Nipo Nyamisati, nimeambiwa nilale siku mbili ndipo nitapata usafiri wa kuelekea Mafia

Nipo Nyamisati, nimeambiwa nilale siku mbili ndipo nitapata usafiri wa kuelekea Mafia

Fene

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2021
Posts
2,824
Reaction score
4,447
Habari wanabodi,

Leo nimefika hapa Nyamisati mida asubuhi nimeambiwa tiketi nimeshakosa napaswa nisubiri hadi Jumatano au Alhamisi ndipo meli itatoka tena kuelekea Mafia.

Hiyo bado haitoshi kuna watu ambao wamebahatika kukata tiketi leo wao wameniambia wana siku ya nne tokea wafike hapa, usafiri ni shida.

Inasikitisha sana na gharama za maisha zilivyo juu mtu anafika hapa bandarini anaambiwa anapaswa asubiri siku kadhaa ndipo asafiri.

Na hili pia mkaliangalie.

Nawasilisha
 
Kwamba meli ni moja, au abiria ni wachache, so inabidi kuwasubiria hadi wajaze Chombo?
 
Pole sana, Mafia nimeanza kusikia shida ya Usafiri muda mrefu mno, sijui kwanini hawawezi kutatua hili shida.
 
Kwamba meli ni moja, au abiria ni wachache, so inabidi kuwasubiria hadi wajaze Chombo?
Meli kwasasa zipo mbili ila ndo wamejiwekea hivyo route mara mbil kwa wiki. Na sio kusema abiria wachache coz wanaoachwa ni wengi sana.

Sababu kuu ni meli iliyo official kabisa kwaajil ya Mafia ambayo ni Mv. Kilindoni ni mbovu ambayo ilikuwa inafanya route kila siku.
 
Vipi mmbu hapo umewaonaje

Hivi mv potwe na mv jubini bado zipo

Ova
 
Back
Top Bottom