basi ungempa jina sawa na mshika nchi iwe kumbukumbu maana inaweza isitokee tena.
 
Muite chaupole ili akikua aweze kuitwa kulingana na tabia zake.

Akiwa mtaratibu abaki akiitwa Chau-pole

Mbea aitwe Chau-mbea

Mcharuko aitwe Chau-siku


Kila la kheri baba Chau
Kule Japan nadhani,kila happy birthday mtoto anabadilishwa jina,bongo bahati mbaya ukipewa 1 mpaka kifo....
 
Shekh kwakuwa kazaliwa awamu ya 6 na mama ndio kashika nchi basi ungempa jina sawa na mshika nchi iwe kumbukumbu maana inaweza isitokee tena.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
Hii nimeipenda sana mkuu,changamoto ni mimi mkristo bila dini hakika hii imeingia kwenye kinyang'anyiro.
 
Kiroho,mwanao kwanza atakua mtu makini, pili, atakua mkali simanishi sura namanisha kiroho maana hii karama mungu kanipa,huyu type za ni za wale shangazi wa tweete,akili nyingi sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]......kwamba ni hasara et!!!
Watoto wa kiume ni hasara tupu,kwetu tupo watoto wa kiume watatu ambao wamesomeshwa na wana maisha yao mazuri tu ila wazazi wanasaidiwa na watoto wa kike ambao waliishia la saba ambao ni wauza magenge.Baba na Mama walidharau kusomesha watoto wa kike na kung'ang'ania kusomesha wa kiume wakifikiri kuwa wako sahihi kumbe waliruka mkojo wakakanyaga mavi.Hali ya maisha ya Baba na Mama siyo nzuri.
 
Pole sana aiseee sasa napata maana halisi ya kwanini ulisema vile....lakini hii si inategemea na akili ya mtu pamoja na makuzi anayopitia?
 
Kiroho,mwanao kwanza atakua mtu makini, pili, atakua mkali simanishi sura namanisha kiroho maana hii karama mungu kanipa,huyu type za ni za wale shangazi wa tweete,akili nyingi sana
Halelluyaah......ameeeeen[emoji350]
 
Pole sana aiseee sasa napata maana halisi ya kwanini ulisema vile....lakini hii si inategemea na akili ya mtu pamoja na makuzi anayopitia?
Wala,mfano sisi kwetu watoto wa kiume tuna maugomvi yasiyoisha kati yetu ambayo yamepelekea mpaka kutokuwasiliana na wazazi na pia imepelekea kublock misaada kwenda kwa wazazi pia wakati watoto wa kike wanaishi kwa umoja,upendo na kuheshimiana.Nilichojifunza ni kwamba watoto wa kiume siyo watoto sahihi wa kuzaa.Kwetu kila mtoto wa kiume anajiona yeye ndiye mkubwa na mbabe kupita wengine kitu ambacho kimesababisha kila mtu kuishi life lake na mbaya zaidi moto unachochewa na wazazi kutaka kumpendelea mmoja zaidi na kudharau wengine.
 
Aisee...kwahiyo mkuu simu inapandikizwa kizazi kimoja hadi kingi....kwenye shughuli za jamii mnakutana??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…