Nisaidie mwanangu, muulize mama yako, kwanini ananinyima unyumba?

Hili ni somo fupi lakini lenye ujazo mzito sana kwa vijana.

Sio vyema kuingilia ugomvi wa baba na mama yako.
Ingawa nivyema ukawaamua baba na mama yako na kuwahisi wasigombane iwapo wataanza kupasuana ikiwa upo nyumbani.

Hapa tumepata mfano mzuri kabisa wa jibu alilopata kijana kutoka kwa baba yake baada ya kutamani kudadisi wapi hasa mama anamkosea baba, lakini pia kuna mchangiaji amecomment kwamba kijana alipaswa akasikilize na upande wa pili yaani kwa mama...πŸ˜‚πŸ˜‚

Kwa mtazamo wangu... hili lingekua kosa lingine la pili kwa kijana kumuuliza mama yake kwanini wanapigana na baba nini hasa chanzo.

Je na mama angejibu kwamba (baba yako sikuizi ananipelekea moto hadi nachubuka...πŸ™„πŸ™„

Hapo bilashaka kijana angekua ameipata laana aliokua anaitafuta.

Nami nasisitiza kwamba ugomvi wa baba na mama mtoto usiingilie, labda unaweza ukawaamua ili wasipasuane na usitake kusikiliza kwamba nani kamkosea nani.
 
Mtuvumilie tu,Kuna umri kiu inakata kabisa.....ukiona mtu mzima mama bado anaendekeza libeneke huyo ana matatizo yake
 
Samahani wadau mm n mgeni katika jukwaa ili pendwa naomba mtu aliyepo kiteto kibaya tuwasiliane pm kuna masuala mbal mbal ya kibiashara nataka anijuze please kama yuko anicheki pm.
 
Ni changamoto sana na watu tulipaswa kujua moja kati ya mahitaji makubwa ya binadamu ni unyumba.
Wapo wanaosingizia kuchoka, kukinai, kukumbuka makosa aliyotendewa na mwanaume wake, msongo wa mawazo nk
Ila wengine basi tu huwa kuna mahali wanapata maji kwahiyo hawana kiu, badala yake wanatesa walio waweka ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…