Uchaguzi 2020 Nipo tayari kukabiliana na Mathayo David au Angela Kairuki Ubunge Same Magharibi

Uchaguzi 2020 Nipo tayari kukabiliana na Mathayo David au Angela Kairuki Ubunge Same Magharibi

justine lowasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
727
Reaction score
794
Wakuu Wasalaam!

Natumai mnaendelea vyema na Ujenzi wa Taifa letu tukufu. Leo napenda kuwajulisha rasmi azma yangu ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Same Magharibi kwa tiketi ya Chama Changu cha CHADEMA .

Mimi Fredrick Justine ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwenye kadi ya uanachama namba 222111 nilitangaza nia hiyo tangu tarehe 20 March 2020 kwakumuandikia barua katibu wa Kanda ya Kaskazini kama utaratibu wa Chama ulivyotuelekeza.

Katika barua yangu, nilimjulisha katibu wa kanda kwamba,

“Nimefikia uammuzi huu baada yakujipima na kuona natosha kuwatumikia ndugu zangu wa Same na umma wa Watanzania, huku moyo wangu ukiwa umejaa shauku kubwa nikitamani kuiona Tanzania, nchi tuipendayo kwa moyo wote inapata ustawi na kuendeleza matamanio, matarajio na ndoto za watu wake, kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa kwa ujumla"

Pia niliendelea kwa kumuandikia katibu wa Kanda.

“Katika kuwapatia maendeleo endevu wananchi wa Same yatupaswa kuwa na Taifa linalosimamia uhuru na haki za watu, utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari,na demokrasia ya kweli inayowapa wananchi mamlaka kuhusu mustakabali na mwelekeo wa nchi kupitia chaguzi za viongozi zilizo huru na za haki.

Pia, nilieleza namna nilivyojipanga kushirikiana na viongozi wengine watakaochaguliwa kuunda serikali katika kusimamia utatuzi wa kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa Same katika sekta ya Afya, Elimu, Kilimo, Ufugaji na utatuzi wa migogoro ya Ardhi baina ya wafugaji na wakulima inayowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Same Magharibi.

Mbali na mambo hayo pia nilieleza endapo ntapata ridhaa ya Chama na wananchi ntashirikiana kwa karibu na wadau wa elimu na wanaharakati wa masuala ya Elimu kuishinikiza serikali kutoa Elimu bila ubaguzi hususani kwa watu wenye mahitaji maalum na mabinti wanaopata ujauzito wakiwa mashuleni ili kuwapa fursa ya kujiendeleza na kufikia malengo yao bila kukwamishwa na sheria, kanuni au matamko kandamizi.

Naombeni ushirikiano wenu katika safari hii muhimu kwa ustawi wa Taifa letu, Mungu Awabariki wotee [emoji120].

Fredrick Mbwambo Justine.

Frederick%20.jpeg
 
Wewe una undugu na Lowasa eti?
 
Kuna tofauti mbili hapa, wao CDM kura za maoni kwa kiasi kikubwa ndiyo zinamtangaza mgombea udiwani na ubunge kwenye jimbo husika, kwa upande wetu wana Lumumba itategemea na upepo wa mwenyekigoda wetu kaamkaje siku hiyo.

Hongera kijana kwa kujipambanua, wapiga kura wako wa jimbo ndiyo wataamua kama wafaa ama lah!!
 
Pamoja na ukweli kuwa Sina chama ila vijana Ni wakati wenu kuchukua nafssi za uongozi. Mnakwama wapi ? Atoke ccm ccj cuf act nccr awe kijana. Tumechoka mawazo yaleyale Kila mwaka. Wazee mpumzike waachieni vijana wataongoza lini? Mzee uko bungeni miaka 40 hats aibu huna huna jipya zaidi ya kuunga mkono bila hoja na mawazo mufilisi .WALIOMALIZA 30^ BUNGENI Ondokeni waachieni. Vijana hatujali anatoka chama gani. Mnakera nyie wazee
 
Pamoja na madhaifu waliyonayo chadema ila nina uhakika kwa 100% hawaerzi kufanya kosa la kukupitisha wewe. Nimemaliza
 
Kujiita Justine Lowasa kumeshakuharibia . Chadema hawataki kusikia jina Lowasa

Tuanzie hapa kwa Nini unajiita Justine Lowasa Ni tapeli wewe au ? Hilo jina Lowasa ulijipa kwa sababu gani?
 
Pamoja na madhaifu waliyonayo chadema ila nina uhakika kwa 100% hawaerzi kufanya kosa la kukupitisha wewe. Nimemaliza
Yeye mwanaume kajitokeza hadharani kuwania uongozi tena ubunge, comment yako ina porojo sababu haina facts, ungemjibu kwa facts kwamba kwanini unadhani hawezi kupitishwa na sio porojo
 
Huyu kijana atakuwa mhamiaji haramu wengi hupenda kujiita majina ya Koo kubwa kubwa.Uhamiaji mfuatilieni huyo angalieni anajiita Justine Lowasa huyu atakuwa mhamiaji haramu nendeni mkamhakiki
 
Back
Top Bottom