Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Hapo wanakufukuza kijanja.. Hawataki kukuona na inawezekana unalala sebuleni au nawatoto..
 
Acha kusengenya wenyeji wako!!! Hata hivyo umejikaribisha mwenyewe ni vyema uvumilie hadi utakaporudi kwako. Lasivyo tafuta kiguest na kigenge cha mama ntilie hadi utakapomaliza shughuli zako hapo kijijini.
 
Bora wewe umekata nusu,ningekua mimi ningekula wote,wao si ndio wenyeji wangeenda jikoni kupika tena,sio kula kama unaonja,kwanza huku kijijini kabla ya chakula tunaanza na karanga mara maziwa na manumbu mpka chakula kinakuja mtu ushaanza kushiba,
 
Hao ndio watu wamjini budget za msosi kama wahindi.Gunia tatu za dengu matumizi mwaka mzima kazi kuongeza pilipili tu kuleta ladha.
Ha ha ha huko chooni inakuwaje!
 
Kuna siku nilikuwa na wageni Fulani watasha sehemu Fulani, wao wanakula Kidogo sana, Mimi nikamsoma dereva maana mswahili mwenzangu, yeye anajifanya anazuga alafu anaaga anaenda kufata vocha aloo Kumbe anaenda kwenye mgahawa wa karibu na kupiga mapigo ya kibongo. Niliunga tela fasta siku inayofata nikamwambia na Mimi nataka nitume M-pesa sehemu akaniambia njiani asee Mimi huwa sishibi hiyo misosi nikamwambia sio peke yako, alicheka sana. Nikaagiza ugali sahani mbili chap, dereva alicheka sana. Hii ndio mipango. [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mkaanza kupanga matofari
 
Mtu unakula ugali kama ngumi ya mtoto na dagaa tatu mchuzi ndoo ya maji ....harafu ukiwa Kwa bed unataka kupiga goli 3 ,na upelekee moto ,my friend utaendelea kujiona huna nguvu ,kumbe hata nguvu za kawaida tu huna ....

Watu dsm wanashinda njaa kiasi kwamba wanakosa hata nguvu za kuongea ,..
 
Kusema kweli mjini hasa Dar watu wanakula share ndogo sana. Chakula kinapikwa hadi unajiwazia kweli hiki watu wanashiba? Ila ndio life la town!!
🤣🤣🤣🤣 Kumbe
 
Back
Top Bottom