Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Wanafanya Nn siku zote hizo,
Mkuu walikuja kutembea kabla ya ramadhani Ila jana nimemsikia wife mwenyewe akisema wataftie nauli waondoke ,maana ningesema mimi ningeonekena staki ndgu wa wife ,maana washakuja wengi miyayusho na huwa namwambia wife huyu simtaki arudi hapa kutokana na Tabia zake ,
Sasa huyu mwingine nilinyamaza kimya nikaacha shetani ataje jina (wife mwenyewe afikie uwamuzi ) Ila yeye mwenyewe maana kachoka maana alishindwa hata na bint yangu wa kwanza ana miaka 10 ,usiku wa ijumaa ambapo j mosi ndo sikukuu kulikuwa na maandalizi ya vitafunwa asubuhi ,
Bint alipomuona mama ake pilika nyingi ilibidi aaende jikoni kumsaidia ,Mpaka akamwambia mama ake ,si umwambie shangazi aje akusaidie ,Ila yule wife mtu alikuwa zake ukumbini ana angalia Tv ,Aisee kuna watu hawana haya wala hawajui vibaya aiseeee,
 
Aisee ifikie kipindi ndugu muache gubu. Huyo mke wako ndio mama mwenye nyumba anashindwa vipi kumwambia ndugu yake njoo jikoni unisaidie kazi?

Kuna binadamu wengine hawajui kujiongeza inatakiwa wewe ndio umpe muongozo!

Sasa wote mpo nae mmekaa kimya hamumwambii lolote mnabaki kugugumia chini chini utafikiri yeye ndio mwenye nyumba mnamuogopa na kuna uwezekano alipotoka huko hamna tv na ndio kaikuta hapo kwako ana usongo nao na nyie mmemkalia kimya hamjiongezi!
 
Natamani kucheka lkn nikikumbuka nilipo hapa ha ha ha ha ni balaaa itoshe kusema pole sana mwamba angalia mazingira rafiki kwako!
 
🀣🀣🀣🀣🀣
 
Cha msingi unapofika ugenini hakikisha unakuwa na budget ya ziada ili kuweza kumudu baadhi ya mahitaji yako kama issue ya msosi, sisi wasukuma tumezoea kula hadi kusaza sasa ugenini itanipa shida sana jamani.
 
ukweli kabisa dar ni ngumu sana kwenye misosi chai mkate wa buku watu watano wakati mi nikinuna na futa mi3 peke yangu,, ugali wa dar ndio matatizo matupu mlaini kama wa wagonjwa harafu mdogo jamani dar watu wanateseka sana
 
Babu (R.I.P) alikuwa anasema watu wa town wanakula msosi na jagi la maji ya kunywa pembeni ili kujazia tumbo maana hawashibi msosi ni wa kuungaunga.
 
Wenyeji wako ni wapare au wahaya?
Hao ndio zao, chakula wanakiona kitu adimu Sana.
 
Hakuna lodge huko?
 
rahisi sana nenda sokoni nunua unga kg 10 wa ugali,mchele kg 15,mafuta lita 5 nyanya,vitunguu,na nyama upeleke
 
Mama yangu alinifundisha sana kuhusu chakula na mgeni.

Kukiwa na mgeni hakikisha chakula ni kingi zaidi ya mlivyozoea mkiwa pekee yenu

Kukiwa na mgeni hakikisha chakula kinaandaliwa mapema, sio mmezoea kupata chai sa tano bhasi na mgeni mnamuandalia saa tano

au mnakulaga cha usiku saa 5 bhasi na mgeni mnamsubirisha.

Si uugwana kabisa labda kuwe na sababu za msingi.

Haya huwa nayazingatia sana maishani mwangu.

Mgeni kwagu ni baraka, na katika hili wageni wengi niliowahi kuwapokea, mbele katika maisha huwa wanani treat vizuri sana nikiwa kwenye situation flani.
 
Wanabana matumizi, maisha magumu haya jamani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…