Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Huyo ni mdada na inaonekana alienda huko akiwa na mambo ya Dar. Aliposema Mr akamwambia atazoea tu ni mume wake. Inaonekana mume wake alimsindikiza kwenda huko Mtwara.
 
Nikipata usafiri wangu ndo ntazoea! Usafiri shida sana huku boda boda unamtafuta kwa Tochi.. muda unamuhitaji akuwaishe Hahaha unampigia anakwambia yupo kwenye mashamba ya chunvi😄 yani ni vioja kuna siku hadi nililia
Kumbe una akili za kijiñga, unalilia bodaboda? Ukikua utaona pazuri tuu,
 
Huijui Mtwara ya miaka hiyo kabla ya daraja la Mkapa, Mtwara ya sasa iko juu sana na ina fursa ikiwemo korosho. Kulikuwa na mradi wa maji ya kutoka ndanda nafikiri ambayo si ya chumvi, usafiri kuja Dar ni kugusa tu.....unataka nini zaidi dada.​
Hafahamu hayo, nimeishi huko miaka ya 1998 hadi 2002 ingekuwa ni yeye sijui angesemaje!!! Analalamika Mtwara ya 2025!!!
 
Vingi alivyosema ni uongo tatizo lake haijui mtwara na hajatembea, eti anasema hadi huduma za kifedha ni shida!. Huyu alikuja na dar es salaam yake kichwani
Sehemu yoyote kama sio mwenyeji kupata huduma lazima uteseke, hata Dar waweza kutembea unatafta huduma ya mpesa au mtandao mwingine lkn kila kibanda unafikia utaambiwa sina float, labda kama unatuma au kutoa chini ya laki 1, mpaka uje kumfahamu mwenye float ya uhakika ulishachoka.
 
Hilo kwenye kuloga hilo huenda Ni kweli
 
Sema ndugu zetu wa Daslamu mnakuaga na mikwara. Huko Dar sehemu classic za kuspend na kuishi zipo kibao lakini tunabanana uswahilini. Huko MaKFC sijui MacDonald kufanyaje Serena sijui hatuwaoni tunakutana kwa Mama Amina Kurasini tunagonga msosi wa buku mbili maisha yanaenda.

Mkifika mikoani sasa, Maghorofa yako wapi? Sehemu za kijanja za kula bata wapi?

Huwa najiuliza hayo maghorofa tukiwaonesha yatawasaidia nini nyie wakazi wa Tandale? Umeshindwa kwenda sehemu za kijanja Dar utaweza huku mkoani?

Dar na Mwanza yote ni majiji, ila utavyoishi Dar sivyo utavyoishi Mwanza. Songea ni nyumbani kabisa ila sijawahi kukosa usafiri hata nikirudi maskani saa tisa usiku.

Kama mnavyosema ukiwa na pesa Dar hupotei ndivyo ilivyo huko mikoani. Huko population sio kubwa hakuna boss mwenye akili timamu aache gari inazunguka muda ambao research yake imemuambia hakuna abiria. Kuna mtu anaweza kuacha daladala yake barabarani muda ambao abiria ni wawili?


Mwisho, ipo hivi jiji la Dar ni jiji la kibiashara wakati huko mikoani biashara tunaweza kuzipa asilimia 30 hadi 40 mzunguko wa pesa upo kwenye kilimo.

Kafungue frame hapo Songea utasema biashara ngumu mzunguko mdogo lakini angalia takwimu za TRA zimeirank Songea namba ngapi katika halmashauri zinaingiza mapato makubwa. Unaweza ukaguess pesa zinatoka wapi?

Respect kwa watu wa mikoani wanajua kubadilika kutokana na mazingira nafikiri ndio watu wenye exposure kubwa zaidi kutokana na kusafiri mara kwa mara.

Ila nyie ndugu zetu ifike mjitafakari, mkishindwa kusoma mazingira na kuendana nayo sio tu utashindwa kuishi Mtwara bali hata siku ukienda London utapaona pachungu.
 
Dogo, mbona unakuwa muongo hivi, ni Mtwara gani uliyoenda wewe?
 
Ondoa fikra za "Dar ndo kila kitu" utazoea tu. Binafsi nafikiri mapungufu uliyoyaona ndo fursa kwako. Kama kuna upungufu wa vyakula, fanya biashara ya vyakula ili ujiingizie kipato, kama huduma za kifedha ziko chache basi fungua biashara za huduma za kifedha (M-PESA, Airtel money, Mixx by yas, halopesa, CRDB, NMB, equity, exim n.k) ili ujiingizie kipato cha ziada. Badilisha mtazamo, hizo changamoto zilizopo zibadilishe kuwa fursa.
 
Safi. Mawazo mazuri. Nitayafanyia kazi inshallah
 
Huna akili
 
Dogo, mbona unakuwa muongo hivi, ni Mtwara gani uliyoenda wewe?
Tutumie picha ya kituo kikuu cha mabasi hapo mtwara mjini..
Mtwara sijafika nimeishia Lindi tu , ila kwa barabara ile inaonesha huko ni mbwinde huwezi kufananisha hata n Njombe/ Mafinga
 
Tutumie picha ya kituo kikuu cha mabasi hapo mtwara mjini..
Mtwara sijafika nimeishia Lindi tu , ila kwa barabara ile inaonesha huko ni mbwinde huwezi kufananisha hata n Njombe/ Mafinga
Hana akili huyo anatetea kwao
 
Huu uzi umenifanya niamin wamakonde n wabishi na wanatabia za kihaya tofauti n shule n ufukara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…