Nipepo au ni uraibu? Anaomba msaada

Huyo jamaa yako ana afya ya akili kuweni makini naye sana.

Kindege kimeshamvuruga.
 
Acha kumpotezea muda mtoto wa watu, kuna aunt ananiletea mazoea kitaa hapa, mi sio mambo zangu acha nikugee pande mwanangu .
 
Anahitaji maombi ili akombolewe...
 
BOSSI nakushauri kila siku asubuhi ukiamka anza kusoma machapisho /makala yanayohusu athari za betting.

Kubeti na ukiliwa ni jambo la aibu maana unapoteza pesa hivyo jaribu kumuhusisha mke wako au familia yako,huwenda ukahisi aibu au wakakushauri na hatimae ukaacha huo mchezo.

keep busy/usipendelee kuweka macho yako au kushika simu hovyo jaribu kutafuta vijiwe vya wazee au vijana wanao jitambua ila vijana wengi kwa sasa mishe zao ni kubet.

usijitenge,kaa karibu na marafiki hapa ni jambo muhimu,ila tambuaBetting ni mchezo unaleta madhara katika maeneo ya tofauti mfano Fedha/uchumi,Saikolojia,Mahusiano n.k.

Unachopitia siyo peke yako ni watu wengi wapo kwenye hilo zimwi.

ukweli ni kwamba vijana hatujui tunataka nini ukiwa na elfu 20 utahitaji elfu 50 na kadhalika,hii inakuwa ni tamaa na utumwa,ulaghai.

Hatimae huoni faida pesa yote unarudisha kwa mzungu,unaweza kula leo ila baada ya wiki 2 umerejesha pesa zote.
 
Anataka kuwa rubani bila kuusomea🀣🀣🀣
 
Yote yanawezekana. Ila...

Ila lakuzingatia ni kwamba huyo jamaa kashakamatwa na uraibu wa betting sio uchawi wala mapepo ni uraibu huo.

Uraibu hata uwe na Akili timamu kiasi gani ukishaingia kwenye 18 za uraibu hesabu umekwisha hakuna cha u-genius wala nini,

tena watu ambao wako vizuri upstairs ndio huwa wananasa katika uraibu wakutupwa.
 
Hata Mimi nilimuona fala na uzri nayeye mwenyewe Huwa anajiona fala akifikiria yanayomtokea. Issue nikwamba anatokaje huko asiendelee kuwa fala?
Suluhisho pekee ni YESU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…