Nipepo au ni uraibu? Anaomba msaada

Nipepo au ni uraibu? Anaomba msaada

Huyo jamaa yako ana afya ya akili kuweni makini naye sana.

Kindege kimeshamvuruga.
 
Vishu umeniandama sana skumbili hzi...
Yaaani wewe kila mfano unaohusu mambo ya mishangazi lazima unitag mimi aiseee...😃😃😃😃😃😃

Mkuu mi kwa sasa natafuta mtoto mmoja hvi mbichi anaitwa swaumu..

Huyu mtoto mara nyingi huwa anapenda kuniita mi dady...
Acha kumpotezea muda mtoto wa watu, kuna aunt ananiletea mazoea kitaa hapa, mi sio mambo zangu acha nikugee pande mwanangu .
 
Salaam wanajukwaa. Jamaa yangu amepatwa na tatizo ambalo yeye mwenyewe halielewi na hata Mimi aliyenisimulia nimeshindwa kumuelewa ndomana nimelileta kwenu. Iko hivi, huyu rafiki ni mtumishi wa umma kwa zaidi ya miaka 10 sasa.

Pamoja na mshahara anaopata anajitahidi kupambana nje yakazi na maisha yake sio mabaya, anajiweza. Tatizo lake limeanza rasmi mwezi July mwaka Jana na limemporomosha kiuchumi vibaya kiasi sasa amechanganyikiwa.

AVIATOR! mwanzo aliponitajia hiki kitu sikumwelewa kwani nilikuwa sijui kabisa.Alijaribu kunifafanulia mwisho nikaelewa nimchezo Fulani jamiii ya betting wenyewe wanaita kandege. Jamaa yangu anacheza huo mchezo na kwa wiki anaweza apoteze zaidi ya laki6!

Anadai amefikia kiwango Cha kuuza mali zake kutokana na madeni aliyokopa nakuyaelekeza kwenye mchezo huo.Tumeshauri njia nyingi zakuacha hadi akaamua kuharibu Simu yake ili asiingie mtandaoni lakini Bado mwamba ametengeneza na amerudi mchezoni.

Ana ofisi flan ya huduma za stationary ila wateja wakitanguliza pesa jamaa anaziweka kwenye kindege analiwa kinachobaki ni kusumbuana na wateja.

Najua betting Ina kula na kuliwa lakini kwa uliwaji huu na Bado anaendelea kucheza nahisi(nahata yeye)anaamini Kuna jambo nyuma.Anasema akishika tu pesa mkononi wazo lakwanza linamjia nikucheza kindege,Zikiisha anabaki na majuto huku akijiapiza hatarudia tena.

Ana mke na watoto,ila kwa Hali ilivyo ndoa ipo mashakani.Nifupishe tu kwakusema jamaa anahitaji msaada wa kutoka kwenye huo mchezo kwani anahisi Kuna mchezo kafanyiwa na sio akili zake.

Wakati Fulani niliingia jukwaa la wazee wakubeti hapa hapa JF nikaulizia ili nijue betting za kindege zinakuwa na madhara kama hayo kwa watu wote au Kuna kitu sio bure.

Uwezo wangu na ndugu wengine wakumshauri aache umeshindikana kwani Jana tu katoka kuliwa laki4 .
Anahitaji maombi ili akombolewe...
 
Nikitegemea San mchango kama huu

Nilitegemea San comment kama hii kwani ndivyo wengi tulivyo hapa JF.Mtu anapowasilisha changamot zamtu mwingine inaonekana niyeye ila akieleza mafanikio na utajiri wa mtu mwingine hapo comments zitamhusu mlengwa moja kwa moja.Ningesema Kuna jamaa yangu tajiri Wala usingethubutu kusema huyo jamaa nimimi. Anyways,tufanye nimimi mwenye hyo shida....naomba msaada wako mkuu
BOSSI nakushauri kila siku asubuhi ukiamka anza kusoma machapisho /makala yanayohusu athari za betting.

Kubeti na ukiliwa ni jambo la aibu maana unapoteza pesa hivyo jaribu kumuhusisha mke wako au familia yako,huwenda ukahisi aibu au wakakushauri na hatimae ukaacha huo mchezo.

keep busy/usipendelee kuweka macho yako au kushika simu hovyo jaribu kutafuta vijiwe vya wazee au vijana wanao jitambua ila vijana wengi kwa sasa mishe zao ni kubet.

usijitenge,kaa karibu na marafiki hapa ni jambo muhimu,ila tambuaBetting ni mchezo unaleta madhara katika maeneo ya tofauti mfano Fedha/uchumi,Saikolojia,Mahusiano n.k.

Unachopitia siyo peke yako ni watu wengi wapo kwenye hilo zimwi.

ukweli ni kwamba vijana hatujui tunataka nini ukiwa na elfu 20 utahitaji elfu 50 na kadhalika,hii inakuwa ni tamaa na utumwa,ulaghai.

Hatimae huoni faida pesa yote unarudisha kwa mzungu,unaweza kula leo ila baada ya wiki 2 umerejesha pesa zote.
 
Salaam wanajukwaa. Jamaa yangu amepatwa na tatizo ambalo yeye mwenyewe halielewi na hata Mimi aliyenisimulia nimeshindwa kumuelewa ndomana nimelileta kwenu. Iko hivi, huyu rafiki ni mtumishi wa umma kwa zaidi ya miaka 10 sasa.

Pamoja na mshahara anaopata anajitahidi kupambana nje yakazi na maisha yake sio mabaya, anajiweza. Tatizo lake limeanza rasmi mwezi July mwaka Jana na limemporomosha kiuchumi vibaya kiasi sasa amechanganyikiwa.

AVIATOR! mwanzo aliponitajia hiki kitu sikumwelewa kwani nilikuwa sijui kabisa.Alijaribu kunifafanulia mwisho nikaelewa nimchezo Fulani jamiii ya betting wenyewe wanaita kandege. Jamaa yangu anacheza huo mchezo na kwa wiki anaweza apoteze zaidi ya laki6!

Anadai amefikia kiwango Cha kuuza mali zake kutokana na madeni aliyokopa nakuyaelekeza kwenye mchezo huo.Tumeshauri njia nyingi zakuacha hadi akaamua kuharibu Simu yake ili asiingie mtandaoni lakini Bado mwamba ametengeneza na amerudi mchezoni.

Ana ofisi flan ya huduma za stationary ila wateja wakitanguliza pesa jamaa anaziweka kwenye kindege analiwa kinachobaki ni kusumbuana na wateja.

Najua betting Ina kula na kuliwa lakini kwa uliwaji huu na Bado anaendelea kucheza nahisi(nahata yeye)anaamini Kuna jambo nyuma.Anasema akishika tu pesa mkononi wazo lakwanza linamjia nikucheza kindege,Zikiisha anabaki na majuto huku akijiapiza hatarudia tena.

Ana mke na watoto,ila kwa Hali ilivyo ndoa ipo mashakani.Nifupishe tu kwakusema jamaa anahitaji msaada wa kutoka kwenye huo mchezo kwani anahisi Kuna mchezo kafanyiwa na sio akili zake.

Wakati Fulani niliingia jukwaa la wazee wakubeti hapa hapa JF nikaulizia ili nijue betting za kindege zinakuwa na madhara kama hayo kwa watu wote au Kuna kitu sio bure.

Uwezo wangu na ndugu wengine wakumshauri aache umeshindikana kwani Jana tu katoka kuliwa laki4 .
Yote yanawezekana. Ila...

Ila lakuzingatia ni kwamba huyo jamaa kashakamatwa na uraibu wa betting sio uchawi wala mapepo ni uraibu huo.

Uraibu hata uwe na Akili timamu kiasi gani ukishaingia kwenye 18 za uraibu hesabu umekwisha hakuna cha u-genius wala nini,

tena watu ambao wako vizuri upstairs ndio huwa wananasa katika uraibu wakutupwa.
 
Back
Top Bottom