Sharobaro la jf
JF-Expert Member
- Apr 23, 2020
- 237
- 325
Kiukweli mapenzi yanauma sana jamni acheni tu, kuna mwanamke nipo nae sasa tuna miezi mitatu, tulikutanaga instagram ndipo tukawa tunawasilana hadi baadae tulipoingia kwenye uchumba, bahati nzuri tunakaa mtaa sio mbali mbali, yeye yupo kihonda mimi nipo msamvu na uwa tunakutana mara kwa mara ila sasa hatujaonana mda mrefu zaidi ya kuwasiliana tu kwa simu, sasa kinachoniumiza ni kumuona huyu mtu kabadilika ghafla, inabidi kila siku mimi ndie wa kumuanza kumtafuta, nisipomtafuta yeye wala hanitafuti, nimejukuta mimi tu ndio wa kutetea penzi langu na yeye wala hajali, anaweza kukaa wiki nzima asikutafute hadi umuanze, binafsi nimejitahidi kuwa mvumilivu nikahisi huenda labda ananipima uvumilivu wangu lakini naona kama nakata tamaa, kweli nampenda ila dharau alizoanza kunionyeshea ndio zinanivunja moyo,
Naombeni ushauri?
Naombeni ushauri?