Nipeni ushauri kutokana na uzoefu wenu katika ujenzi

Mkuu ukitaka ujenzi wewe anza tu hela ikiwa mikononi majanga hayeshi bora ujenge sasa kabla jinsia nyengine ikataka nusu yake.
Ushauri mzuri sana huu umempa!! Ujenzi wa kudunduliza unakula nafasi ya kufanya na mambo mengine ya dharula. Majanga kwa mtu mweusi hayajawahi kuisha
 
Mkuu nyumba ya vyumba vinne ni kubwa sana. Jenga ya vyumba vitatu kimoja self na viwili vya kawaida. Ila kama kipato chako kina mtiririko mzuri jenga hiyo ya vyumba vinne (vitatu self na kimoja cha kawaida).
Hawa ndio wanaotuachia mapagala mjini hapa

Hawataki kuhesabu gharama ma uwezo wao
 
Tafuta ramani kisha utapata makadirio ya mahitaji, anza kukusanya material taratibu ukimaliza jenga kwa awamu kulingana na uwezo wako.
 
Nimeanza ujenzi wa vyumba vitatu(nyumba ya kawaida tu) msingi tu nimetumia mil1.5 nimenunua na tofali za kupandishia hadi lenta mtonyo umekata navuta pumzi

Ningeanza na iyo mil5 kama wewe ingebaki kupaua na bati
 
KUjenga ni timing tu kama unaweza anza kidogo dogo usisubiri upate mamilion vingnevyo hutaweza kujenga anza na msingi kwanza tulia then ukipata ela unaendelea
 
Tukiassume nyumba itakamilika kwa 50m

Kwa hiyo ina maana atahitaji 8 yrs kuimaliza

Basi sio maamuzi mazuri kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…