Kwa anayeijua soka vilivyo na aliyeona soka kwa uhakika ni ngumu sana kutaja wachezaji 11 tu katika hiyo miaka 16, ambayo kwa mahesabu ya haraka inaanzia mwaka 1995 unless atumie mapenzi binafsi na si uwezo halisi wa wachezaji. Ninaamini ili uweze kupata hao wachezaji kuna ligi kadhaa ambazo ndio zina competition kubwa zaidi na zenye mvuto zaidi duniani zikiongozwa na kombe la dunia, kome la ulaya (EURO) na kombe la ulaya la vilabu (UCL)
Ili uweze kupata hiyo list ni lazima kwanza uweke vigezo kadhaa na pia uweke upenzi wa timu pembeni. Ukiangalia uwezo binafsi wa mchezaji, msaada wake katika club yake, umuhimu wake katika timu ya taifa na pia mafanikio aliyoweza kuyapata kama mchezaji na kama timu hapo tayari utakuwa umeweza kuweka vigezo kadhaa vya kuweza kupata hao wachezaji husika.
Nikikumbuka mwaka 1995, ndio mwaka ambao Ajax ilikuwa bingwa baada ya kumfunga AC Milan goli 1 la Patrick Kluivert, kumbuka kuwa AC Milan ilikuwa bingwa 1994. Wakati huo huo Brazil ya kina Romario, Bebeto na kapteni Dunga ilikuwa bingwa wa dunia 1994. Bingwa wa Ulaya kipindi hicho ilikuwa Denmark ya kina Laudrup ambayo kwa hakika wapenzi wengi wa soka tunaamini ilichukua ubingwa huo wa mwaka 1992 kwa bahati ya mtende.
Katika kipindi cha miaka ya 94, 95, 96 ambako ndio hasa mtoa mada anapenda tuanze kuchambua hao wakali ni kipindi ambacho, AC Milan ya kina Geogre Weah, Ajax ya kina Edgar Davids, Mark Overmars, Nwanko Kanu na Van Der Sar zilikuwa zipo katika kiwango cha juu mno na huku Barcelona iliyokuwa na wakali sana kama Romario, Histro Stoichkov na Pep ndio ilikuwa inaanza kushuka baada ya ile wao wanayoiita the dream team ya mwaka 1992. Pia Juventus ya kina del Piero na Fabrizio Ravanelli ilikuwa kati ya timu zenye kiwango cha kuogopwa sana ulaya
Nimejaribu kuzungumzia haya machache katika kutaka kuweka misingi ya wapi tunaanzia kwenye kuwachambua hao wachezaji bora 11, maana kila mmoja anajua wapi tunaishia ambako ni mwaka huu !
Binafsi nitataja wachezaji 20 ambao kwangu naona kuwa wamekuwa au walikuwa ni wakali zaidi, na hivyo sitapanga kikosi cha hao wachezaji 11.
Zinedine Zidane. Huyu ni midfield maestro. Mchezaji bora zaidi kutokea katika hicho kipindi mtoa mada anachokisema.
Edgar Davids. Huyu ni holding midfielder mkali zaidi niliyewahi kumuona akicheza. Ninaamini Davids ndio kiungo bora zaidi wa kukaba katika hiki kipindi. Combination ya Davids na Zizzou katika midfielder waliifanya Juventus kuwa timu kali sana mwishoni mwa miaka ya 90.
Ronaldinho Gaucho
Alessandro Del Piero
Louis Figo
Ronaldo De Lima
Romario
Edwin Van Der Sar
Paolo Maldini
Alessandro Nesta
Marcos Evangelista De Moraes wengi mnamjua kwa jina moja la Cafu
Roberto Carlos
Lionel Messi
Rivaldo Vitor Borba Ferreira
Oliver Khan
Christiano Ronaldo
Gabriel Batistuta
Erick Cantona
Mark Overmars
na wa 20 ni Histro Stoichkov.
Histro Stoichkov huyu kwangu ndiye mchezaji mkali zaidi niliyewahi kumuona wa dead balls. Japokuwa Juninho Pernambucano naye alikuwa ni hatari sana wa dead balls, ila hayupo katika list yangu ya wachezaji 20.