Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Ugenini noma asee nilimtembelea jamaa angu asee yan chakula cha usiku wanakula saa tano usiku...

Siku ya kwanza nilijua labda jion hawali naona chele saa tatu tatu ndio linachambuliwa mama anawasha moto
🀣🀣🀣🀣🀣🀣
Umenikumbusha sehemu, wao walikua wanakula chakula Cha usiku saa sita
 
Hayo ni yako shabiki wa City
 
Mwaka jana kuna project nilienda kufanya mkoa fulani hivi ya kama wik mbili nilipofika nikapokelewa na mwenyeji wangu. Basi baada ya stori mbili tatu nikamwambia anipeleke Lodge nzuri. Jamaa akaniambia Lodge ya nini wakati home kwake kuna chumba cha wageni. Nikakataa lkn jamaa akasisitiza niende nikaona isiwe case. Nikajiongeza tukapitia kwa mangi nikafungasha haswa vitu vya ndani mamichele,unga wa ngano mafuta,tambi na mazaga zaga kibao nikamuuliza kama ana frigi akasema anayo tukapitia na buchani kununua nyama na masoseji. Basi tukafika home tukapokelewa na mke wake na watoto wake wanne wawili wa kike wawili wa kiume. Kesho yake nikaanza mishe. Yaani wale watu ni wakarimu ajabu. Shemeji kila asubuhi baada ya heavy breakfast kabla sijaondoka ananiuliza nikirudi nitapendelea kula nini,wale watoto wa kike asubuhi wananiambia niwatolee nguo chafu wafue. Mi ni Mkristo na wao ni Waislamu safi lkn awajawahi kunistrict kupiga mambo yetu yale. Tukienda bar na yule jamaa mi nakamatia vitu yeye anacharaza zake Redbull tukiondoka tunachukua nyama ya mbuzi kilo tunarudi home tunakula na familia yake fresh tuu. Siku ya kuondoka ilivyofika hakuna aliyekuwa anataka niondoke na walihuzunika sana hadi kulia. Mpaka leo ni kama ndugu zangu kabisa wananitembelea na familia yangu huwa tunafunga safari kwenda kuwatembelea. Sorry kwa uandishi mbovu.
 
Huo usiku ulikuwa mrefu sana kwako bila shaka. Natafakari Hali kama hii uliyoipata ningekuwa ni Mimi ningeamka mgonjwa kabisa [emoji23]
 
Ila ugenini kunaweza kukufanya usiwe na raha kuna sehemu nilifikia kabla ya kulala usiku wanaka ibada wanakusanyika sebuleni wakiamka ahsubuhi saa 12 kaibada nami sijazoea hiyo michongo
Ndo siku nyingine uende guest au hotel
 
Halaf sio kwamba wao wanakula kidogo hapana huko wanapotoka makazini kwao wanakula wanashiba wakifika home wanajazilizia kidogo
Watu wa hivyo siku wakija kwenu wapikie chakula kingi na kizurii wale sana
Hatutaki wageni wasio na faida
 
Hao ni wachoyo...kuna kipindi kimoja nilienda kumtembelea baba yangu mdogo Kilosa mkewe alikuwa mchoyo sana anapika chakula kidogo sana nikajirudia zangu CHABIMA ndani huko karibu na Lumuma.
Unaenda salimia watu nenda na chakula sio unapeleka mavi na mkojo
 
Sio b


Kula kidogo haiusiani na budget Sio budget Matumbo ya watu wa mjini yameshazoea portion ndogo Nyie wa mikoani ugali kilo moja unataka ule peko yako ni tumbo la kibinadamu ni pipa
 
Pole, kumbe Bado upo ugenini Hadi sasa. Kwa mazingira hayo vumilia tu. Ila kama utakaa kitambo Kidogo tafuta rafiki fasta ili uwenae matembezi mida Fulani hivi, kwa strategy hii atakuonyesha kijiwe poa tu.
 
Kusema kweli mjini hasa Dar watu wanakula share ndogo sana. Chakula kinapikwa hadi unajiwazia kweli hiki watu wanashiba? Ila ndio life la town!!
Tabia ya kupika chakula kingi au kidogo inategemea na Jamii usika na siyo mjini au kijijini

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Hii familia ya mang'ati? Pia inawezekana upo single mkuu alafu ulipoenda Kuna mabinti single [emoji23][emoji23][emoji23]. Maana hii iliwahi nikuta Mimi miaka ya 2007/2008, nilipanga mahali alafu nipo single na kunabinti pale mtoto wa mwenyenyumba asee wakichinja kuku, nusu nzima nakula Mimi. Baadae wakaniamishia chumba kubwa kwenye Nyumba Yao ya familia alooo! Nilifaidi sana na Nia Yao niliing'amua lakini nikatulia tu na kuendelea kula misosi.
 
Ila mikoa ya huku mnapitia magumu, kwetu tangu tukiwa watoto ukipika chakula lazima uweke cha mgeni na cha watoto watakacho kula saa 12 jioni ili wasisinzie bila kula usiku.

Mpaka leo huwezi kwenda mama yangu jion saa 10 usikute chakula.

Tukila mchana lazima kitolewe cha kuku, mbwa, kilichobaki kinatunzwa jikoni kwa ajili ya mgeni akija gafla. Hii ratiba ni almost kila siku.
Embu tuseme hii life ni la kijijini.

Huku mjini ndio kuna bajeti lakini mimi nikipika chakula napika changu tu ila.mboga lazima iwe nyingi ili mgeni akitokea nimsongee hata ugali.
Nyie watu wengine ni wachoyo hivi mwanaume anaweza kula ka ugali kadogo kama ngumi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…