Nipo single, haya ni Matumizi yangu ya wiki moja - nipe ushauri

Kwa mwezi ni laki 9.
Bado kuna dharura, gesi , bills za maji na umeme.
Mchele na nyama, huwezi pika robo tuu kwa wiki.
Andaa 1M kila mwezi.
Mwambie aache ujinga.
But amesha declare kwamba yupo single au unahisi ni Player boy
 
wale wapiga ndefu na wala kambale waliochina km ndugu yangu kiduku lilo hapa wanataman sadaka ungewapa wao
 
Budget lazima ijadiliwe kabla ya kupitishwa, yako imejadiliwa na kuidhinishwa na nani. Lake ni pia tujulishe kipato chako ili tulinganishe.
 
Mkuu hebu tupe uzoefu wako wa bajeti na hiyo family upoje kuna kitu tunaweza jifunza pia from you
Aisee bro;
Umeme 40000 kwa mwezi
Maji 30000 kwa mwezi
Mikate 40000 kwa mwezi
Sukari 56000(25kgs)
Cooking oil 30000 (sunflower 10lts)
Blue band 8000 (2kgs)
Sabuni ya unga 14000 (3.5kgs)
Sabuni ya mche 29000
Nishati mkaa 60000
Nishati gas 54000
Chumvi 2000
Mboga za majani mix 15000
Matunda mix 30000
Kingamuzi/cable 15000
Sadaka Mimi 20000
Sadaka wife 20000
Sadaka watoto 5 25000
Sadaka dada 6000
Nguo za watoto 1000000 mwaka
Viatu 600000 mwaka
Mavazi mke 500000 mwaka
Mavazi mimi 200000 mwaka
Matibabu mtoto 1 tu 50400 bimabinafsi wengine bima ya kazini
Karo mtoto kwanza 1900000
Karo mtoto pili 1115000
Karo mtoto tatu 800000
Karo mtoto nne 800000
Mtoto tano 000000
Fuel 200000 (kwa mwezi
Mshahara wa Dada 50000
Tunamhudumia Dada kila kitu Matibabu,nauli zake, sadaka,Pads na nguo
HIYO BRO NDO BUDGET YANGU Tena kwa uchache sana kumbuka mimi ni muumini mzuri wa castle lager kwa wastani 5beers kwa siku mambo ya kidinda Konyagi ya Kati 8000 inanuhusu au kale kadogo 4000
Pia kutimoto mara moja moja kwa familia ni lazima,siku ya kutoka out mara kwa mara jumapili hasa sehemu zenye michezo ya watoto
Nb:mke ni mjasiliamali mdogomdogo pia nina nyumba mbili za ziada napangisha 8000000 zote pamoja kwa mwaka tuna kitexie angalau kinalaza 20000 kwa siku. Mshahara baada ya makato 1.5 but bado kuna extra allowances.
 
Kwani ameandika kwamba hiyo sadaka anapeleka kanisani???
Kwan nani kaasema anapeleka kanisani....

Zingatia kula kabla haujavuta... Ukikosoa ujinga jiandae na kuuepuka ujinga mdogo mdogo.
 
Hata vitu vingine nimesahau
Mchele kutokana na ukubwa wa familia yangu uwa najitahidi kuweka magunia 6 mpunga ndani kila mwaka wa msimu wa mpunga ambapo gunia moja halizidi 40000
Pia naweka gunia moja la mahindi
Maharage gunia moja
Dagaa hata nusu debe kwa mwezi.
So nyama tunatumia 1kg siku ikisukumwa na mboga za majani na dagaa
Samaki ni mlo mbadala wa nyama samaki 40000 wanatutosha kwa mwezi.
Bro bado hapa kuna kusaidia ndugu na marafiki.

Nb hakuna nililofake katika matumizi haya ila kuna vitu vingi nitakuwa nimesahau.
Naomba pia ushauri japo mie naona sina namna ya kukwepa majukumu haya kwa familia yangu pendwa
 
Hiyo bajeti ni kubwa mno unaweza ukaishi kwa bajeti ndogo tu na wewe ukawa na maisha mazuri tu poromoa hiyo bajetibyote ukija hapa isizidi laki moja kwa mwezi
Inatakiwa aoe,au kama vp muonee huruma kakae nae mwezi tu Dada angu,huyu hajielewi eti sadaka 75,000 kwa week kwa mwezi inakuwa 300,000 na hapo ukute anakaa chumba kimoja
 
nadhani alisema mafala
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hatari lakini salama
 
Kwa hiyo kila wiki unanunua nguo! Hizo nguo ni aina gani nepi au pampas!?
 
Asante bro nami uwa najiuliza sijui ingekuwaje kama ningelioa kabla sijajenga anyway uwa nafurahi kuwaona wanangu wakiwa na furaha siku zote ila siku ukiwa na familia jifunze kununua mazagazaga ya home kwako kwa whole sales make hivi vitu vya rejareja sijui kilo mbili za mchele nk zinaumiza sana japo pia inategemea na aina ya mke ulienae na binti wa kazi make kuna wanawake ambao kadri unavununua vitu kwa jumla ndivo pia wanavokuwa na matumizi ya vyakula hovyo,siku ukianza kuona mbwa koko kwenye jalala lako home chukua hatua jua wameanza uharabifu wa chakula.
Raha ya kununua kwa wholesale unapata hata angalau ka muda ka kunywa castle baridi bila mawazo.
But sukari au mkate umeisha castle utakuwa unaubaka moyo wako kwa mawazo
 
Pia weka shemela wa jirani kwenda nae gest kwa sababu kumleta kwako ni noma.
Kwa mwezi ni laki 9.
Bado kuna dharura, gesi , bills za maji na umeme.
Mchele na nyama, huwezi pika robo tuu kwa wiki.
Andaa 1M kila mwezi.
Mwambie aache ujinga.
 
Investment muhimu. Ila katika budget weka na debe la viazi mviringo.mara moja moja chips mayai. watoto wanapenda sana chips. unga WA ngano kwaajili ya kupika maandazi na chapati hasa siku za weekend
Kaka vyote nafanya ni kwamba nimesahau kuandika wewe tena kiepe kwa watoto,weekend wanangu uwa tunahakikisha wanakula vyakula tofauti na walivokula shule week nzima, kuanzia breakfast,lunch mpk dinner.Uzuri sikupenda watoto wangu kusoma boarding wakiwa wadogo,so kila siku ninaonana jioni na weekend zote nashinda nao.
Asante kaka kwa mawazo mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…