Inaweza kuwa ni hormones inbalance. Kuna umuhimu wa ku-rule out cancer, manake hiyo inaweza kumaanisha una ductile papilloma (inakuwa na 5% chance ya kuendea kwenye kansa miaka hata 10 baadae).
Cha kufanya ni kuonana na breast surgeon, naweza kukupa namba ya mmoja wa muhimbili. Utafanya breast cytology baada ya kufanyiwa physical check kuona kama una uvimbe wowote. Ni kipimo rahisi tu bila maumivu, maziwa yanakamuliwa kwenye slide na kuchekiwa maabara.
Una tabia ya kufanya uchunguzi wa matiti yako kila mara? Ni utaratibu mzuri wa kujizoeza.