Nipe maoni yako mdau, natokaje hapo na hawa NIDA

Nipe maoni yako mdau, natokaje hapo na hawa NIDA

second chance

Member
Joined
Sep 20, 2022
Posts
15
Reaction score
13
Habari za wakati huku wanajamvi wa jamii forum. Natumai mu wazima wa AFYA teletele.

Napenda kutumia fursa hii kuwasilisha dukuduku langu kuhusu masuala ya USAJILI wa huduma mbalimbali katika kizazi hiki. Tunaishukuru serikali imeleta USAJILI kupitia NIDA na kupitia NIDA, watu wafanye USAJILI wa akaunti zao benki, mashuleni/vyuoni, visa, USAJILI wa SIMCARD, ajira, na nyingine nyingi.

Ili kwa namna moja au nyingine ili kuongeza uwajibikaji, kupunguza upotevu wa taarifa muhimu na kuondoa udanganyifu.

Na kwa vyovyote vile tulitegemea na tunaendelea kutegemea kurahisisha zaidi maswala ya sajili mbalimbali ikiwemo suala la mifumo kusomana. Ila kilichopo mtaani watu wanaumizwa sana ikiwemo mimi kuhusu huu USAJILI wa NIDA. Nitaelezea kwa kadiri niwezavyo kuwaelewesha masaibu hayo. Huenda kuna mwenye kuweza kunishauri jambo hapa jukwaani.

Mambo ni mawili

MOSI.
Nilifanya mabadiliko ya jina kwenye NIDA na kabla mabadiliko hayajafanyika bahati nzuri nikapata ajira kupitia jina la hio NIDA (nilifanya mabadiliko hayo ya majina kwa sababu majina yalikuwa hayafanani na majina yaliyopo kwenye vyeti, na wao NIDA ndio walionakili tofauti na uhalisia. Mf. Stephano kwa Stefano au masawe kwa massawe. Nazungumzia tofauti ndogo ndogo sio za kwenda kuapa) yenye majina yenye makosa. Miezi kadhaa ikapita nikiwa ajirani na NIDA wakawa wamerekebisha majina yakawa yanafanana na vyeti, niliona nimefanikiwa sana.

Lakini isivyo bahati nikihitaji huduma mbalimbali zinazohitaji namba ya NIDA kunatokea mgongano kwenye mifumo. Mwajiri ananitambua kwa majina ya NIDA ya zamani, na sasa NIDA wamenibadilishia majina. Kwa hio nakosa huduma kwa sababu ya mabadiliko hayo. Na pia nilimwandikia barua mwajiri kuomba kufanyike mabadiliko kwenye majina hayo, naona hakuna majibu ni mwaka mmoja umepita sasa. Naomba wadau nifanyeje kwa kadhia hii?

PILI.
Mifumo hii tulitegemea na tunategemea iturahisishie mambo kama nilivyokwisha eleza. Pia ningependa kuona taasisi au makampuni tuliowapa taarifa zetu za NIDA, wawe Wana HUISHA/UPDATE taarifa zetu. Waiweke hata iwe AUTOMATIC Ili baada ya muda fulani kupita taarifa zetu ziwe za leoleo.

Ipo pia changamoto wakati wa uhakiki wa NIDA, mfano unaulizwa jina la mama la mwisho au la kati hii haina shida sana, shida ipo hapa- mfano wanauliza pia kata uliyozaliwa, au wilaya uliyomalizia darasa la saba au kata uliyojiandikisha NIDA na wakati huo upo mjini na uliandika kuwa umezaliwa kata ya kule kijijini kwenye ile form yangu ya NIDA wakati naapply. Ni nani awajibike kwa makosa haya? Tuliandika taarifa kwenye form, lakini sio taarifa zinazowekwa kwenye mfumo.

Ushauri, maoni, nini kufanyike ili tuzidi kusonga mbele kama taifa, karibuni wanajamvi.
 
Back
Top Bottom