Nipeni ufafanuzi juu ya majina ya ukoo yanayoanza na "Mwa" kutumika Mbeya, Njombe na Iringa

Nipeni ufafanuzi juu ya majina ya ukoo yanayoanza na "Mwa" kutumika Mbeya, Njombe na Iringa

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Hapo zamani kila mtu ambae jina lake lilianzia "Mwa" nilidhani ni mnyakyusa, ila baada ya muda nikajua kwamba watu wenye haya majina wamesambaa makabila mengi ya Mbeya, Iringa na Njombe

Wanyakyusa wapo kina Mwakyusa,

Wahehe wapo kina mwakatundu (mfano msanii mike tee)

Wabena wapo kina Mwajombe

Wasafwa wapo kina Mwashinga.

Wakinga wapo kina Mwakipande

Na makabila mbalimbali ambayo yapo hayo maeneo si ajabu kukuta haya majina.

Naombeni mnipeni elimu juu ya hili fumbo
 
Upo sawa majina hayo yenye kuanza na Mwa yapo mikoa hiyo uliotaja,ila asilimia 99% ya majina hayo ni ya wanyakyusa, mimi nimezaliwa Mbeya na kukulia huko,nilichogundua ni kwamba,kwa wanyakyusa neno Mwa hapo zamani sana walilitumia kama Mr, au Sir, sababu ukienda huko kwao utakuta katika ukoo kama wanaume wataitwa Mwakipesile basi wanawake wataitwa Kipesile au kama wanaume wataitwa Mwambapa basi wanawake wataitwa Mbapa,hii isikuchanganye sana huwa inatumika unapomuita mtu unataka either kuongea naye au kumpa kitu fulani,lakini linapokuwa ni suapa la kuandikishwa shule au cheti cha hospitali ,mwanamke ataandikwa jina la ukoo wake kama lilivyo. Lakini pia kwa faida ya wasomaji zipo Koo zingine za kinyakyusa hazianzii na Mwa,mfano Kibonde,Kasulu,Kakuyu n.k ila ni asilimia ndogo.
 
Hapo zamani kila mtu ambae jina lake lilianzia "Mwa" nilidhani ni mnyakyusa, ila baada ya muda nikajua kwamba watu wenye haya majina wamesambaa makabila mengi ya Mbeya, Iringa na Njombe

Wanyakyusa wapo kina Mwakyusa,

wahehe wapo kina mwakatundu (mfano msanii mike tee)

Wabena wapo kina Mwajombe

Wasafwa wapo kina Mwashinga.

Wakinga wapo kina Mwakipande

Na makabila mbalimbali ambayo yapo hayo maeneo si ajabu kukuta haya majina.

Naombeni mnipeni elimu juu ya hili fumbo
Mwakatundu ni Wanyakyusa sio Wahehe. Mike Tee anajiita mnyalu kwa sababu amekulia Iringa.
 
Back
Top Bottom