Upo sawa majina hayo yenye kuanza na Mwa yapo mikoa hiyo uliotaja,ila asilimia 99% ya majina hayo ni ya wanyakyusa, mimi nimezaliwa Mbeya na kukulia huko,nilichogundua ni kwamba,kwa wanyakyusa neno Mwa hapo zamani sana walilitumia kama Mr, au Sir, sababu ukienda huko kwao utakuta katika ukoo kama wanaume wataitwa Mwakipesile basi wanawake wataitwa Kipesile au kama wanaume wataitwa Mwambapa basi wanawake wataitwa Mbapa,hii isikuchanganye sana huwa inatumika unapomuita mtu unataka either kuongea naye au kumpa kitu fulani,lakini linapokuwa ni suapa la kuandikishwa shule au cheti cha hospitali ,mwanamke ataandikwa jina la ukoo wake kama lilivyo. Lakini pia kwa faida ya wasomaji zipo Koo zingine za kinyakyusa hazianzii na Mwa,mfano Kibonde,Kasulu,Kakuyu n.k ila ni asilimia ndogo.