Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Barabara ya Mtwara - Dar ni nzuri tu ila kuna baadhi ya sehemu kuna hitilafu kidogo haswa baada ya kuja hizi mvua za karibuni
Inategemeana ni nzuri kulinganisha na ipi...
Mm nimeishia Lindi, kwa kweli kibara bara n chembamba mnoo, rafu baadhi ya maeneo
 
Tangu nifike Mtwara miezi kadhaa iliyopita, mambo ninayokutana nayo sikuyategemea kabisa. Picha inaanza wakati nakuja kuripoti, ile nafika bus stand ya Mkanaredi naambiwa hapa ndiyo Manispaa ya Mikindani na ndiyo mjini.

Sikuamini! Mr. akanitia moyo na kuniambia nitazoea mazingira. Nikasema, "Sawa, maadam ni mjini, kitu cha msingi ni huduma."


Tukachukua lodge (na lodge zenyewe maji hayatoki, wanategemea maji ya mvua... yani ni tafrani tupu!). To cut a long story short, maisha ya Mtwara ni magumu kwenye nyanja zote! Maji ni shida, bei ya vitu iko juu sana kuliko hata Dar es Salaam, na miundombinu hafifu inafanya usafiri kuwa wa tabu.

Huduma za kifedha ni chache na ziko mbali, yani kulala au kushinda njaa ukiwa na hela mfukoni ni kitu cha kawaida sana hapa!

Ikifika saa 3 usiku, barabarani ni nyeupe kabisa—huoni mtu, na maduka yanafungwa mapema. Viwanja vipo, lakini The Shooters ndicho kiwanja pekee nilichoelewa, na nikiwa hapo najihisi kama niko Dar es Salaam.

Serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa!
Acha kazi urudi dar si unaona raha kukaa dar
 
Ukiona mkoa watu wake wanavaa manguo marefu marefu na makobazi, jua hapo hamna kitu. Fanya utafiti utagundua. Muarabu ameharibu sana hiyo kanda ya huko.
 
Back
Top Bottom