Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Mimi nilipangiwa mamba, moshi vijijini, kabla sijafika huku nilifikiri ninaenda sehemu iliyoendelea kuliko zote Tanzani.. kutokana na sifa za mwana JF, Lwambo Makiadi, kwamba moshi ni kama ulaya.
1. Hakuna maji
2. Hakuna umeme
3. Hakuna mtandao wa simu au internet
4. Barabara ni mbovu kamaza ngombe
5. Hakuna watu...vijana wamelewa muda wote
6. Chakula hakuna
7. Mbunge ni kama hawana
😂😂😂😂😂😂
 
Dada, mm naona huna pesa za kutosha, peaa unazo ila sio za kutosha!!
 
Tangu nifike Mtwara miezi kadhaa iliyopita, mambo ninayokutana nayo sikuyategemea kabisa. Picha inaanza wakati nakuja kuripoti, ile nafika bus stand ya Mkanaredi naambiwa hapa ndiyo Manispaa ya Mikindani na ndiyo mjini.

Sikuamini! Mr. akanitia moyo na kuniambia nitazoea mazingira. Nikasema, "Sawa, maadam ni mjini, kitu cha msingi ni huduma."


Tukachukua lodge (na lodge zenyewe maji hayatoki, wanategemea maji ya mvua... yani ni tafrani tupu!). To cut a long story short, maisha ya Mtwara ni magumu kwenye nyanja zote! Maji ni shida, bei ya vitu iko juu sana kuliko hata Dar es Salaam, na miundombinu hafifu inafanya usafiri kuwa wa tabu.

Huduma za kifedha ni chache na ziko mbali, yani kulala au kushinda njaa ukiwa na hela mfukoni ni kitu cha kawaida sana hapa!

Ikifika saa 3 usiku, barabarani ni nyeupe kabisa—huoni mtu, na maduka yanafungwa mapema. Viwanja vipo, lakini The Shooters ndicho kiwanja pekee nilichoelewa, na nikiwa hapo najihisi kama niko Dar es Salaam.

Serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa!
Umeshazoea purukushani za Kariakoo, Mbagala Rangi tatu, Tandika n.k wewe. Tulia upate New Experience ya Maisha.
 
Mikoa yote inafanana Tu kama Akili yako umeipanga izoee mazingira utaweza kuishi popote
Unataka uishi kama upo DAR hapo ni kujidanganya, TANZANIA bado Sana hasa Huko mikoani hata hiyo DAR nayo imechoka sanaa sioni utofauti na mikoani tu
Dar kuna fujo nyingi kuliko Mikoani. Fujo mojawapo ni watu kupanda daladala kwa kugombania hadi wengine wanakosa ustaarabu wanaingia ndani kupitia dirishani.
Mengine mtaongezea wazoefu wa hapo Bongo.
 
Kusema mtwara maji shida kwamba wanategemea maji ya mvuo ni uongo

Usafiri kusema shida uongo usafiri mkubwa wa mtwara ni bodaboda popote unapo enda ni buku up buku jero kwa usafiri wa haraka

Viwanja vipo vingi sana ujatembea kuna leopard pili msimbati ukienda utatamni kwenda kila siku

Chakula kuwa shida ni uongo sema huna hela ni kweli vitu viko juu sana ila pesa yake kuipata sio ngumu kama unajua kutafuta pesa ila kama unategemea mshahara mtwara hapakufai toka

Kusema saa tatu watu hamna ni kweli watu wa mtwara wanapenda kutulia sana hasa nyakati za usiku mwisho saa moja kutokana na alshababu kuvamia wanaotoka msumbiji ndio maana now mtwara ukitaka kutembea tembea na batua ya utambulisho wa mtaa wako ukikutwa na polis usiku unabebwa kama ulivyo unahisiwa wewe ni alshababu so watu wanakaa majumbani kwasababu
Wewe ndio mjinga wa mwisho, unatetea ujinga huu wa huo mkoa?. Huo mkoa umelaaniwa na watu wake ni wavivu sana ndio maana kila kitu kinakwama.
 
Wewe ndio mjinga wa mwisho, unatetea ujinga huu wa huo mkoa?. Huo mkoa umelaaniwa na watu wake ni wavivu sana ndio maana kila kitu kinakwama.
Asante😁
 
Tutumie picha ya kituo kikuu cha mabasi hapo mtwara mjini..
Mtwara sijafika nimeishia Lindi tu , ila kwa barabara ile inaonesha huko ni mbwinde huwezi kufananisha hata n Njombe/ Mafinga
Barabara ya Mtwara - Dar ni nzuri tu ila kuna baadhi ya sehemu kuna hitilafu kidogo haswa baada ya kuja hizi mvua za karibuni
 
Back
Top Bottom