Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Ndio maana wasukuma wakienda mijini wanateseka sana..ugenini wewe jilie zako nje ukija homu unagusa tonge moja tu ya kuzugia.
Sipendi kulala kwa mtu sana
ERoni
 
Good recommendation. [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kusini gan yenye misosi maan npo huku 5years chakula ni shda familia zinakula milo mi2 had mmoja baada ya msimu wa korosho

30% wanalima mahind na wakulima wachache sana wenye uwezo wa kuvuna magunia ya mahindi 7+


Huku n njaaa
Nyanda za juu kusini. Iringa
 

Nunua vitu ingia jikoni pika bana halaf jaza kwa hotpot ,asubuhi nunua mayai jikaangie na chapati kula we subiri vya bure
 
Ukifika ugenini make sure unafanya backup kabla ya kurudi home, pita mahali kula kidogo, ukirudi home unakula kiasi tu kwa amani bila huzuni za kutoshiba.
 
Ukienda ugenini kale kitaa achana na msosi wa shikamoo shemeji.
 
Kula kutokana na Kazi yako sio upo tu nyumbani hautoki unataka kula nusu ya Ugali mtu mmoja ni hatari kwa Afya binafsi Mimi sioni Kama chakula ni kidogo isipokuwa naona unataka kuforce kula Sana Kama mtu anayebeba zege .
 
Umeandika vizuri tu na umeeleweka safi. HIYO FAMILIA NZURI SANA, MPAKA NATAMANI NINGEKUWA MIMI NIMEPITA HAPO. KWAKUWA HUJATAJA MKOA SIO MBAYA UNGETAJA INGEKUWA POA ILI SIKU NIKIKATIZA HUKO NIKAWASALIMU.
 
Acha uroho kama hushibi zi ule njee hafu unakuja kula ndani nenda kwenu
 
Sasa huyu mwenyeji wako anapata hata nguvu za kunyandua kweli ikiwa lishe ni kiduchu hivyo?
Kuna unalzima gani wa wewe kuendelea kuwepo mahali hapo?
Hakuna lodge/hotel/guest house jirani?
Jiongeze kijana!!
 
Ndugu kama ulivosoma post sipend vitonga , huku mtwara vijijini hakuna gest kbsa na Kuna ishu muhimu ilinileta ,
Nachangia Sana na Leo nanunua kuku , cpendi vitonga
Huyu kuku usimnunuwe ushanunua kitimoto inatosha.
Shemeji yako ni mchoyo kesho unaondoka wewe leo wakipakuwa pakuwa kingi ushibe watajua wenyewe.
Hivi ndugu yako haoni hiyo hali anajifanya kujisahaulisha nyumbani mnavyo kula? Kwa nini asimwambie mke wake apike chakula cha kutosha?
Mgeni anatakiwa ale atowe ka jasho kha!
 
kuna sisi tulio kulia maisha ya kula kila mda tukifika sehem ya bajet bajet hatukai tuna lala mbereee

nakumbuka tuu zamani tulipokuwa wadogo home

maziwa yakumwaga
matunda kamayote
nyama ya kuku usiseme
mahindi

yani unakuta namsosi wakutosha unapikwa tunakula na kusaza

Hadi leo nyumba ambayo chakula hakibaki naiona ina mapungufu

mama alituambia msimalize chakula chote lazima kibaki kidogo anaweza kuja mtu mwenye njaa Kali mkashindwa kumsaidia japo tonge moja na akawafia

tenga msosi mtu ale aache kikibaki kesho kinapaswa watu wananywea chai
 
Mama ana Roho ya utakatifu kabisa. Naambieni wazazi Wetu, bibi na Babu wa ZETU ni watakatifu maana walikuwa na ukarimu mkubwa sana. Walitunza misitu, wakapata Mvua nyingi na kulima mazao Kwa wingi hivyo kuwa na chakula Cha kutosha. Ila sikuhizi tunaiga uzungu kuliko kawaida, tumekata misitu, Mvua tabu, mazoa Kidogo. Sasa chakula tunakula Kwa kujilamba tu. [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…