Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Mzee alikua lijendi haswaaa
 
Kuna jamaa tulikua tunaishi magetoni nyumba moja yeye anakaa chumba kinachofata baada ya changu..huyo jamaa alikua anaweka bajeti ya mwezi mzima anatumia laki 1 tu kwa chakula
Anaweza akanunua nyama robo akaikaanga akala hata siku 3 anachukua finyango mbili anamix na spinach/chainizi/sukumawiki anasonga na ugali anakula
Sasa mtu kama huyu akija kua na familia atakua na bajeti kali sana
 
Kwani lazima ule ww ushawaletea zawadi na umeona msosi mdogo ikifika mida ya jioni tafuta sehemu kula kitimoto yako kilo na ndizi mbili ukisindikiza na coke ya baridiiiii mchana tafuta hata mama lishe kula wali wako hapo nyumbani wana bajeti zao temana nao kabisa.

Mimi nilikua nikienda kwa shangazi yangu asubuhi natoka nachukua mikate miwili mmoja wa kwao mmoja wangu nanunua na blueband au peanut butter nikifika muda wa chai naiweka yote mezani wanaanza kuleta bajeti eti mmoja ubaki hapo ndipo nawaambia huu nakula mwenyewe ili nisiharibu ratiba zenu huo kuleni nyie mwanzo walipata tabu ila walizoea mchana natoka nikirudi jioni napitia sehemu ya nyama au kuku naagiza chakula najipigia nikirud home nimeshiba nagusa gusa vijiko viwili nalala nikiwa njema kabisa. Kama huna hela kufa njaa tu hamna namna
 
Chief kitimoto kilo nzima na ndizi unaikandamiza yote?
 
Doh!
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ungesema asante umeshiba
 
Kula mgahawani mpenzi kula tani Yako jamani dar hawajui kupika unataka kutapika mpaka uzirai acha tu . Hawajui
 
Yani kuna familia za ajabu sana mkuu. Walinikomalia tena shemeji ndio kanikazania kwa kua nilikua mgen ikabidi tu nifuate maelekezo

Kilichotokea ndio hicho wanabaki kushangaa tu .
Aseeh sisi kwetu mgeni haendi peke yake mezani anaenda na mwenyeji wake. Yan hiyo inamfanya anajisikia comfortable kuliko kumuacha peke ake. Sio ustaarabu kabisa
 
Hahaa.. eti hapa katikati[emoji23][emoji23]
 
Aiseeeee...nimecheka Kwa sauti Hadi wananishangaa
 
Kusema kweli mjini hasa Dar watu wanakula share ndogo sana. Chakula kinapikwa hadi unajiwazia kweli hiki watu wanashiba? Ila ndio life la town!!
Swala sio life la town ishu ni kipato ,kuna watu wako town wanakula msosi heavy na wengine wako village msosi kiduchu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…