HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
Kwanza mgeni anatakiwa afikie guestHuna hela za kula hata nyama choma bar ,unarudi home unajazia unalala ..
Mgeni unakula kama utitili ,....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanza mgeni anatakiwa afikie guestHuna hela za kula hata nyama choma bar ,unarudi home unajazia unalala ..
Mgeni unakula kama utitili ,....
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Ugenini noma asee nilimtembelea jamaa angu asee yan chakula cha usiku wanakula saa tano usiku...
Siku ya kwanza nilijua labda jion hawali naona chele saa tatu tatu ndio linachambuliwa mama anawasha moto
Hayo ni yako shabiki wa CityMtu unakula ugali kama ngumi ya mtoto na dagaa tatu mchuzi ndoo ya maji ....harafu ukiwa Kwa bed unataka kupiga goli 3 ,na upelekee moto ,my friend utaendelea kujiona huna nguvu ,kumbe hata nguvu za kawaida tu huna ....
Watu dsm wanashinda njaa kiasi kwamba wanakosa hata nguvu za kuongea ,..
Hadi kijijini siku hizi, maana nao hununuaMjini mahesabu
Huo usiku ulikuwa mrefu sana kwako bila shaka. Natafakari Hali kama hii uliyoipata ningekuwa ni Mimi ningeamka mgonjwa kabisa [emoji23]First appointment tangu nilipangiwa Pwani, kutokana na bajeti finyu niliyokuwa nayo sikula chochote njia nzima mpaka nafika
Miaka hiyo hakukuwa na bodaboda hivyo kushuka stendi nikaelekezwa tu kwa mwenyeji wangu. Alikuwa mzee maarufu sana hiyo mitaa, nikatembea mwendo wa dakika kumi nikafika. Ilikuwa kwenye saa nane hivi
Nikakuta wako mesi wanagonga wali maharagwe na samaki, nikakaribishwa kwa bashasha sana lakini nikazuga nimeshiba sana maana njiani gari ilisimama mahali tukala ( najuta kufanya vile)
Ningekuwa nafahamu taratibu za watu ningekubali kula siku ile, lakini bila kujua nilijipa moyo kwamba jioni nitakula nishibe maana nilikotoka nilikuwa nimekunywa chai rangi na andazi moja tu asubuhi
Yule mzee alikuwa mkarimu na mtu wa story sana kwahiyo mchana wote tulishinda hapo kwake upenuni mpaka jioni alipoenda msikitini
Sasa mimi njaa inauma mida inasogea kigiza kinaingia ila sioni harakati zozote za maandalizi ya dinner ( ilikuwa familia ya watu watano baba, mama, mabinti wawili na kijana wa kiume)
Nikajipa moyo kwamba pengine kilipikwa na cha jioni ule mchana.. Kufika saa mbili usiku mzee akarudi na mkate! Kwa mawazo yangu ulikuwa kwa ajili ya kesho asubuhi
Dakika chache baada ya mzee kurudi nikaitwa ndani kwa ajili ya dinner..! Lahaula rasuli! Dinner ilikuwa kikombe cha chai ya rangi na silesi mbili za mkate[emoji23]
Kwanza nilidhani tunapasha matumbo joto halafu mahanjumati yaja.. Pengine misamaki tasi, kolekole, pweza wa kubanikwa chapati na mkate wa kumimina ama kiporo cha mchana! Naona kila anayemaliza ananyanyuka mezani.. Nilikuwa wa mwisho
Hakuna kitu kinatesa kama njaa ya ugenini..!!!
Ndo siku nyingine uende guest au hotelIla ugenini kunaweza kukufanya usiwe na raha kuna sehemu nilifikia kabla ya kulala usiku wanaka ibada wanakusanyika sebuleni wakiamka ahsubuhi saa 12 kaibada nami sijazoea hiyo michongo
Hatutaki wageni wasio na faidaHalaf sio kwamba wao wanakula kidogo hapana huko wanapotoka makazini kwao wanakula wanashiba wakifika home wanajazilizia kidogo
Watu wa hivyo siku wakija kwenu wapikie chakula kingi na kizurii wale sana
Unaenda salimia watu nenda na chakula sio unapeleka mavi na mkojoHao ni wachoyo...kuna kipindi kimoja nilienda kumtembelea baba yangu mdogo Kilosa mkewe alikuwa mchoyo sana anapika chakula kidogo sana nikajirudia zangu CHABIMA ndani huko karibu na Lumuma.
Aseee! Hiyo kawaida kabisa, hutokea watu wengi sana. Sisi watu wa kusini tumezoea kujaza sahani maana misosi yakutosha, hao wa Dar Wana budget Kali sana. Ila kama unamishe zako si vema sana kufikia Kwa ndugu ama jamaa, panga budget yako vema ili ufikie lodge ya Bei unayoimudu.
Pole, kumbe Bado upo ugenini Hadi sasa. Kwa mazingira hayo vumilia tu. Ila kama utakaa kitambo Kidogo tafuta rafiki fasta ili uwenae matembezi mida Fulani hivi, kwa strategy hii atakuonyesha kijiwe poa tu.Nashukuru Wadau kwa michango yenu
Ila nipo mtwara ndani ndani , kwanza ni kijijin hakuna gest kbsa,Cha pili migahawa imefungwa maana wengi hapa wamefunga si mnajua huu mwezi wa Ramadhani,
Pale sokon Kuna watu jion wanauza uji na ftali ,
Ila apo wanapo uza Kuna duka la dawa la huyu dada nilipofikia na anauza mdogo wake , Jana nimeenda nikaona nikinywa uji dogo atakuja kuchoma nikala chungwa moja,
Daah yan
Muwaambie wasije kama chakula ni shidaHatutaki wageni wasio na faida
Tabia ya kupika chakula kingi au kidogo inategemea na Jamii usika na siyo mjini au kijijiniKusema kweli mjini hasa Dar watu wanakula share ndogo sana. Chakula kinapikwa hadi unajiwazia kweli hiki watu wanashiba? Ila ndio life la town!!
Hii familia ya mang'ati? Pia inawezekana upo single mkuu alafu ulipoenda Kuna mabinti single [emoji23][emoji23][emoji23]. Maana hii iliwahi nikuta Mimi miaka ya 2007/2008, nilipanga mahali alafu nipo single na kunabinti pale mtoto wa mwenyenyumba asee wakichinja kuku, nusu nzima nakula Mimi. Baadae wakaniamishia chumba kubwa kwenye Nyumba Yao ya familia alooo! Nilifaidi sana na Nia Yao niliing'amua lakini nikatulia tu na kuendelea kula misosi.Kuna mahala nipo mimi ni mgeni, unakaangiwa nusu kuku na hapo wanataka ule na supu.Ukikaa kidogo wanakukaangia ndizi na perege kwa kweli nimekula.Pasaka wakataka kuniua wakanipikia machalari na minyama mikubwa kama ngumi ya mandonga.
Sijakaa vizuri wakaniletea chipsi na nyama za mbuzi za kuchoma.Hamadi wakaleta pilau mbuzi na vipande vya tikiti sijui na saladi.Nikala mpaka nikakasirika kwa furaha.Walivyo kiboko wakaniletea na supu.Mara paap bia hizi nkasema mi sinnywi bia wakaniletea soda tatu, ya mchana, ya asubuhi na ya jioni wakati wa kulala.Ratiba ya kuzinywa nilipanga mimi.
Yaani wakuu nilikuwa na uhakika wa kula nusu kuku kila siku.saa nyingine asubuhi kidari mchana Firigisi, jioni kipaja asubuhi namalizia kidari wakati mwingine.Nimekaa siku kumi na nne.Kuna kazi nilienda kuifanya kwao wameniambia nirudi tena kufanya ingine.NAONA KUCHELEWA.
SHIKAMOO WALE WATU WALIJUA KUNINYOOSHA KWA KWELI.ila mkuu pole hao watu ni wachoyo.jaiwezekani chakula ambacho hata panya hamalizi mle watu wanne.HAO NI WACHOYO.
Nyie mmezidi jamni 😀
😂😂😂Japo kwenye kitimoto pamekukera mgeni alikuwa muungwana 😂😂Wapuuzi wakubwa kumbe uliwanunulia na kitimoto kg 2? Ukute walikuwekea nyama mbili.