First appointment tangu nilipangiwa Pwani, kutokana na bajeti finyu niliyokuwa nayo sikula chochote njia nzima mpaka nafika
Miaka hiyo hakukuwa na bodaboda hivyo kushuka stendi nikaelekezwa tu kwa mwenyeji wangu. Alikuwa mzee maarufu sana hiyo mitaa, nikatembea mwendo wa dakika kumi nikafika. Ilikuwa kwenye saa nane hivi
Nikakuta wako mesi wanagonga wali maharagwe na samaki, nikakaribishwa kwa bashasha sana lakini nikazuga nimeshiba sana maana njiani gari ilisimama mahali tukala ( najuta kufanya vile)
Ningekuwa nafahamu taratibu za watu ningekubali kula siku ile, lakini bila kujua nilijipa moyo kwamba jioni nitakula nishibe maana nilikotoka nilikuwa nimekunywa chai rangi na andazi moja tu asubuhi
Yule mzee alikuwa mkarimu na mtu wa story sana kwahiyo mchana wote tulishinda hapo kwake upenuni mpaka jioni alipoenda msikitini
Sasa mimi njaa inauma mida inasogea kigiza kinaingia ila sioni harakati zozote za maandalizi ya dinner ( ilikuwa familia ya watu watano baba, mama, mabinti wawili na kijana wa kiume)
Nikajipa moyo kwamba pengine kilipikwa na cha jioni ule mchana.. Kufika saa mbili usiku mzee akarudi na mkate! Kwa mawazo yangu ulikuwa kwa ajili ya kesho asubuhi
Dakika chache baada ya mzee kurudi nikaitwa ndani kwa ajili ya dinner..! Lahaula rasuli! Dinner ilikuwa kikombe cha chai ya rangi na silesi mbili za mkate[emoji23]
Kwanza nilidhani tunapasha matumbo joto halafu mahanjumati yaja.. Pengine misamaki tasi, kolekole, pweza wa kubanikwa chapati na mkate wa kumimina ama kiporo cha mchana! Naona kila anayemaliza ananyanyuka mezani.. Nilikuwa wa mwisho
Hakuna kitu kinatesa kama njaa ya ugenini..!!!