Kama nimekupata vema, inaonekana ushahidi ulitolewa na upande wa mashitaka ila mwisho wa siku ikaonekana hautoshi kukutia hatiani. Hapa ndipo ugumu unapokuja. i kila mara unapopelekwa courtini upatikane na hatia. Pia si kila kesi mtuhumiwa anaposhindwa anakuwa na haki ya kufungua shauri la madai. Sheria ya jinai inaeleza kuwa kama kuna "reasonable suspicion" kuwa mtu ametenda kosa la jinai basi na apelekwe court. Kwa uelewa wangu, mara nyingi ni vigumu kuthibitisha malicious prosecution labda uoneshe kuwa kulikuwa na nia mbaya na mashitaka dhidi yako yalitungwa. Lakini kama kweli yalikuwepo mazingira ya kukuhusisha wewe na nyara hata kama ki-ukweli (in fact) huhusiki, basi Jamhuri ilikuwa sahihi kukushtaki. Kupatikana na hatia au la ni suala lingine. Vinginevyo court zetu zingejaa case za malicious prosecution kama mtu yeyote anayeshinda kesi ana haki ya moja kwa moja kushtaki katika tort.