Nipeni ushauri kutokana na uzoefu wenu katika ujenzi

ABSHAM

Member
Joined
Sep 11, 2022
Posts
24
Reaction score
44
Lengo ni kwamba nahitaji kuanza ujenzi.

Ila mpaka sasa nime save 5ml, ila nina uhakika wa kusave laki 6 kila mwezi.

Nahitaji kujenga nyumba ya kawaida tu iwe na vyumba vinne je naweza kuanza taratibu au niendelee tu kujichanga.

Site ni DSM maeneo ya chamazi.. Nipeni uzoefu wenu wadau
 
Mkuu vyumba vinne kwanza sio nyumba ya kawaida ni kubwa hapo hujaweka vikolokolo vingine kama vyoo, jiko nk.

Ushari.

Hiyo fedha iweke kwenye msingi uukamilishe (kuwa na usimamizi mzuri mana inatosha hasa Kwa Dar bado bei za bidhaa zinavumilika)

Jenga sasa mana sio muda kutakua na ongezeko la ghafla la bei za bidhaa za ujenzi.. sababu ya kuadimika Kwa dollar na msukumo kutoka nje ya Tanzania mathalani vita zinazonukia mashariki ya kati hazita tuacha salama.

weka fedha ya dharura (kulingana na mahitaji Yako) hii isihusike katika ujenzi kabisaaa inaweza kuwa 1 million.

ukiamilisha fedha ya dharura kiasi ulichokua unakiweka Kwa muda mrefu 600k kipeleke site Moja Kwa moja usikiweke Tena.

NB: FEDHA YA UJENZI HAITUNZWI KAMA HUNA KIPATO CHA UHAKIKA

HITIMISHO:
Kujenga ni dhamira na kama unayo utajenga... Kila la kheri mkuuu.
 
Je, naweza kuanza na hiyo 5ml kiongozi
Hujasema 5m hizi unazipata katika kazi, biashara au shughuli yako ni Nini? Ili tukupe ushauri Kulingana na kipato chako.

Kama ni biashara sikushauri kwenda kuzika hizo pesa ulipo ni mbali sana na uhalisia wa unachokitaka. Nina nyumba ya vyumba nne imenicost zaidi 50m vinginevyo uwe unataka nyumba za kiswahili ambazo hazifuati kanuni za ujenzi.

Hebu ona kipato chako 600k x 12= 7.2m. Tufanye assumption utajenga nyumba isiyokamilika, lakini itakuruhusu kuhamia ya vyumba nne kwa 30m. Maana yake una miaka nne mbele ya kukamilisha mradi wako. Ndiposa nakushauri Kama hiyo unayotoa ni sehem ya mtaji usijaribu kuitoa kwa sasa, huenda nyumba hiyo itakufilisi na biashara yakko yote kwa tamaa ya kutaka kuona inaisha. Ujenzi usipokuwa mzoefu na hela za mawazo unafilisi utabaki na nyumba au watoto hawaendi chooni.

Kama ni mfanyakazi na hujui chochote nje ya kazi Basi nenda kazike hizo hela. Lakini Kama ungekuwa mtu mwerevu kwa namna yoyote ningekuambia hizi 5m ukizungusha baada ya mwaka zitakupa 5m nyingine. Iko hivi Kama utaweza kuzalisha faida ndogo tu ya 500k kwa mwezi kutoka kwa hiyo 5 bhasi toa hizo faida ingiza mdogo mdogo kwenye ujenzi baada ya mwaka utakuwa umebakiwa na mtaji na ujenzi unaendelea.

Huu ni ushauri wangu Kulingana na uzoefu wangu ktk ujenzi, biashara mtaani, kazi serikalini. Kila la kheri.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kiongozi shukran sana.. Nime note hii
 
Nimeajiriwa ila pia nafanya biashara japo sijaweka nguvu kubwa katika biashara kwa sababu kiukweli asilimia 80℅ ya muda wangu nautumia kwenye ajira..mshahara wangu ni 1.3ml hyo ni take home baada ya makato na sina marupu marupu yeyote.. Na kwenye biashara kwa sasa nina uhakika wa kutengeneza faida isiyozidi laki 5 kutokana na pesa na muda niliyoweka kwenye biashara yani kiufupi sina muda wa kusimamia biashara yangu mimi mwenyewe.. Na pia nina familia inanitegemea na sio familia ndogo ni kubwa kiukweli.. Umri wangu ni miaka 29 naelekea 30🥲...hivyo nimeandika hapo nina uhakika wa kusave laki 6 kwa mwezi kutokana na majukumu niliyo nayo na pia huwa natoa kiasi flan kila mwezi kuongezea kwenye biashara yangu... Kuna muda huwa nafikiria nifanye kazi kwa Muda wa miaka miwili kisha hela yote niiweke kwenye biashara then niache kazi nipambane na biashara ila akili inakataa na hata familia nikiwagusia hilo hata hawanielewi ila naamini kuna siku nitafanya haya maamuzi... NAHITAJI USHAURU ZAIDI WAKUU
 
Aisee Kama ingekuwa Mimi bado ningeimarisha biashara Kwanza. Kwa sababu hii 5m bado ni chini sana. Ingefika hata 10m ningekushauri Kama una kiwanja kikubwa kaanze na nyumba ili uhamie kwako wakati unapambana na kubwa. Brother ujenzi ni safari ndefu usiingie wakati hujajiimarisha kiuchumi hasa wewe unaetaka kujenga kwa pressure ya kuingiza familia mwisho usipokuwa na vyanzo makini itakuingiz kwenye mikopo kichefuchefu.

Wewe ndie ujuaye maisha yako na kero zako, amua Kulingana chenye faida kwako.

Nimepokea ushauri kiongozi.. Shukran sana
 
Lengo ni kwamba nahitaji kuanza ujenzi.

Ila mpaka sasa nime save 5ml, ila nina uhakika wa kusave laki 6 kila mwezi.

Nahitaji kujenga nyumba ya kawaida tu iwe na vyumba vinne je naweza kuanza taratibu au niendelee tu kujichanga.

Site ni DSM maeneo ya chamazi.. Nipeni uzoefu wenu wadau
Mkuu nyumba ya vyumba vinne ni kubwa sana. Jenga ya vyumba vitatu kimoja self na viwili vya kawaida. Ila kama kipato chako kina mtiririko mzuri jenga hiyo ya vyumba vinne (vitatu self na kimoja cha kawaida).
 
Kwan kutakuwa na tofauti kubwa ya pesa mkuu
 
Back
Top Bottom