Uchaguzi 2020 Nipo tayari kukabiliana na Mathayo David au Angela Kairuki Ubunge Same Magharibi

Mungu akutangulie!! Dhamiri yako ya ndani ikakupe hiki unachokitamani,
 
Naona una jina la Wamasai, usije kuongoza kama unachunga mifugo...

Best of lucky kijana
 
Kwa Same Magharibi nafasi bado iko wazi kwa mgombea yeyote atakayepitishwa na CCM mkazi wa jimbo hili na mwenye mapenzi na nyumbani.
Wapare ni wakarimu, wacha Mungu, wachapakazi na wastahimilivu pia.
Kwa sasa wamevumilia na wamechoka, wamechoka tena wamechoka kweli.
Kiufupi unawexa ukapata endapo CCM itamrejesha Mathayo David,vinginevyo kama atatokea mgombea mwingine kama anavyotajwa Angelah Jasmin Kairuki, baasi kaka tafuta shamba la Tangawizi au vitunguu Ruvu uhangaike nalo.
Mathayo David anachangamoto nyingi nyingi tena anawakera wapare na sasa wanamsubiria kwa hamu.
Omba uzima wanaotajwa kuwagusa wananchi wa Same kama Mh Mama Kairuki wasije kuchukua form hapo CHADEMA mtaserereka asubuhi na ubunge.
Bon voyage.
 
Kila la kheri ila usiweke mayai yote kwenye kikapu kimoja.
Kawe Alumin. safi kaka unanikumbushga maneo ya mwalimu wangu wa uchumi kule mzumbe ( marehemu dr kiwango) alikuwa akipenda sana hayo maneno uliyoyaema. Usiweke mayai yote kwenye kikapu kimoja. ...
 
Weka wazi Mkuu wewe binafsi unampigia debe Mh Anjela Kairuki na siyo eti yeye ndiye chaguo la Wana Same Magharibi.
 
Mkishachaguliwa hamkawii kujiuzulu na kuunga juhudi mkono,mnasahau wapambanaji wenu walivyowapambania mpaka mkafika mjengoni,

Unawahakikishia vipi wana Same hautokuwa miongoni mwa misukule dizaini hiyo.
 
mathayo hashindi tena ubunge kwa SAME, jimbo liko wazi kwa ANGELLAH KAIRUKI.
 
Miujiza iko mingi Duniani.
Matahyo mbunge wa jimbo la Same MAGHARIBI ktk uongozi wa awamu ya nne akiwa waziri wa mifugo alilazimishwa kuachia uwaziri kwa kuwa amekuwa MZIGO MZITO.
Tumeshuhudiwa Mathayo David akizomewa mbele ya mhe Makamu wa Rais mama Samia Suluhu ktk viwanja vya Kwasakwasa mjini Same alipoitembelea wilaya hiyo.
Mbunge huyo na waziri mzigo wa zamani, amekuwa akitafutwa na Spika bungeni na hivyo kuweka kwenye orodha ya wabunge watoro bungeni jambo lililoleta tafrani baada ya kubainika hata jimboni kwake haonekani kwa kipindi kirefu.
Mathayo David amezomewa mbele ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Kassim Majaliwa Kassim alipotembelea Same na kufanya mikutano ktk mji wa Hedaru na Same.
Mbunge huyo alipata fedheha na kukidhalilisha chama cha Mapinduzi baada ya kuzomewa tena ktk mkutano wa ndani uliojumuisha makada wa chama, madiwani na watumishi ktk ukumbi wa Halmashauri ya Same.
David Mathayo ameshindwa kusemea na kuwatetea wananchi wake wa jimbo ili wapate maji safi na salama licha ya mh Rais JPM kuwaletea mradi wa bil 80 wa maji toka bwawa la nyumba ya Mungu lililopo wilayani Mwanga, ktk miaka yote mitano hajawahi kuzungumzia masuala ya maji jimboni kwake.
Kwa sasa Mathayo anagawa magari nane aina ya Noah hivi ili zitumike kama ambulance ktk kata nane za ushindi alizozichagua kuhonga.
RUSHWA, hongo na takrima hiyo inafanyika leo Same mbele ya TAKUKURU, Chama cha Mapinduzi wilaya wakiwa wamevalia tai na kusafirisha makada wao toka kata nane zinazohongwa gari hizo zikiwa na wapambe wake aliowachagua kuja kufanya maandamano ya mapokezi ya magari.
Wastaarabu tunajiuliza;
1.Mathayo David amekuwa mbunge kwa miaka 15 ktk jimbo hili mbona asiyalete magari haya siku zoote hizo asubili wakati huu wa kampeni?
2.Kama ana nia njema kwa nini asiyakabidhi magari kwa HALMASHAURI yake iyapeleke huko kadri itakavyopendeza?
3.Pamoja na kuitwa waziri mzigo, mbunge mtoro na kuzomewa na wananchi wake, bado anavunja kanuni na katiba ya chama na viongozi wa CCM wako kimya mnataka watanzania tuwaelewe vipi?
Mh Rais na mwkt wa CCM, katibu wake Bashiru na Polepole Hamphrey wamesikika mara nyingi wakikemea Rushwa na wagombea kufuata taratibu, je Kwa matayo wamempa kibali cha kuendesha kampeni ya hongo na Rushwa???
Viongozi wa Kilimanjaro na Same msitumike ku endorse ubaya na Rushwa, DCI Issaya Mungulu unatuangusha you must be firm as Magufuli.
TAKUKURU fanyeni kazi yenu msisubiri kuagizwa hadharani.
TENDENI HAKI.
 
[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Sina tatizo nawewe kugombea ni demokrasia ila vijana mnaitumia chadema kupata umaarufu mkishafikia malengo mnanyea kambi .
Njia pekee ya mkato mnayoiona ni kupitia chadema mkishapata umaarufu mnaenda kuunga mkono juhudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…