Nisaidie Kumchallenge mpenzi wangu tuna mwaka kwenye mahusiano yetu, ataje mwanamke anayempenda

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,501
Reaction score
6,649
JICHO; Habari yako magical power, nisaidie kumchallenge mpenzi wangu tuna mwaka kwenye mahusiano yetu, ataje mwanamke anayempenda.

Magical power; Kwani una wasiwasi nae?

JICHO; Hii miezi minne simuelewi kabisa, yani mawasiliano ya kutosha hakuna, ananitafuta akijisikia.

Magical power; Pole

JICHO; Asante sana

Magical power; Haya nipe mawasiliano yake na jina lake.

JICHO; 07........Anaitwa AMIRI

Magical power; Sawa nakurejea

🔴🔴🔴🔴

Magical power; Kaka habari yako

AMIRI; Safi, kwema

Magical power; Kwema kabisa, bwana mimi naitwa magical power ni mshauri wa mahusiano na maisha, mimi bwana pia nafanya challenge za mahusiano kwa wapendanao na lengo likiwa ni kudumisha na kuimarisha mahusiano. Sasa katika pitapita zangu hapa nimekutana na mdada ambaye amenisimamisha anasema anataka challenge kwa mpenzi wake aone kama na yeye anapendwaaaa.

Anasema anakupenda sana, kwake uko mwenyewe dunia nzima, anaomba na wewe utaje mpenzi wako unayempenda ambaye unamuona yeye pekee dunia nzima.

AMIRI; Mimi nina mpenzi mmoja ninayempenda alafu nina marafiki wa pembeni.

Magical power; Basi yeye amesema sio rafiki ni mpenzi wako.

AMIRI; Kama ni mpenzi basi anaitwa Naah Rashidy, nampenda sana ni zaidi ya mpenzi kwasababu tumekuwa pamoja kwa miaka minne

Magical power; Sawa hongereni, na ikiwa aliyenituma sio Naah Rashidy? Nimwambie nini?

AMIRI; Ndio maana nikasema huyo ni kama rafiki, sio mpenzi tunasogeza siku tu.

Magical power; Haya sawa, nashukuru.

🔴🔴🔴🔴

Magical power; Una voice yako huko WhatsApp, kaisikilize kisha unirudie.

JICHO; Sawa.

🔴BAADA YA KUSIKILIZA VOICE WHATSAPP 👇🏻

JICHO; Ila wanaume jamani!!!!😭 mwaka na zaidi mtu anasema mimi ni rafiki yake kumbe ana mwanamke wake huko. Mimi nashangaa kwasababu kila kitu ananipa, nikisema kila kitu namaanisha, ni hii miezi minne ndio nimeacha kumuelewa, labda wakati anakuja kwangu alikuwa amegombana na huyo mchumba wake.

Na inaonyesha siko mwenyewe😭 uuuuwiii nikapime ukimwi kama sina nitulie, yani wanaume sijui kama ni watu kweli.

Magical power; Uahaanza kunitusi tayari, kama sio watu ni nini? ni Mbuzi?

JICHO; Kwendeni huko, kwenda huko hata wewe ni walewale keng£ tu hakuna mwenye unafuu😭😭😭.

Magical power; Nyamazaaa 😔

JICHO; Niacheeeeeee!!! achana na mimiii😭😭

Magical power; Sasa mimi nimekufanya nini?

JICHO; (Akakata simu)

Magical power; 😞😞🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️
 
Kaa jinga ivi.
Yani mwehu gani akupe hela kwa kazi iyo.
 
JAMES; Kaka mwambie mke wangu awe na amani, nampenda sana na sipo tayari kumsaliti leo wala kesho hata kama tupo mbali. Najua ana wasiwasi kwasababu ndoa ya dada yake ni dhaifu, dada yake kila siku analia na mume wake na yeye anampenda sana dada yake ila sasa anaumia sana anapoona dada yake anateseka ndio maana ameamua kunifanyia challenge.

Magical power; Kwani ilikuwaje mpaka huyo dada yake akaanza kuteseka? aliolewa vipi na mwanaume Mtesi?

JAMES; Yani huyo dada wa mke wangu anajiweza sana ana pesa za kutosha, alikubali kuolewa na mwanaume wa kipato cha chini akamuwezesha akammilikisha baadhi ya mali na sasa hivi jamaa yuko vizuri kwasababu kapewa ramani ya kutafuta pesa na mwanamke. Sasa hivi anamdharau anatembea na kila aina ya mwamke mara halali nyumbani.

Mke wangu anashindwa kuelewa kwamba mimi sio limbukeni wa pesa, mimi milioni 100 milioni 150 nimeanza kuzishika enzi na enzi na nimezitafuta mwenyewe sijapewa, tofautisha kupewa na kuzitafuta mwenyewe, mimi mke wangu alinikuta niko vizuri na bado sijawahi kumchiti. Huyo shemeji yake kaaminiwa lakini anamuumiza sana mkewe, ni limbukeni.

Nampenda sana mke wangu na kwa umri huu tayari siwezi kufanya uzinzi tena, aondoe wasiwasi, kila anachotaka nampatia, juzi tu hapa tumetoka Misri Vacation, siwezi kuchukia kwamba kwanini anafanya challenge, namuelewa sana maumivu ya dada yake yanamfanya hata yeye aogope asiniamini, ila nampenda sana.

Magical power; Asante nashukuru sana.
 
Mambo ya Sekondari Haya,
Nilikua kidem changu, darasa zima wa najua nakigonga ila siku tulipoambiwa tuandike watu wenye mahusiano shuleni mimi na yule dada hatukuandikwa,Anaitwa Neema.
Ila Niliandikwa na wanawake wengine.
Basi Neema alilia kwa sauti wakati mwalimu anasoma majina darasani alipoulizwa unalia nini akasema nampenda Legacy.
Aisee nilichapwa mwalimu,(Bahati mbaya mwalimu mku alikua baba yake)
 
😂😂😂
 
SALA; Habari yako kaka magical power, mimi naomba unisaidie kufanya challenge kwa mchepuko wa mume wangu, huyu mwanamke ananinyima raha, ananikosesha amani miaka saba ya ndoa sina raha, amekuwa mchepuko sugu amefanya moyo wangu umepata majeraha ya kudumu ambayo yanakula pesa zangu nyingi kwa ajili ya kujitibu.

Mume wangu aliniambia wameachana lakini ni wiki mbili sasa naona hana raha, amemuweka huyo mwanamke profile WhatsApp, moyo wangu unaumia, nimezaa nae watoto watano lakini hajaona hata mtoto mmoja wa kumuweka frofile ameenda kumuweka huyo mwanamke. Maumivu yangu yanaongezeka siku hadi siku magical power, naomba umchallenge huyo mwanamke nijue kama kamuoa au wanapendana tu.

Magical power; Kwanini unahisi atakuwa kamuoa? Umewaza mbali sana.

SALA; Sasa kama mtu anawekwa kwenye DP ya WhatsApp kuna kuachana hapo na wamezaa mtoto mmoja.

Magical power; Kumbe wamezaa?

SALA; Eeeeh wamezaa pamoja mtoto anaitwa Hajji, nateseka mimi magical power we acha tu.

Magical power; Pole, nipe mawasiliano yake na anavyofahamika huyo mchepuko nipe na jina la mume wako.

SALA; Mchepuko anaitwa DIJA, mawasiliano yake ni 06.........

Magical power; Sawa nakurejea, unaonekana una maumivu!!!

SALA; Sanaaa, yani huyo mwanamke natamani nimfinyangeee, kwanza maneno aliyonitamkia mwezi wa nne yananifanya hata nimuogope, alinitukanaaaa!!! Yeee!!!!💔💔

Magical power; Poleee, haya nakurejea.

🔴🔴🔴

Magical power...Mbona napiga hapatikani!!

SALA; Hapatikani?

Magical power; Ndio hapatikani

SALA; Mmmm!! alafu nina muda Sijampigia, huku pia hapatikani.....labda wapo gest na mume wangu wanaendeleza walipoishia, ngoja nikupe mawasiliano ya kaka yake, nilichukuaga hii namba kwenye simu ya mume wangu walikuwa wanajadili kuhusu mtoto wao. 07......Anaitwa Rajabu.

Magical power; Sawa

🔴🔴🔴

Magical power; Kaka habari

RAJABU; Salama habari yako

Magical power; Njema kabisa, samahani naitwa magical power naongea na Rajabu kaka yake DIJA?

RAJABU; Ndio

Magical power; Sawa nina shida nae naomba mawasiliano yake hizi namba zake za mwanzo hazipatikani.

RAJABU; Mmmmh mbona DIJA tumeshamzika hii wiki ya tatu inaenda.

Magical power; Unataka kusema DIJA amefarik!?

RAJABU; Ndio, muda mrefu tunaisaka wiki ya tatu sasa!!! hayupo, kwani wewe ni nani yake?

Magical power; Rafiki tuu, basi poleni sana Mungu awatie nguvu. Haya bye 👋

🔴🔴🔴

Magical power; Sikiliza hiyo voice kisha unirudie, nimekutumia WhatsApp.

SALA; Sawa

🔴BAADA YA KUSIKILIZA VOICE WHATSAPP 👇🏻

SALA; Ariririririiiiiiiiiiiiii🤣🤣🤣🤗🤗🤗🤗🤑😇💫❤️❤️❤️❤️❤️ aii aiii aii aiiii magical power nisaidie kushangwekaaaa. Mungu amejibu maombi yanguuuu. Uuuuuuwi nalia machozi ya furaha😭🤗🤗🤗umejua kunitesa mfu weweeeeeeee!!! ulijua utaishi mileleeeee!!!!. Asante Munguuuuuu yeeeee, kwenda janamke nyok@!!!!!

Magical power; Sajakuelewa, mbona una furaha sasa wakati mwenzako kaaga, nini shida?

SALA; Achaaaaa aendeeee tena nina furaha ya ghafla magical power sijui nile nini😄😄😄 kilo ya mbuzi au kuku nusu nimpapule na kachumbali. Nimefurahiiiii. Oooooh kumbe ndio maana amemuweka profile na ana masikitiko kumbe anaomboleza.

Magical power; Ngoja mimi nikuache uendelee na shughuli ya kufurahi 🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️

🔴KUFANYA CHALLENGE NI ELFU KUMI

🔴KUOMBA USHAURI NI ELFU TANO HADI ELFU KUMI

🔴KARIBU UZUNGUMZE NAMI
 
SHANGA; Kaka magical power naomba unisaidie nipate haki yangu, jana usiku kuna wakaka wawili walinitafuta kibiashara nikaenda kuwahudumia, nimewahudumia tangu saa sita mpaka saa nane za usiku walipoona wamemaliza haja zao wakanipulizia sumu usoni nikazimia.

Nimelala tangu huo muda nikaja kuzinduka saa 11 alfajiri, hawajaniibia kitu lakini nikakuta wamenivalisha chup! mpya na dazani la chup! nyingine 12 liko pembeni💔. Nikaenda kuulinzi nje wakasema hao vijana wamepita hapa saa nane na dakika 40 usiku.

Magical power; Pole sana, ni wapi huko?

SHANGA; Manzese

Magical power; Pole 😞 sasa unawafahamu?

SHANGA; Namfahamu mmoja ambaye nilikuwa nawasiliana nae, ni dereva roli hata huyo mwenzake ni dereva pia. Nakupatia mawasiliano yake ujifanye wewe ni meneja wa hii gest mwambie sipumui aje haraka.

Magical power; Iyeee!! haupumui kwa nini? We ni jiwe?

SHANGA; Yani ili aje anilipe pesa yangu, yeye na mwenzake nawadai elfu 30.

Magical power; Sawa nipe mawasiliano yao

SHANGA; 07.......Anaitwa DERE

Magical power; Haya sawa nakurejea

🔴BAADA YA DAKIKA MBILI 👇🏻👇🏻👇🏻

SHANGA; Kaka Magical power ngojaaaa usiwapigie kwanza au umewapigia?

Magical power; Bado, kwani vipi?

SHANGA; Kumbe wameniwekea elfu 40 kwenye pochi yangu nilikuwa sijaona, amenitumia ujumbe hapa anasema pesa ipo kwenye pochi.

Magical power; Pochi gani?

SHANGA; Kwani nina pochi ngapi na wewe si pochi yangu hii ya mkononi..

Magical power; Oooh sawa, nisamehe. Ila wewe si umesema walikuwekea vitu machoni wakatoroka, vipi tena!!

SHANGA; Nilikudanganya ili unionee huruma unisaidie, nilizidiwa tu nikajikuta nimelala.

Magical power; Aibu yako, na hizo chup! ulizosema, ni kweli au uongo?

SHANGA; Chup! ni kweli, nawashukuru sana ni mara chache kupata wanaume kama hawa.

Magical power; 😖 Haya bye 👋

SHANGA; Sawa karibuu

Magical power; Nikaribie wapi?

SHANGA; Kwangu

Magical power; Shindweee!!! mfirisi....!🏇

🔴KUFANYA CHALLENGE NI ELFU KUMI

🔴KUOMBA USHAURI NI ELFU TANO HADI ELFU KUMI INATEGEMEA NA AINA YA USHAURI

🔴KARIBU UZUNGUMZE NAMI 👉
 
Mfirisi🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…