Nisaidie Kumchallenge mpenzi wangu tuna mwaka kwenye mahusiano yetu, ataje mwanamke anayempenda

MOH; Habari yako magical power, na mimi naomba unifanyie challenge kwa mpenzi wangu tunapima mambo bwana naona wanawake wanafanya wacha na mimi ni jaribu kwa girlfriend wangu.

Magical power; Karibu, mpo kwenye levo gani ya mahusiano?

MOH; Sikumbuki tuko pamoja kwa muda gani haya mambo wanawake ndio huwa wanayajulia, sisi wanaume tuko bize kutafuta pesa.

Magical power; Kwahiyo haujui mahusiano yako yana muda gani?

MOH; Sijui wallah πŸ˜„πŸ˜„

Magical power; Unacheka nini?

MOH; πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ Hamna kitu nimefurahi tuu πŸ˜„

Magical power; Umefurahi nini? aaaaaaaaaahπŸ€” wewe si ndio Oscar niliongea na wewe siku ile nilitumwa kufanya challenge kwako ukataja mwanamke mwingine?

MOH; πŸ˜ƒπŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Sio mimi bwana

Magical power; Ni weweee!!!!

MOH; Eeeh ndio ni mimi πŸ˜ƒπŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜€ dah kaka una kumbukumbu nimejitahidi kuminya sauti lakini wapiπŸ˜„πŸ˜„

Magical power; Ulisikia wapi sauti la kisukuma ikaminyika, eti MOH, we jamaaa daaaπŸ˜ƒ sasa leo unataka kumchallenge nani?

MOH; Yule unajua tuliachana siku ile

Magical power; Ndio, nilimwambia akimbie mbio, we sio mwanadamu wa kawaida.

MOH; πŸ˜ƒπŸ˜ƒ Uzuri hata mimi nilikuwa simpendi, hakuniuma.

Magical power; Una dharau sana, sasa kwanini haukumwambia aendelee na maisha yake? Mpaka ukangoja challenge.

MOH; Aaaah mbona kwa mwanaume hiyo ni kawaida babuuu!! Unamaindi vitu vidogo, mwanaume hachiti anatimiza wajibu, ni haki yake ya msingi kuchepuka kwasababu ameumbiwa tamaa.

Magical power; Aiseee, wala hiyo challenge yako sikufanyii haina maana, kitu kidogo wakati mwenzako bado ana maumivu...

MOH; Maumivu ya mchongoπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Magical power; Unacheka tena, haya 40 zako zaja endelea kutumia uanaume wako kuliza mabinti, toka hapa na kachallenge kako, ghasia tupatupa wewe.
 
Hapo ukute hata huyo dada angefanyiwa hiyo challenge angemtaja mume mungine tofauti na AMIRI.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ Okay endelea na challenge mkuu.
NANA ZIPU; Kaka magical power naomba uniokoe umeniponza mwenyewe nisaidie mahusiano yangu yasiangamie mimi huyu mwanaume bado nampenda sanaaa 😭

Magical power; Nimekuponza nimekufanyaje?

NANA ZIPU; Nilisevu namba yako my love πŸ’“ mpenzi wangu ameiona anadhani ni namba ya mpenzi wangu kaichukua anasema mtakula sahani moja na yeye nisaidiee.

Magical power; Iyeee!! 😳 ale sahani moja na mimi kwani nimemfanya nini? Mimi sikujuii πŸ€·β€β™‚οΈ sasa kwanini unataka kunitia matatizoni.

NANA ZIPU; magical power kuna kipindi sikuwa na mpenzi nilikuwa nimegombana nae nikasema ngoja hata nisevu hili jina marafiki zangu walionage tu hapo isionekane nipo single.

Magical power; Sasa kwani kuwa single ni vibaya? we vipiiii!!! mimi sitaki matatizo. Ndio kasema atanipigia?

NANA ZIPU; Ndio kanipiga ngumi za pua sijui hata kama nipo salama damu zinatoka nyingi😭 ongea nae umwambie wewe ni mshauri tuu!!! atakuelewa. Mawasiliano yake ni 07.....anaitwa Adam.

Magical power; Jamani mbona unaniingiza kwenye matatizo?πŸ˜” aaai.

πŸ”΄πŸ”΄πŸ”΄

Magical power; Kaka habari yako

ADAM; We mseng....................nitakukamata popote ulipo k........ni....na) (matusi yaliyoshiba)

Magical power; Nisikilize basi kaka

ADAM; Nikusikilize nini k........m wewe!!!!!! Huyo mwanamke nimemtambulisha kwetu na kila sehemu anajulikana, namhudumia kuanzia kifungua kinywa mpaka kifunga kinywa, we ...........) (matusi mazito).......Nikaona hatutaelewana nikaamua kumblock.

πŸ”΄πŸ”΄πŸ”΄πŸ”΄

Magical power; Umenikosea ujue, alafu mwanaume wako nae mbona hataki hata kunisikiliza!!! ni matusi tu.

NANA ZIPU; Kanipigia hapa anasema anaenda nyumbani kwetu kusema amenifumania...nikupe mawasiliano ya wazazi wangu uwawahi magical power jamani ndoa naitaka natakiwa kuolewa mwezi wa 10. Au mpigie tena msisitize usijali matusi yake nijali mimi, tusi haliui.

Magical power; Aaaai!! samahani kwa hili sitaweza, malizaneni wenyewe nikiingilia linaweza kuwa kubwa zaidi. Futa hilo jina andika magical power tu kawaida kwani we huwezi kuthamini husiano lako?

NANA ZIPU: Kwa wakati huo sikuwaga kwenye mahusiano nilikuwa single. Nimeshabadilisha.

Magical power; Haya bye πŸ‘‹
 
Atakunyoosha huyo jamaa πŸ˜€
 
Umetoa kwa fahari media kule tunga zako acha kucopyπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…