Salaam wanajukwaa. Jamaa yangu amepatwa na tatizo ambalo yeye mwenyewe halielewi na hata Mimi aliyenisimulia nimeshindwa kumuelewa ndomana nimelileta kwenu. Iko hivi, huyu rafiki ni mtumishi wa umma kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Pamoja na mshahara anaopata anajitahidi kupambana nje yakazi na maisha yake sio mabaya, anajiweza. Tatizo lake limeanza rasmi mwezi July mwaka Jana na limemporomosha kiuchumi vibaya kiasi sasa amechanganyikiwa.
AVIATOR! mwanzo aliponitajia hiki kitu sikumwelewa kwani nilikuwa sijui kabisa.Alijaribu kunifafanulia mwisho nikaelewa nimchezo Fulani jamiii ya betting wenyewe wanaita kandege. Jamaa yangu anacheza huo mchezo na kwa wiki anaweza apoteze zaidi ya laki6!
Anadai amefikia kiwango Cha kuuza mali zake kutokana na madeni aliyokopa nakuyaelekeza kwenye mchezo huo.Tumeshauri njia nyingi zakuacha hadi akaamua kuharibu Simu yake ili asiingie mtandaoni lakini Bado mwamba ametengeneza na amerudi mchezoni.
Ana ofisi flan ya huduma za stationary ila wateja wakitanguliza pesa jamaa anaziweka kwenye kindege analiwa kinachobaki ni kusumbuana na wateja.
Najua betting Ina kula na kuliwa lakini kwa uliwaji huu na Bado anaendelea kucheza nahisi(nahata yeye)anaamini Kuna jambo nyuma.Anasema akishika tu pesa mkononi wazo lakwanza linamjia nikucheza kindege,Zikiisha anabaki na majuto huku akijiapiza hatarudia tena.
Ana mke na watoto,ila kwa Hali ilivyo ndoa ipo mashakani.Nifupishe tu kwakusema jamaa anahitaji msaada wa kutoka kwenye huo mchezo kwani anahisi Kuna mchezo kafanyiwa na sio akili zake.
Wakati Fulani niliingia jukwaa la wazee wakubeti hapa hapa JF nikaulizia ili nijue betting za kindege zinakuwa na madhara kama hayo kwa watu wote au Kuna kitu sio bure.
Uwezo wangu na ndugu wengine wakumshauri aache umeshindikana kwani Jana tu katoka kuliwa laki4 .