Hujasema 5m hizi unazipata katika kazi, biashara au shughuli yako ni Nini? Ili tukupe ushauri Kulingana na kipato chako.
Kama ni biashara sikushauri kwenda kuzika hizo pesa ulipo ni mbali sana na uhalisia wa unachokitaka. Nina nyumba ya vyumba nne imenicost zaidi 50m vinginevyo uwe unataka nyumba za kiswahili ambazo hazifuati kanuni za ujenzi.
Hebu ona kipato chako 600k x 12= 7.2m. Tufanye assumption utajenga nyumba isiyokamilika, lakini itakuruhusu kuhamia ya vyumba nne kwa 30m. Maana yake una miaka nne mbele ya kukamilisha mradi wako. Ndiposa nakushauri Kama hiyo unayotoa ni sehem ya mtaji usijaribu kuitoa kwa sasa, huenda nyumba hiyo itakufilisi na biashara yakko yote kwa tamaa ya kutaka kuona inaisha. Ujenzi usipokuwa mzoefu na hela za mawazo unafilisi utabaki na nyumba au watoto hawaendi chooni.
Kama ni mfanyakazi na hujui chochote nje ya kazi Basi nenda kazike hizo hela. Lakini Kama ungekuwa mtu mwerevu kwa namna yoyote ningekuambia hizi 5m ukizungusha baada ya mwaka zitakupa 5m nyingine. Iko hivi Kama utaweza kuzalisha faida ndogo tu ya 500k kwa mwezi kutoka kwa hiyo 5 bhasi toa hizo faida ingiza mdogo mdogo kwenye ujenzi baada ya mwaka utakuwa umebakiwa na mtaji na ujenzi unaendelea.
Huu ni ushauri wangu Kulingana na uzoefu wangu ktk ujenzi, biashara mtaani, kazi serikalini. Kila la kheri.
Sent from my TECNO BA2 using
JamiiForums mobile app