Nisaidie Kumchallenge mpenzi wangu tuna mwaka kwenye mahusiano yetu, ataje mwanamke anayempenda

Nisaidie Kumchallenge mpenzi wangu tuna mwaka kwenye mahusiano yetu, ataje mwanamke anayempenda

MOH; Habari yako magical power, na mimi naomba unifanyie challenge kwa mpenzi wangu tunapima mambo bwana naona wanawake wanafanya wacha na mimi ni jaribu kwa girlfriend wangu.

Magical power; Karibu, mpo kwenye levo gani ya mahusiano?

MOH; Sikumbuki tuko pamoja kwa muda gani haya mambo wanawake ndio huwa wanayajulia, sisi wanaume tuko bize kutafuta pesa.

Magical power; Kwahiyo haujui mahusiano yako yana muda gani?

MOH; Sijui wallah 😄😄

Magical power; Unacheka nini?

MOH; 😄😄😄😄😄😄 Hamna kitu nimefurahi tuu 😄

Magical power; Umefurahi nini? aaaaaaaaaah🤔 wewe si ndio Oscar niliongea na wewe siku ile nilitumwa kufanya challenge kwako ukataja mwanamke mwingine?

MOH; 😃😀😃😀😀😀😀😀 Sio mimi bwana

Magical power; Ni weweee!!!!

MOH; Eeeh ndio ni mimi 😃😀😃😀 dah kaka una kumbukumbu nimejitahidi kuminya sauti lakini wapi😄😄

Magical power; Ulisikia wapi sauti la kisukuma ikaminyika, eti MOH, we jamaaa daaa😃 sasa leo unataka kumchallenge nani?

MOH; Yule unajua tuliachana siku ile

Magical power; Ndio, nilimwambia akimbie mbio, we sio mwanadamu wa kawaida.

MOH; 😃😃 Uzuri hata mimi nilikuwa simpendi, hakuniuma.

Magical power; Una dharau sana, sasa kwanini haukumwambia aendelee na maisha yake? Mpaka ukangoja challenge.

MOH; Aaaah mbona kwa mwanaume hiyo ni kawaida babuuu!! Unamaindi vitu vidogo, mwanaume hachiti anatimiza wajibu, ni haki yake ya msingi kuchepuka kwasababu ameumbiwa tamaa.

Magical power; Aiseee, wala hiyo challenge yako sikufanyii haina maana, kitu kidogo wakati mwenzako bado ana maumivu...

MOH; Maumivu ya mchongo😃😃😃

Magical power; Unacheka tena, haya 40 zako zaja endelea kutumia uanaume wako kuliza mabinti, toka hapa na kachallenge kako, ghasia tupatupa wewe.
1753760106627.jpg
 
Hapo ukute hata huyo dada angefanyiwa hiyo challenge angemtaja mume mungine tofauti na AMIRI.
 
😂😂 Okay endelea na challenge mkuu.
NANA ZIPU; Kaka magical power naomba uniokoe umeniponza mwenyewe nisaidie mahusiano yangu yasiangamie mimi huyu mwanaume bado nampenda sanaaa 😭

Magical power; Nimekuponza nimekufanyaje?

NANA ZIPU; Nilisevu namba yako my love 💓 mpenzi wangu ameiona anadhani ni namba ya mpenzi wangu kaichukua anasema mtakula sahani moja na yeye nisaidiee.

Magical power; Iyeee!! 😳 ale sahani moja na mimi kwani nimemfanya nini? Mimi sikujuii 🤷‍♂️ sasa kwanini unataka kunitia matatizoni.

NANA ZIPU; magical power kuna kipindi sikuwa na mpenzi nilikuwa nimegombana nae nikasema ngoja hata nisevu hili jina marafiki zangu walionage tu hapo isionekane nipo single.

Magical power; Sasa kwani kuwa single ni vibaya? we vipiiii!!! mimi sitaki matatizo. Ndio kasema atanipigia?

NANA ZIPU; Ndio kanipiga ngumi za pua sijui hata kama nipo salama damu zinatoka nyingi😭 ongea nae umwambie wewe ni mshauri tuu!!! atakuelewa. Mawasiliano yake ni 07.....anaitwa Adam.

Magical power; Jamani mbona unaniingiza kwenye matatizo?😔 aaai.

🔴🔴🔴

Magical power; Kaka habari yako

ADAM; We mseng....................nitakukamata popote ulipo k........ni....na) (matusi yaliyoshiba)

Magical power; Nisikilize basi kaka

ADAM; Nikusikilize nini k........m wewe!!!!!! Huyo mwanamke nimemtambulisha kwetu na kila sehemu anajulikana, namhudumia kuanzia kifungua kinywa mpaka kifunga kinywa, we ...........) (matusi mazito).......Nikaona hatutaelewana nikaamua kumblock.

🔴🔴🔴🔴

Magical power; Umenikosea ujue, alafu mwanaume wako nae mbona hataki hata kunisikiliza!!! ni matusi tu.

NANA ZIPU; Kanipigia hapa anasema anaenda nyumbani kwetu kusema amenifumania...nikupe mawasiliano ya wazazi wangu uwawahi magical power jamani ndoa naitaka natakiwa kuolewa mwezi wa 10. Au mpigie tena msisitize usijali matusi yake nijali mimi, tusi haliui.

Magical power; Aaaai!! samahani kwa hili sitaweza, malizaneni wenyewe nikiingilia linaweza kuwa kubwa zaidi. Futa hilo jina andika magical power tu kawaida kwani we huwezi kuthamini husiano lako?

NANA ZIPU: Kwa wakati huo sikuwaga kwenye mahusiano nilikuwa single. Nimeshabadilisha.

Magical power; Haya bye 👋
1753762923446.jpg
 
Atakunyoosha huyo jamaa 😀
 
SALA; Habari yako kaka magical power, mimi naomba unisaidie kufanya challenge kwa mchepuko wa mume wangu, huyu mwanamke ananinyima raha, ananikosesha amani miaka saba ya ndoa sina raha, amekuwa mchepuko sugu amefanya moyo wangu umepata majeraha ya kudumu ambayo yanakula pesa zangu nyingi kwa ajili ya kujitibu.

Mume wangu aliniambia wameachana lakini ni wiki mbili sasa naona hana raha, amemuweka huyo mwanamke profile WhatsApp, moyo wangu unaumia, nimezaa nae watoto watano lakini hajaona hata mtoto mmoja wa kumuweka frofile ameenda kumuweka huyo mwanamke. Maumivu yangu yanaongezeka siku hadi siku magical power, naomba umchallenge huyo mwanamke nijue kama kamuoa au wanapendana tu.

Magical power; Kwanini unahisi atakuwa kamuoa? Umewaza mbali sana.

SALA; Sasa kama mtu anawekwa kwenye DP ya WhatsApp kuna kuachana hapo na wamezaa mtoto mmoja.

Magical power; Kumbe wamezaa?

SALA; Eeeeh wamezaa pamoja mtoto anaitwa Hajji, nateseka mimi magical power we acha tu.

Magical power; Pole, nipe mawasiliano yake na anavyofahamika huyo mchepuko nipe na jina la mume wako.

SALA; Mchepuko anaitwa DIJA, mawasiliano yake ni 06.........

Magical power; Sawa nakurejea, unaonekana una maumivu!!!

SALA; Sanaaa, yani huyo mwanamke natamani nimfinyangeee, kwanza maneno aliyonitamkia mwezi wa nne yananifanya hata nimuogope, alinitukanaaaa!!! Yeee!!!!💔💔

Magical power; Poleee, haya nakurejea.

🔴🔴🔴

Magical power...Mbona napiga hapatikani!!

SALA; Hapatikani?

Magical power; Ndio hapatikani

SALA; Mmmm!! alafu nina muda Sijampigia, huku pia hapatikani.....labda wapo gest na mume wangu wanaendeleza walipoishia, ngoja nikupe mawasiliano ya kaka yake, nilichukuaga hii namba kwenye simu ya mume wangu walikuwa wanajadili kuhusu mtoto wao. 07......Anaitwa Rajabu.

Magical power; Sawa

🔴🔴🔴

Magical power; Kaka habari

RAJABU; Salama habari yako

Magical power; Njema kabisa, samahani naitwa magical power naongea na Rajabu kaka yake DIJA?

RAJABU; Ndio

Magical power; Sawa nina shida nae naomba mawasiliano yake hizi namba zake za mwanzo hazipatikani.

RAJABU; Mmmmh mbona DIJA tumeshamzika hii wiki ya tatu inaenda.

Magical power; Unataka kusema DIJA amefarik!?

RAJABU; Ndio, muda mrefu tunaisaka wiki ya tatu sasa!!! hayupo, kwani wewe ni nani yake?

Magical power; Rafiki tuu, basi poleni sana Mungu awatie nguvu. Haya bye 👋

🔴🔴🔴

Magical power; Sikiliza hiyo voice kisha unirudie, nimekutumia WhatsApp.

SALA; Sawa

🔴BAADA YA KUSIKILIZA VOICE WHATSAPP 👇🏻

SALA; Ariririririiiiiiiiiiiiii🤣🤣🤣🤗🤗🤗🤗🤑😇💫❤️❤️❤️❤️❤️ aii aiii aii aiiii magical power nisaidie kushangwekaaaa. Mungu amejibu maombi yanguuuu. Uuuuuuwi nalia machozi ya furaha😭🤗🤗🤗umejua kunitesa mfu weweeeeeeee!!! ulijua utaishi mileleeeee!!!!. Asante Munguuuuuu yeeeee, kwenda janamke nyok@!!!!!

Magical power; Sajakuelewa, mbona una furaha sasa wakati mwenzako kaaga, nini shida?

SALA; Achaaaaa aendeeee tena nina furaha ya ghafla magical power sijui nile nini😄😄😄 kilo ya mbuzi au kuku nusu nimpapule na kachumbali. Nimefurahiiiii. Oooooh kumbe ndio maana amemuweka profile na ana masikitiko kumbe anaomboleza.

Magical power; Ngoja mimi nikuache uendelee na shughuli ya kufurahi 🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️

🔴KUFANYA CHALLENGE NI ELFU KUMI

🔴KUOMBA USHAURI NI ELFU TANO HADI ELFU KUMI

🔴KARIBU UZUNGUMZE NAMI
Umetoa kwa fahari media kule tunga zako acha kucopy😂😂😂
 
Back
Top Bottom