Sikuachi hadi mwisho wa dahari, nitakuwa nawe kwenye hali zote, raha na huzuni kwenye kusifiwa na kwenye kusimangwa nitakuwa nawe, kwa kuwa hakuna binadamu aliye mkamilifu nitasimama na wewe kwenye hayo mapungufu yako yakibinadamu uliyonayo,najua wengi wanapenda ukosee ili wakusimange na kwakweli unapikosea huwa wanakusimanga kwa kila aina ya lugha na maneno, binafsi nimeamua kuwa kinyume na wao,.
Nimeamua kukuombea kwa mola nimayemuamini kwa sababu nimegundua unapokosea wewe mimi na wanajamii wenzangu tunaathirika moja kwa moja, ninayoyaona sasa nakuyasikia sijaanza kuyaona na kuyasikia leo wala jana,nimeanza kuyasikia na kuyaona kabla hata sijakufahamu wala kuwaza kama siku moja nitakuja kukufahamu,mimi nimechagua kukuombea na wewe nakuomba tena kwa unyenyekevu mkubwa kama kuna makosa ambayo siyo ya lazima na yale ambayo yanajirudia kila mwaka basi yapunguze ikiwezekana yaondoe kabisa.
Kumbuka tunaishi kwenye jamii yenye mfumo dume wa kiwango kikubwa,wapo ambao hadi leo hii hawaamini kuwa wewe ndiye na wamezikataza akili zao kukubali kuwa wewe ndiye hivyo wanakufuatilia kwa karibu sana kwa kila hatua unayopiga na wapo makini sana kuangalia makosa na madhaifu yako tu ili wakuseme vibaya nakukudhalilisha kwa wanajamii.
Vile vile naomba ukumbuke tunaishi kwenye jamii ambayo asilimia kubwa ya wanawake hawapendani,muda mwingi kwao ni majungu na hao wanakusubiria kwa hamu ushindwe waseme kuwa tulijua kuwa hawezi lolote,hapa sitowazungumzia wale ambao uliwakuta mjini,ambao wanakuona wa kuja so hufahi kuwa ulipo,yani Mambo ni mengi muda ni mchache ila binafsi nimeamua KUSIMAMA na wewe,wanajamii wanakupenda sana ila lalamiko lao kubwa ni kwamba umezidisha upole.
Wanajamii wanakuomba uwe mkali sana kwa watu wote wanaokurudisha nyuma,wanatamani kuona hatua kali zikichukuliwa kwa wale wezi wote wa mali za jamii,wanajamii wengine wanalalamika kuwa baadhi ya wasaidizi wako wa ndani hawakusaidii ipasavyo wenyewe wanawaza 2030 kuchukua kijiti chako,na hao pia ishi nao kitaalamu nakuomba,yote kwa yote nakupenda sana na nipo tayari KUSIMAMA na wewe katika hali zote!!