Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno


Ondoka tu, maana ungeweza kwenda kula tu huko nje.
 
Bangi zinachangi sana kufanya watu kula sana
 
Hii mambo huwa inategemea na mwanaume wa familia kumpush mkewe., maana mke anaweza kuwa hajiongezi kulingana na idadi ya watu waliopo., mnaweza kuwa mmezoea kupika chakula cha watu watatu wakaongezeka wageni watatu, obvious kipimo kitaongezeka ila ukikuta mke anapika ratio ile ile wakati watu wameongezeka hapo lazima kuna watu watateseka kimoyomoyo.
 
Imagine mtu anaenda kununua nyanya mbili, kitunguu kimoja, mafuta ya jero, hoho moja, karoti moja, dagaa wa buku na unga nusu na robo.

Unadhani kuna nini hapo? Hongera mkuu kama hujawahi ona au kuishi namna hiyo.
Ukiwa maduka ya Mangi hayo mambo ya kawaida.
Anatumwa mtoto anunue mafuta ya 500
Unga Robo 3
 
Tatizo ulienda kwa watu masikini, kimasikini
 
Solution ni kuacha kufikia kwa watu. Kwanza kufikia kwa watu unabadili utaratibu wao wa maisha. Ni heri upange ratiba zako ufikie lodge ufante yako usepe
Haya mambo yamepungua sana siku hizi, baada ya simu kuja hivyo mtu anafanya mawasiliano kujuliana hali.
Hospital za Rufaa Kanda nazo zimesaidia watu kutorundikana kwa watu

Shule kila sehemu zimesaidia watu kutoenda kwa watu
 
Nyumba zina utaratibu na nyingine ni vituko kwenda mbele mpaka dhambi, niliwahi kutembelea familia moja, nilichoona sikukipenda kabisa, wakati wa kula wote tulikaa mezani lakini msichana wa kazi anakaa jikoni na kula huko na kibaya zaidi kama Kuna kitu kimekosekana anaitwa akilete, I didn't like it na baadaye wakati na mwenyeji wangu peke yetu I confronted him na nilimsema bila kujali, aliahidi kubadili ule utaratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…