Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Kuna Dogo Karudi Juzi Kutoka Dar Kanivunja Sana Mbavu.

Mana Amezoea Zake Huku Asubuhi Wakat Anasubilia Zake Chai Anatafuna Ndiz Za Kuchoma Na Palachcha Ndipo Anywe Chai Na Maandaz.

Mchana Anakula Zake Ndiz Mbiv Na Matunda Mbalimbal Huku Anasubilia Sufuria Ya Ugal Inatokota.

Sasa Alichokutana Nacho Huko Kimara Mwisho Amerud Mwenyewe Home.

DAR Ni Ufahar Tu Ila Maisha Yao Kimlo N Ya Hovyo Sana.

Wanaokula Milo Mitatu Kamili Ni Wakuwahesabu.
 
Yaani mimi mambo ya ajabu sitaki kabisa kwangu mtu msosi unapikwa mpaka mwenyeji unajiuliza nini hiki!!

Mimi kuna siku chakula killipikwa harafu ndani tuko watu wazima 3 kuangalia msosi nikasema hapa leo lazima mtu alale njaa, nikamwambia mpishi wazi kabisa mbele ya mgeni kwamba nenda kapike tena, hapa hupati kitu tukala na mgeni chote yeye akarudia kupika
 
Kuna kipindi nilitoka jkt hapo Kabuku Tanga nikaona sio kesi wacha nipitie hapo DSM kwa anko, ile nimefika siku ya kwanza jioni hivi aunt anaanza kuandaa Mchele Anko akamwambia ongeza kipimo ( maana tunafahamiana vizuri na anko amewahi kaa home enzi hizo anasoma). Sasa wakati wa kula aunt akataka anipakulie msosi ndipo anko akasema wewe mke wangu hebu tujipakulie sisi yeye atajikadiria kwa namna awezavyo. Kufupisha stori nikajikadiria nikapiga mpaka nikashiba nikamuacha shangazi akitumbua macho kwa namna haamini kilichotokea kwwnye hotpot.
 
Nimekupenda bure
 
Yani kuna familia za ajabu sana mkuu. Walinikomalia tena shemeji ndio kanikazania kwa kua nilikua mgen ikabidi tu nifuate maelekezo

Kilichotokea ndio hicho wanabaki kushangaa tu .
 
Aisee Kuna watu Wana roho mbaya,[emoji23][emoji23]
 
Si shangaz yetu yan mke wa uncle ulikuwa ukitoka kujisavia chakula unakatwa jicho hilo haroo nilikaa nao miezi mitano nikaenda kupambana mbele huko, watu wa hapa katikati hapa kama enaenda Kilimanjaro kabla hujafika kwa wapare, hapa katikati kidogo wanasifika kwa uchoyo coz chakula kwao wanaona dili sana kwa kuwa watokea sehem msos wa shida. Utawasikia, mtamisamehe,mtamiona,
 
Kuna siku nilienda mkoa flani sasa ile ndugu wanakufosi unafikiaje Lodge na sisi tupo? nikaona sio kesi acha nifikie kwao nikawa natoka usbh narudi usiku siku ya kwanza wakaleta chapati mbili mbili na maharage na chai nikasema poa sio mbaya labda uzungu kesho tena ivo ivo na siku ya tatu vile vile nikaaaga inabidi kesho twende wilayani sina uhakika kama tutarudi au tutalala huko huko, asbh nikatoka na begi langu nikahamia Lodge mbali kidogo na wanapoishi nimekaa siku tatu sasa siku moja jioni nazungukia bar za pale mjini nikakutana na baba mwenye nyumba akashtuka upo ikabidi nizuge ndio tumeingia muda huu tunatafuta chakula tuendelee na safari.
 
Good hapo ulicheza sana
 
Umenikumbusha kuna rafiki yangu anatoka mwz kajaa dar kakaribishwa na mtoto wa babaake mdogo wajumuike pamoja lunch. msosi katwanga wotee na kuacha kijispece cha jion punde si punde familia ikajumuika na madogo wa shule wamefika toka shule kwenye mahotpot hola mwambaa kakomba na matonge hadi vile vmchuzi vya pembeni lile toto la form one likaanza kulia et leo halijala kitu chochote school af msosi umeisha wotee jamaa alijisikia vibaya sana alijua et ilikuwa ni kwaajiri yake mgeni ikabdi avunge akawaachia 50000 mpka leo anasemaga mie siwezi kula na watu wa dar niwachoyo Sana akifikaga dar anakuja kajipanga Sana huwa anakupigia simu upo wapi njoo sehemu flan uone wanaume tunavyokula mwambaa kufuta kuku mzmaaa ni sekunde tuu tenaa huku anakupigisha story
 
Kijana unakula msosi heavy kama wa komandoo mafunzoni 😅
 
Dsm kumbe life tight hvyo?
 
Hii ilishanikuta, tulikuwa na jamaa yangu Dar. Aisee katika maisha yangu sijawahi kula kijiko kimoja Cha wali.

Nikajiuliza hii ni kutufukuza au ni nini, kibaya zaidi tulienda kumsalimia tu mchana. Chakula kilicholetwa Cha watu wazima watano, Kwa hakika, mtoto wa miaka SITA hashibi.

Mpaka Leo sijawahi PATA jawabu ya kile kitendawili.
 
Umenifanya nicheke sana kiongozi. Umetoa uzoefu wako kaka.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukiingia kwenye mji wa mtu soma kwanza mchezo wanaishi vipi. Hapa Dar kuna watu wanaishi kwa rakaa moja au mbili ya msosi kwa siku.

Yaani wanaamka asubuhi chai ya rangi na andazi moja au mbili kisha deshi hadi jioni kinapikwa ndio nitolee.
 
Huyo nae kazidi, kuku mzima peke yake hiyo ni kufuru.
 
[emoji23] Nimechekaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…