Nipo njia ya panda, Japan..............dah!

Nipo njia ya panda, Japan..............dah!

unasubiri yesu akuletee neema mkononi eeh
nenda ukaanze kutuletea magari wakikuuliza waambie unatafuta hela ya kijikimu wengine waulize wenzako marekani walienda na nini na wako wapi sembuse weye una mtaji wa kununua magari ya doleer 300 uje kumpiga pdidy doller 2000..ama unaitaji chozi la inzi uamini neema imekudondokea
 
Mimi najiuliza sana hivi vijana wetu huko UDSM hawafundishwi kuanalyze events? nini maana ya elimu? KWeli mdogo wangu hukuingia darasa la DS ambalo ni basic kwa wote na maengineer wakiwemo? suala la exposure, international experience, networking, opportunity nalo huna idea nalo? unaongelea laki 6 ambayo hata muuza genge mbunifu asiye na elimu ya sekondari anatengeza?

Ninasikitika graduate kuuliza swali hili? au ndio elimu yetu ya kudesa inacreate fear na kupeana ajira kwa kujuana kunaleta hofu sana kuwa nikitoka na anayenitegemeza akiondoka ndio nimekwisha?
Jamani elimu lengo lake ni kutuwezeshwa kupambana na mazingira tuliyonayo, elimu huondoa hofu , elimu hujenga ujasiri ambao unaweza kusema , I dare to do it.

Nakushauri ufanye tathmini wewe binafsi na kupambanua yajayo kutokana na mabadiliko ya teknolojia,uongozi, mtandao kisha weka vipimo vyako mezani na angalia kazi ya laki sita inakuwezesha kukua career wise au elimu na ubunifu uliopata kwenye nchi ya teknolojia ndio muhimu. Yakupasa uelewe dhana hizi mwenyewe na siyo mtu kukuamulia ndio utapata mwamko na ari ya kutenda utachoamua kwa uthabiti na si vinginevyo.
 
Halafu naona missing link katika maelezo yako unasema kuna full sponsorship japan kwa october 2011 na mchakato wa kuwa enrolled mwisho december. Clearly naona bado hujawa admitted bado na kama maombi ya admission ni kwa mwendo huu basi kuna shida katika kupata hiyo scholarship. NAkushauri ujizatiti katika uandikaji wa maombi ya scholarship na kujieleza.
Good luck
 
Jamani nipo njia ya panda.Kuna full sponsoreship kwenda kusoma masters Japan, course: Nucleur Enginering, mmi nime graduate pale udsm, Electro-mechanical engineering, NILIMALIZA MWAKA JANA, nafanya kazi nalipwa 600,000/= kwa mwezi. nahisi kwenda huko ni kupoteza muda kulingana na hali harisi ya tanzania kwenye sector ya nucleur, naomba michango yenu. Program inaanza mwakani october.mchakato wa kuwa enrolled mwisho ni december 10, 2010.Wasiwasi wangu ni kwenye ajira. Nifungueni macho jamani kama yamefumba

600,000? ndio inakufanya uwe njia panda? yaani wewe unachohofu ni kusoma nuclear power kwakuwa Tanzania hutapata kazi, and what if ukafanya vizuri huko japan na ukapata kazi hukohuko? what if ukakutana na opportunity nyingine huko japan say ukawa mfanyabiashara, mi naona wewe unasumbuliwa na Tatizo la uwoga, let me tell you something: If you are not willing to risk, you can not grow; if you can not grow, you can not become your best; if you can not become your best, you can't be happy; and if you cant be happy then what else is there (LES BROWN). Dogo, hizo opportunity huwa haziji mara mbili njoo huku ufunguke macho na matongotongo yakutoke.
 
Look outside the box bana, msomi mzima unakuja na kaswali kakitoto hivyo. Wewe endekeza hako ka laki sita udhani umefika!
 
Nakushauri songa mbele na shule, sasa hvi degree moja ni kama form six, every one is having first degree, usijekujutia hiyo nafasi. Watu wengi tunatafuta scholarship
 
Hebu nenda bwana mie nikajua unalipwa milioni sita kumbe laki sita..
Hizi kazi zipo ukirudi utazikuta
 
Nenda kasome ndugu yangu. Migodi mingi sana inafunguliwa hasa ule wa songea wa Uranium na mwingine unatarajiwa kufunguliwa sehemu za Bahi Dodoma katika siku za karibuni. Nenda kasome, hela unayolipwa ni hela ayayolipwa kuruta wa kushuka mgodini kule kahama.
Naamini ipo siku tutakuwa na kitengo cha kiini atomi hapa Tanzania na uwezekano mkubwa ni watu kama nyinyi kushika vitengo hivyo.
Hongera na mshike elimu usimwache aende zake.
 
Mimi nilisoma Dar Technical College nowdays Dar Institute of Technology; kuna wakati miaka ya nyuma wale waliyokuwa wanasoma Electronics walidharauliwa sana na kuambiwa watakuwa mafundi redio mitaani. Kwana ajira zilionekana ni TTCL na RTD tu. Lakini miaka iliposonga wale waliyokuwa na taaluma ya Electronics kwa level hiyo tu ya FTC walitafutwa. Nenda kasome kwani mambo yanabadilika.

Vile vile unapotafuta taaluma usifikirie kuajiriwa tu; kwa nini usifikiriwe kujiajiri (kutengeneza kinu chako cha nuclear), inawezekana it's a matter of determinatiom.
 
Du kaka laki sita ya kibongo ndio inakufanya usiende soma,dunia siku hizi ni kijiji kaka ukiwa na sifa utafanya kazi mahala popote duniani,tena unapelekwa na mwajiri wako kwenda kufanya kazi,si umeona hata hapa bongo tuna wanaijeria ,waingereza n.k na ni vivyo hivyo hata kwenye nchi nyingine,ukiwa mweledi katika taaluma yako kazi utafanya popote pale kwenye hii sayari
 
hongera sana kwa kupata nafasi hiyo. mimi nakushauri usiangalie hali ya sasa ya hapa kwetu, jaribu kufocus miaka kadhaa ijayo. unaweza ukawa miongoni wa wataalamu wa mwanzo kabisa wa nuclear hapa tz. na pia unaweza ukapata opportunity kufanya kazi nje ya nchi. Lakini zaidi sana inategemea malengo yako, finally unataka kufanya nini.

Na kina Dr. Mohamed Gharib Bilal na Dr. Mohamed Tulli, watakuwa kina nani? ikiwa huyu atakuwa katika waTanzania wa mwanzo? mwambie kweli, atakuwa mmoja wapo, ajiendeleze kimasomo, hao wawili niliokutajia wote ni ma nuclear physicists wenye ma Phd. na wapo wengine kibao wenye masters na pia Phd, wanaajiriwa nje ya TZ kwa sasa.
 
Dogo changamka , kuna wenzio huku wanatafuta sponsorship hata za kwenda kusoma performing arts. At a time upo huko Japan unatakiwa uwe mjanja wa kutafuta Links ktk Taasisi za kimataifa zinazojihusisha na hiyo fani hata ukafanyie research kwao nili ukimaliza unakuja kutimiza wajibu wa hiyo scholarship yako bongo then unaangalia mambo megine.
SONGA MBELE JOMBAAA.
 
jamani nipo njia ya panda.kuna full sponsoreship kwenda kusoma masters japan, course: Nucleur enginering, mmi nime graduate pale udsm, electro-mechanical engineering, nilimaliza mwaka jana, nafanya kazi nalipwa 600,000/= kwa mwezi. Nahisi kwenda huko ni kupoteza muda kulingana na hali harisi ya tanzania kwenye sector ya nucleur, naomba michango yenu. Program inaanza mwakani october.mchakato wa kuwa enrolled mwisho ni december 10, 2010.wasiwasi wangu ni kwenye ajira. Nifungueni macho jamani kama yamefumba


kabebe kitu hich mwana kisha rudia iran au norh korea; unafanya kama hujui wapi kuna deal!!!!
 
kaka nakupongeza kwa kupata hiyo nafasi..bahati hairudi mara mbili..njoo usome,ubadirishe mawazo na upate challenge mpya za maisha..bongo ni bongo tu...pesa unayoripwa tz kwa mwezi hapa unauwezo wa kuitafuta na kuipata ndani ya siku 5.acha uzembe wewe!..soma alama za nyakati ufungue milango ya kwenda kufanya kazi nchi nyingine nakwa maslahi zaidi.YOUR WELCOME MAN!
 
Kuna wengi sana wamesoma na hawapo nchini.................. NENDA KASOME Tshs. 600,000/= si kiasi cha kutaja, ni kdogo mno. Inaonekana unajilinganisha na WALIMU WA JK....!!!!

SWALI KWAKO.................. kinachokufanya usite ni hizo Tshs. 600,000/= au hali harisi ya Tanzania kwenye sector ya nucleur..????

nilivyomtafsiri mimi ni kua anawasiwasi na ajira kutokana na secta ya nuklia hapa TZ, lakini ndugu yangu ushauri wa haraka hapo ni ukasome. hizo 600,000 ukirudu utazikuta na utakua nazo + master ya nuclear. pia sio lazima kua uafanye kazi tz, lakini pia imagine leo wanahitajika watanzania wenye sifa hizo, je wapo/ kam wapo ni wangapi.
To me its a golden chance i couldnt hestate to take.
 
Back
Top Bottom