Nipo single, haya ni Matumizi yangu ya wiki moja - nipe ushauri

Mimi nikipiga mahesabu najionaga fala kweli maana matumizi ni makubwa sana.
 
Hapo nimekupata kiongozi kwani umeeleza kwa kina kabisa na kwakweli sioni kama kuna ufajaji wa pesa zaidi ya matumizi ya msingi

Vipi upo serikalini cyo? Kazi gani km hutamind?... Ikiwa ni private unaweza kuwa na wasiwasi sana lkn kama gvt siyo presha kihivyo (kwa maana ya job security)

Hata hivyo kuwahi kujiwekeza mapema ni jambo la msingi uliofanya.km unaishi kwako hupangi nyumba, unapangisha una walau taxi inapiga kazi hapa unabaki kushusha pumzi tu

With salary of 1.5M na miradi hiyo mingine na bila wasi wasi uko mikono salama kabisa nothing to fear mkuu

Umenichekesha mkuu hapo kwenye vimichepuko kwamba havipati chochote[emoji23][emoji23]... Ila show siyo ya kitoto so lazma vikutafute tu vynyewe[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nahisi amechanganya matumizi ya mwezi na week... kama kweli kila week anatuma hiyo hela kwa ndugu na kwa take hom ya laki 5 basi atafeli
 
Hapa tupo pamoja mkuu...
 
Boom!!Bibi yako wa Muleba kateguka nyonga,mdogo wako kawekwa ndani.

Waafrika hatuna bajet tumelelewa kwenye extended family.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]kumbe haya mambo yapo kila sehem.
 
Nina miaka 11 sijawahi toa sadaka!!

Ondoa sadaka kwanza, mana unalisha walioshiba!!.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Jf Ina vituko sana.
Walioshiba ndio watu gani hao au unamaanisha watu kama akina gwajima?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Piga mahesabu uone utaanza kujisemea "nilikuwa naibiwa sana" kama mkemia wetu wa zao la mtwara
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
mwache tu ampelekee Mzee wa upako siku akienda kuhojiwa anasema wahumini masikini ni wapumbavu[emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Halaf baada ya hapo hawashtuki bado wanaendelea kupeleka tu yaani duniani Kuna watu ni misukule
 
Ukila kwa mama ntilie na bar kila siku uta average 6000 kwa siku, kwa wiki ni 42,000 kwa mwezi ni 168,000. Hayo mengine sijui.
 
Sadaka:-
25, 000 ndo nimetoa direct
50,000 ni kwa watu wenye shida zaidi ya mimi
Hao watu wenye shida zaidi yako wewe unawaokota wapi?
Au hao ndio wanakutafuta wewe kila siku/wiki?
Hata hao akina Bakhresa na Mo dewji hawapeleki kila siku sadaka.
Wewe kwa utajiri gani ulionao hadi uwapangie bajeti ya kila siku watu wa kuwapa hela?
 
Kweli jitathmini, usawa huu ukiwa unabajet kubwa sana hutaweza kufanya maendeleo mengine.

Note; Nna mke kwahyo vitu k.m maharage,mchele, dagaa, sukari, unga, mafuta nanunua jumla na sio rejareja huwa inasaidia kupunguza gharama.
Hata mm mkuu huwa nafanya hvyo na mke wangu.
Yaani najaza mazaga yote kwenye friji na baada ya hapo nafanya kuongezea tu kila wiki.
Unashangaa wiki nzima natumia elfu 50 tu na naenjoy sana yaani full masamaki,manyama na makuku kwenye friji plus mboga za majani hadi raha.
 
Mkuu maisha yako ya aina nyingi sana.
Na take home ya laki 5 sio ya kubeza ni hela standard kibongo bongo.
Yaani hapo amewazid walimu,mapolisi,makarani wa halmashauri.
Sasa kuna haja gani ya kucheka mtu mwenye uhakika wa laki 5 kwa mwezi eti jwa vile una mshahara wa 1.5m.
Tukianza kufanya comparison ya mishahara humu mbona hata hicho kimshahara chako Cha 1.5m ni kidogo sana.
Atakuja mwingine atakwambia 1.5m hata kwa chakula tu haimtoshi na atakucheka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…