Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]Ndugu mleta mada nimepitia uzi wako kwa makini na nimeelewa vizuri shida ulio nayo
Katika gari yoyote ile kitu kinachoongeza uzito kwa kiasi kikubwa kuliko vyote ni injini, hivyo tafuta fundi mwenye uzoefu na ufunguaji wa injini atoe injini yote kwenye gari.
Hapo Utakua umepunguza zaidi ya kilo 500 kwenye gari lako na tatizo lako litakua limeisha
Kila rakheri
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]Kwanza jipunguze mwenyewe kwani una uzito wa kg 80+ kisha usiweke mafuta na maji halafu iondoe chasis na body yote pamoja na marimu yote na hapo uzito utakuwa umepungua kwa kg 600! Walionaje wazo?
Wadau, kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Ninajitahidi kupunguza uzito wa gari yangu toka 960kg angalau ifike 600kg!
Nia na madhumuni ya kutaka kupunguza uzito, kwanza ni kuiwezesha gari iwe nyepesi ili niweze kuendelea kuruka kwenye matuta kwa urahisi.
Pili, ni kupunguza kiwango cha wese ambacho gari inakula.
Ninapofika kwenye matuta, huwa sipendi jinsi gari inavyodunda, sasa kuhakikisha hilo nimeshaanza na kung’ofoa spare tairi kitu ambacho kimeniwezesha niweze kupunguza uzito, kwa takribani 30kg.
Sasa baada ya hapa sioni tena kitu kingine cha kung’ofoa. Sijui ning’ofoe difu!, makochi ya nyuma au?
Embu manaofahamu magari naombeni ushauri wenu. Nitazitoa wapi hizi kg mia tatu ili gari ibaki na uzito wa kg 600?