Katika harakati za kitaifa za kuokoa elimu yetu ya Tanzania,niko tayari kufundisha BURE masomo ya ziada ya Sekondari kwa kidato cha nne. Mimi si Mwalimu kitaaluma....ni Mwanasheria. Lakini,niko tayari kuongeza nguvu hasa katika Shule za Kata. Ratiba zangu zinanipa nafasi siku ya Jumamosi tu kuanzia asubuhi.
Niko tayari kwa kuanzia Mkoa wa Pwani Wilaya yangu ya Kibaha au Mkoa wa Dar es Salaam Wilaya niishiyo ya Kinondoni. Nawaombeni wenzangu wenye uwezo kama mimi mniunge mkono.Malipo nitayapata kwa Mungu.Angalau tupunguze tatizo la upungufu wa Waalimu. Silengi kudharau Walimu waliopo...nalenga kuimarisha na kuongeza nguvu.Matatizo mengine nayo yataisha taratibu.
Masomo niyawezayo kufundisha ni ya Historia,Kiingereza,Kiswahili,Jiografia na Siasa. Wakuu wa Shule,wasilianeni nami kwa:
Simu: 0713 111171 au Imaili:
pemselewa@hotmail.com
Karibuni tuiokoe elimu yetu