Uchaguzi 2020 Nipeni miaka mitano muone maajabu

Asante...

Hatutakuja kupata kiongozi Mungu.

Ila wapinzani waache wapnge maana kupinga ndiyo uhai wao. Waendelee tu.

Kipindi cha Mkapa walilalamika Rais dikteta hafai kututawala.

Akaja JK tukamsema huyu kageuza nchu shamba la bibi. Tu/wakatamani kiongozi mwenye mamlaka. Anayeweza kunguruma kidogo.

Akaja JPM...malalamiko hayajaisha. Rais ni mtu sio Mungu. Lazima wawepo wa kuumizwa na wa kufurahishwa na maamuzi anayotoa.
[emoji122][emoji122][emoji122]
Mimi bado sijaona mbadala wa JPM.
Wiki iliyopita jmosi nilikuwepo pale jamhuri Dodoma kumsikiliza JPM,
Leo nimeenda viwanja vya CCM Mbeya kumsikiliza Lisu.
Naona Lisu bado Sana
 
Nyie chadema mna bangi kweli. Hivi utawaongezea mishahara wafanyakazi alafu serikali iache kuwekeza kwenye miradi Ambayo itakuja kuwa mkombozi kwa wananchi WOTE?

Hivi kupi ni bora kuwekeza kutakapo kuja kukupatia kipato kitakacho kuwezesha kujikimu na kuhudumia familia yako vizuri.

Au Bora kula kipato chote unachokipata pasipo kuwe keza?

Unaposema serikali haija Ajiri watumishi katika sekta je! Ni Vyema kuajiri lundo la wafanyakazi Ambao hutaweza kuwalipa vizuri?

Chadema WOTE Akili zao ni Ndogo sana Mna zani kuongoza nchi ni sawa na kuongoza kijiwe cha kahawa.

Nyinyi ni vipofu na hamjui Impact ya Serikali ya Awamu ya 5 kwa Kazi kubwa iliyofanya Mtakuja kuona Hapo Baadae wakati mmeshapata Akili.
Kama ni watu wote mbona wabunge wamepewa fedha zao zote
 
Mwaka 2015 ulipewa miaka mitano na kwa kweli tumeona maajabu mengi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu watumishi wa umma wakasota miaka mitano bila kupata nyongeza ya mshahara ambayo ni haki yao kisheria. Gharama za maisha zikapanda lakini kipato cha watumishi kikabaki kilekile. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia wahitimu wa kada muhimu kama udaktari na ualimu wakisota mtaani bila ajira lakini hospitali hazina madaktari na shule hazina waalimu. MAAJABU.

Tukashuhudia watu wa Kimara wakivunjiwa nyumba bila kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya kikoloni ya mwaka 1932. Wakaenda mahakamani, na mahakama ikaweka zuio, lakini amri ya mahakama ikapuzwa na nyumba zikavunjwa. MAAJABU.

Tukashuhudia bunge likifanyiwa "shooting" kama bongo movie. Hotuba za wabunge zinakua censored kwanza. Walioongea maneno makali wanakatwa, walioipamba serikali wanaenda hewani. Bunge likapoteza focus na kuanza kuipongeza serikali wakati kazi ya bunge ni kuisimamia serikali. MAAJABU.

Tukashuhudia RC akivamia studio na mitutu ya bunduki kulazimisha "clip yake ya umbea" irushwe hewani. Chombo husika kikaamua kuzingatia maadili na kukataa kurusha clip hiyo. Waandishi wakavamiwa na kutishwa. Waziri aliyeunda Kamati ya kuchunguza suala hilo akafurushwa. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza mifuko ya hifadhi ya jamii ikafuta fao la kujitoa. Watumishi wa mikataba na wa muda mfupi wakaambiwa hadi miaka 60. Mtu mwenye akiba ya 5M na kwa sasa ana maika 25 unamwambia hadi afikishe miaka 60? Yani miaka 35 ijayo? Akifikisha miaka 60 hiyo 5M si itakua ya kununulia mkate tu? MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia Hakimu aliyekua kwenye likizo ya kustaafu akiteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia mbunge akipigwa risasi kwenye makazi yenye CCTV camera. Lissu akasema camera ziliondolewa baada ya tukio. Hakuna mshukiwa hata mmoja aliyekamatwa hadi sasa. MAAJABU.

Tukashuhudia mikutano ya siasa ikipigwa marufuku kinyume na katiba na sheria za nchi. Viongozi wa upinzani walipofanya vikao vya ndani walikamatwa lakini CCM walifanya mikutano ya hadhara na vikao bila bughudha. MAAJABU.

Binafsi naona maajabu yametosha baba. Hatutaki maajabu mengine.!

Malisa GJ
Sasa hivi tunaonajionea miujiza hayo maajabu hapana aisee
 
Maajabu ya bwana Magufuli hayaishi.

Chini ya utawala wake ametamka mara nyingi kwamba majimbo yaliyokosa miradi ya maendeleo ni kwa sababu walichagua wabunge kutoka vyama vya upinzani.

What a stupid remark from the head of the state.

Huyo ndio anaitwa msomi eti.
 
Hivi utawaongezea mishahara wafanyakazi alafu serikali iache kuwekeza kwenye miradi
Leo Magufuli akiongeza mishahara utakuja hapa hapa kushangilia huku unamuita "jembe" la awamu ya tano!

Jamani, tupunguze kuwa viherehere na vifwata upepo! Jifunze kuwa na FIKRA HURU!

Wengi wenu hamuelewi hata basics za kiuchumi. Kazi yenu ni kupiga makofi tu na kubwata!
 
Mama yako angedhalilishwa hivi usingeandika huu upuuzi wako.

Asante...

Hatutakuja kupata kiongozi Mungu.

Ila wapinzani waache wapnge maana kupinga ndiyo uhai wao. Waendelee tu.

Kipindi cha Mkapa walilalamika Rais dikteta hafai kututawala.

Akaja JK tukamsema huyu kageuza nchu shamba la bibi. Tu/wakatamani kiongozi mwenye mamlaka. Anayeweza kunguruma kidogo.

Akaja JPM...malalamiko hayajaisha. Rais ni mtu sio Mungu. Lazima wawepo wa kuumizwa na wa kufurahishwa na maamuzi anayotoa.
 
Magufuli anatosha sana kuirudisha Tanzania kwenye mstari. Tanzania ndio nchi ambayo ilijipambanua kukomboa Africa na kufanikiwa. Baada ya ukombozi na sasa chini ya Rais Magufuli Tanzania imejipambanua kuiendeleza kufikia kiwango cha nchi za Europe. So far at the moment Rais Magufuli anaonyesha kila dalili ya kufanikiwa ingawa wapo wachache wanaombeza.

Hata wakati wa ukombozi wapo waliobeza. Ignore Tanzania and John Pombe Magufuli na utaona Tanzania inayomeremeta. Utakapofika uchaguzi wa 2025 Tanzania itakuwa kwenye level nyingine kabisa economically and politically siasa zetu zitabadilika na kuangalia jinsi tunavyoweza kujitegemea na kuwa tegemeo la nchi nyingine duniani kwa sababu moja kubwa; Afrika haihitaji kuwategemea foreigners kuja kuwatatulia matatizo yao. (Bwawa la Mwalimu Nyerere litakuwa limekwisha, SGR itakuwa imefika makao makuu ya nchi Dodoma).

Watanzania walikuwepo toka enzi na enzi, wezi wa kisasa baada ya kuvamia wamekuwa wanajitajirisha na uroho wa viongozi wachache wasio waaminifu. Wana JF tuombe uzima tu ifikapo 2025, will you be there?
 
Back
Top Bottom