Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Umeyakanyaga
 
Watu wa mkoani wanakula sana. Nakumbuka miaka mingi kidogo tulianda katika wilaya moja mkoa wa Tabora. Sisi ni watu wa Dar. Basi mida wa misosi tunatengewa ugali mkubwa sana, tukila hata robo hatumalizi yaani unaweza kusema ugali wote unaludi jikoni. Walikuwa wanatushangaa sana na kutuona ni watu wa ajabu sana kusema sisi watu wa mjini hatuli kabisa.
 
Hiki kisa kimenikumbusha miaka flani ya 2012 nilimtembelea braza Dodoma nilkua napita tu nikaona kwa kua n broza dam dam na miaka ming hatujaonana basi wacha nikite kambi walau kwa siku moja

Sasa kumbe maisha ya bro yamebadilika sana chakula hali tena kama zamani wametenga ka chakula (wali) kwenye ile hot pot ndogo ni kama walipika nusu kilo hivi basi na vipande vya kuku maharagwe kidogo na mboga za majani hahahaha

Ngoja nicheke kidogo[emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji1787] kumbe ndio chakula cha kula familia nzima (bro , mke wake, house girl na mtoto mmoja wa kama miaka sita hvi na mimi mgeni wao) basi wakanikaribisha huku wakinisisitiza nikapakue

Basi mzee nikainuka kwenda mezani nilivoona ule msosi akili ikaniambia kwa jinsi hiki chakula kilivyo kidogo itakua ni changu peke yangu nilipakua ule wali zaid ya robo tatu tia mboga ya majani na maharage na vipande kama vitatu vya kuku

Sasa baada ya dakika chache huku naendelea kuchakata nawaona na wao wanakuja mezani

Ilibidi niulize kwani na nyie ndio mnakula hiki hiki huku nikiwa na mshangao na taharuki ya hali ya juu ikabidi wajichekeshe chekeshe pale house girl akaingia jikon kupika ugali

Kesho yake niliamsha bila hata kupata breakfast maana siwezi kukaa nyumba yenye njaa mimi
 
Kuna mwaka nilisafiri na treni kutoka Mwanza-Dar. Kufika sehemu kuna jamaa alipakia magunia ya karanga akayaweka kwenye korido ya kwenda chooni. Tukafika ktk kituo kimoja mjamaa alinunua mihogo ya kuchemsha aisee ilikuwa mihogo mingi sana na kachumbali juu, nikawa najuiliza huyu jamaa ataimaliza kweli hiyo mihogo. Aisee nilishangaa sana na nikaamini kuna watu wanakula sana yaani ni ngumu kuamini
 
First appointment tangu nilipangiwa Pwani, kutokana na bajeti finyu niliyokuwa nayo sikula chochote njia nzima mpaka nafika
Miaka hiyo hakukuwa na bodaboda hivyo kushuka stendi nikaelekezwa tu kwa mwenyeji wangu. Alikuwa mzee maarufu sana hiyo mitaa, nikatembea mwendo wa dakika kumi nikafika. Ilikuwa kwenye saa nane hivi
Nikakuta wako mesi wanagonga wali maharagwe na samaki, nikakaribishwa kwa bashasha sana lakini nikazuga nimeshiba sana maana njiani gari ilisimama mahali tukala ( najuta kufanya vile)

Ningekuwa nafahamu taratibu za watu ningekubali kula siku ile, lakini bila kujua nilijipa moyo kwamba jioni nitakula nishibe maana nilikotoka nilikuwa nimekunywa chai rangi na andazi moja tu asubuhi

Yule mzee alikuwa mkarimu na mtu wa story sana kwahiyo mchana wote tulishinda hapo kwake upenuni mpaka jioni alipoenda msikitini
Sasa mimi njaa inauma mida inasogea kigiza kinaingia ila sioni harakati zozote za maandalizi ya dinner ( ilikuwa familia ya watu watano baba, mama, mabinti wawili na kijana wa kiume)

Nikajipa moyo kwamba pengine kilipikwa na cha jioni ule mchana.. Kufika saa mbili usiku mzee akarudi na mkate! Kwa mawazo yangu ulikuwa kwa ajili ya kesho asubuhi
Dakika chache baada ya mzee kurudi nikaitwa ndani kwa ajili ya dinner..! Lahaula rasuli! Dinner ilikuwa kikombe cha chai ya rangi na silesi mbili za mkate[emoji23]
Kwanza nilidhani tunapasha matumbo joto halafu mahanjumati yaja.. Pengine misamaki tasi, kolekole, pweza wa kubanikwa chapati na mkate wa kumimina ama kiporo cha mchana! Naona kila anayemaliza ananyanyuka mezani.. Nilikuwa wa mwisho

Hakuna kitu kinatesa kama njaa ya ugenini..!!!
 
Hakuna kuvunga [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana...

Ondoka hapo mapema..
 
Mkuu hao walikuwa wapare wenzakeo hao. Jamani kula Kwa mpare ni KAZI aseee chakula Chao kidogo oooo wanabana matumizi wale Watu tena ukute mpare msabato aseee utajuta. Kande halijaungwa na kisamvu hakijaungwa
 
Mkuu hao walikuwa wapare wenzakeo hao. Jamani kula Kwa mpare ni KAZI aseee chakula Chao kidogo oooo wanabana matumizi wale Watu tena ukute mpare msabato aseee utajuta. Kande halijaungwa na kisamvu hakijaungwa
Hapana walikuwa watu wa Pwani wasio na kaliba yoyote na Wapare
 
Nenda kale gengeni mkuu sio kila kitu unakuja kulialia huku
 
Nashukuru Wadau kwa michango yenu

Ila nipo mtwara ndani ndani , kwanza ni kijijin hakuna gest kbsa,Cha pili migahawa imefungwa maana wengi hapa wamefunga si mnajua huu mwezi wa Ramadhani,
Pale sokon Kuna watu jion wanauza uji na ftali ,
Ila apo wanapo uza Kuna duka la dawa la huyu dada nilipofikia na anauza mdogo wake , Jana nimeenda nikaona nikinywa uji dogo atakuja kuchoma nikala chungwa moja,
Daah yan
 
Jwanza haya mambo ya mtu mzima kufikia kwa watu sijuwi yanakuwaje Tanzania. Kwanini usifikie hotel ukawa huru?

Dunia ya leo si ya kufikia kwa watu, mahoteli yamejaa kila sehemu.

Kula kwa mtu ni kwa kualikwa tu.
Ni kijijin kbsa sio mjin hakuna gest
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…