Nisaidie ushauri...ndoa imenishinda

Nisaidie ushauri...ndoa imenishinda

swali imefunga ndoa rasmi au ndo kuzalishana na kujimilikisha undoa...? ushauri wewe ndiyo unayejua uchungu unaopata sasa maamuzi yapo kwako,... ila kama ni mimi kwa sabuabu kiuchumi hayupo vizuri nishampiga kapuni mda mrefu tu bila kujali chochote.................. mapenzi ya siwe kigezo cha kunipa karaha maisha yangu yote nisione raha ya maisha.....dharau lete mfukoni upo vizuri haina shida, unadharau alafu unapumulia mashine kwa kweli me siweziiii na Mungu Anisaidie nisipate mume wa ivyo amen
Typical chagga woman! Mbesa mbele km tai
 
Typical chagga woman! Mbesa mbele km tai

sasa mkuu pesa huna mapenzi huna sasa hapo naishi na wewe ili iweje nikuvumilie wakati yeye anakula raha,..... yani niikose paradiso ya duniani na ya mbinguni nikiikosa pia itakuaje..... kwa hiyo mtu uwe umeeshi maisha ya kijehanamu tokea duniani hadi mbinguni sitaki....... USIKOSE MAPENZI NA KUKOSA PESA PIA NA RAHA.
 
Pole sana,simama hayo ni mapito2 ndugu yangu,simama kijasiri kiuanamke mwombee mumeo atoke katika mikono ya ibilisi. Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake. Na mke ni mlinzi kwa mumewe ni maombi na hekima hapo vyahitajika kuisimamisha ndoa.
 
Shosti pole sana,Siwezi kukwambia ondoka muache mumeo lakini kama ningekua mimi naona hata kunisahau ameshanisahau
yani kwenye raha akale na mpenzi wa nje shida ndio ule nae wewe kwani wewe hujui raha au hujui kutumia? kwakwelu shosti huyo sio mume anajishikiza tuu akifanikisha ataondoka tena lakini angalia moyo wako vile unavyokutuma usije hama mji halafu ukampigia cm mtoto anataka kukusalimia,fanya ukiondoka ndio umeondoka,Jengine mawifi shosti katika hao mawifi atakae kuona wifi sawa asiekuona wifi basi shida yako mume sio wifi wala shemeji mwenye gubu hao watu mie hata hawanilazi macho,muhimu mama mkwe na baba mkwe ..............


Uko sahihi, il ahao watu wanaoitwa MAWIFI sina hata hamu nao ni watu wabaya sana kwa hii dunia
 
sasa mkuu pesa huna mapenzi huna sasa hapo naishi na wewe ili iweje nikuvumilie wakati yeye anakula raha,..... Yani niikose paradiso ya duniani na ya mbinguni nikiikosa pia itakuaje..... Kwa hiyo mtu uwe umeeshi maisha ya kijehanamu tokea duniani hadi mbinguni sitaki....... Usikose mapenzi na kukosa pesa pia na raha.

he he he hatariiiiiii!
 
kama anakurudisha nyuma usimuache ila mtenge kwa mda ajifunze, asikufanye ngazi ya kupandia,
kuachana marukfuku ila kutengana inaweza ikarudisha afya ya ndoa
 
^^
Ndoa maji ya shingo.. Hata ukiondoka mtoto wenu ni daraja litakalowaunganisha.
Mnamsaidia mtoto kukosa mapenzi ya wazazi wawili.
^^

Naomba kuuliza...hivi ni sahihi mtoto kuona mama anatukanwa na kupigwa mbele zake? Hata kama umri wake hauzidi miaka 5, mimi naona ajitenge kwa muda aendelee na mambo yake kwanza akiwa nyumbani kwao(kwa wazazi wake) mpaka mume atakapopata akili ya kumfuata..na kuomba msamaha si chini ya mara 3
 
Tatizo lenu ni hayo mahusiano yenu ya nje. Kwa jinsi unavyoeleza inaonesha nyie hamuaminiani na hamko commited to ur relationship. Mara nyingi watu wanaotokatoka nje sana wanakuwa hawajiamini ndani so kutoka ni kama kunawapa emotional stability ambayo waliikosa kwa uvivu wao wakutokutafuta kuwaamini wenzi wao.

Hata kupigwa, kukosa kazi, starehe vyote vinaanzia huko. Wewe utaenda kwenu utaolewa na mwingine na yeye ataoa mwingine lakini ndoa zenu zitakuwa hivyohivyo.
What to do;

  • Ongea na mumeo nendeni kwa wataalamu wa mahusiano, hasahasa viongozi wa kiroho(kidini). Mkaungame dhambi zenu hasa ile kubwa ya kuvunja viapo vya ndoa yenu takatifu. Both of u have been hypocrites and untrustworthy for u breached u r marital contract



  • Mkaapiane upya, mjifunze kupendana upya, mjifunze kuwa waaminifu na pia mjifunze kuaminiana. Kisha muanze ndoa upya (Na msiache kwenda honeymoon).


  • Usitegemee kumbadili huyo mwanaume ndo utapata furaha. Shetani wako ni past yako and its always there to haunt u!
  • Kila la heri

well said....
 
1. utii nidhamu na heshima kwa mumeo ndugu na jamaa zake wanaowazunguka.
2. Kusali,kusoma dini, kwa wote yeye na wewe na watoto
3. Kuomba idhini kwa mume kwa kila jambo unalotaka kulifanya
4. Haitakiwi kusimamia misimamo isiyo kubarika ktk dini inayoweza kuhatarisha ndoa yenu
5. Waonyeshe upendo wazazi/mzazi hatakama ni vigumu kwako jitahidi kuficha hisia zako
6. Mwanaume ni nguzo ya familia unapaswa kutii na kufuata tarataratibu zote za mume ili mradi hatoki ndani ya mafundisho ya imani yenu (dini)
7. Pia hutakiwi kuwa na sauti ya juu kuliko mume wako na jambo la kulia lia bila sababu za msingi halitakiwi
8. Usiwe ni kikwazo cha mume kutafuta lizki halali na kinyume chake umpe moyo na nguvu katika hilo
9. Kuwa na rafiki wema ni jambo zuri sana na kinyume chake ni baya
10. Elimu kwa watoto ni muhimu hakikisha wanaenda madras na shule kwa kuwa wewe ndio unaeshinda nao hapo nyumbani.
11. Jifunze kushukuru kwa kila neema unayopata
Kwa hayo yote mkiyafuata naamini hapatakuwepo na ugomvi .:tape::tape:
 
Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 30. Nina mtoto mmoja. Wakati wa usichana wangu...nilikua kicheche sana na niliishi maisha ya gharama sana na nilibahatika kupendwa na watu wengi sana wenye pesa na wasio na pesa....na ilifikia hatua nikaamua kuacha hayo mambo na kustick na mtu mmoja ambae alikua mwanafunzi wa chuo ambae nilikua nampenda na kuhisi atakua mume wa maisha yangu na ndie niliyezaa nae.


Niliamua kuokoka na kua na hofu ya Mungu. Sikutaka tena mahusiano ya nje. Kwasababu hakukua na kipya kwangu. Kama starehe nilishafanya sana.


Maisha yakaanza...mume wangu alikua ananipenda. Lakin kwasababu ya uzuri wangu wanamme hawajaacha kunisumbua kila leo natongozwa. Mume wangu anajua background yangu...na kwakweli amekua msaada mkubwa katika maisha yangu.


Ni mwanamme anayependa na mwenye matamanio mazuri katika maisha yetu. Kuna ugonjwa mkubwa umenipata na yeye hapo alikubali kua bega kwa bega na mimi mpaka mwisho.

Nikweli alikubaliana na hali yangu lakini kadri siku zinaenda anakua na lugha chafu...kejeli. .dharau..matusi..na kunipiga na kuanzisha mahusiano nje. Mbaya zaidi hua anakuja kuniambia uchafu wote anaoufanya nje.

Alikua na kazi nzuri...lakin ikaisha kwasasabu ya kunidharau na kuchezea pesa na mwanawake wa nje ambae ilifikia mahala anampa simu yake anapokea.


Wakati anafanya yote hayo sikua na faraja na ndipo nilipoamua kutafuta mwanamme wa kuniliwaza nikiwa nimeshakata nae tamaa.

Soon mume alikuja na kunikuta na meseji ya huyo bwana na nikakili kua nina uhusiano nae. Mume wangu akanisamehe na nikamhaidi sitarudia tena lakin cha kushangaza anaenda kwa boss wangu kueleza yanayotokea nyumbani na kunitangaza kwa watu juu ya ugonjwa nilionao na mbaya zaidi bado anawasiliana na mwanamke wake mpaka muda huu. Na huyo mwanamke anapata kiburi cha kunikutaka na kunidharau na kunieleza madhaifu yangu ya magonjwa ambao ambayo mume wangu alimusimulia.


Nazidi kuumia zaidi nnapojua familia ya mme wangu inamfahamu huyo mwanamke wa nje na wanawasiliana na wifi zangu.


Wakati niko peke yangu nikifanya miradi ya maendeleo ambayo hata mume wangu alikua haijui....na iliniwezesha kujikimu kimaisha na mtoto wangu.

Sasa akarudi amerudi kwangu akiwa hana kazi...na akitaka kuanza maisha na mimi huku akisaidiwa mtaji wa biashara na ndugu zake ili tuweze kuishi kama familia.


Lakin mbaya zaidi..simu yangu yake..ya kwake yakwake...na anahisi bado nipo na mahusiano na yule mwanamme. Na hata ninapokwenda kwenye biashara zangu ananichunga na kuniwekewa mipaka ya kufanya kazi.


Akiwa kwangu...hatoi mahitaji wala kujishughulisha na chochote. Na anakua anaishi kwa kunitafutia sababu mpaka anataka kuniua. Hapa nilipo kanipiga sana mpaka nikapelekwa hospital.



Naombeni ushauri wenu ushauri. ..nataka nirudi kwetu na mtoto wangu nina kazi nina uwezo wa kufanya biashara..hapa nilipo nafatilia uhamisho.
piga simu namba 117 watakushauri vizuri ni bure kabisa.
 
Pole sana. Mi nafikiri ni bora kuvumilia yana mwisho hayo. Kama wewe uliishi maisha ya anasa na starehe enzi za ujana wako lakini ukaamua kuacha kwa hiari yako, vivyo hivyo nae ataacha tabia zake mbaya kwa hiari yake. By the way, bado msichana mdogo sana wewe (30) ingawa unajiita mama. Ukiachana na mume wako definately utaolewa tena (uzuri wako) na huyo wa pili ataanza tena masimango, sasa hivi kuhusu mtoto wako (siwezi kulea mtoto wa mwenzangu). Kama ulivyosema umeokoa, basi omba mungu na ombea mumeo abadilike.

Goodluck!
 
hayo ni majanga yaliyokupata ambayo hutakiwi kumshirikisha mtu, ww wajua lipi ni bora kulifanya!
 
Jamani hivi wanawake tuna nini? mtu akupige mpaka ulazwe hospitali bado unavumilia na kuuliza watu eti wakupe ushauri????? Doh ushauri upi? kwamba utayarishe jeneza?? ANZA ANZA usisubiri akuuwe, mapenzi hapo HAKUNA!!!!!:shocked:
 
Naomba kuuliza...hivi ni sahihi mtoto kuona mama anatukanwa na kupigwa mbele zake? Hata kama umri wake hauzidi miaka 5, mimi naona ajitenge kwa muda aendelee na mambo yake kwanza akiwa nyumbani kwao(kwa wazazi wake) mpaka mume atakapopata akili ya kumfuata..na kuomba msamaha si chini ya mara 3

^^
Nakubaliana na mtazamo wako Chujio akili ya mtoto hunasa upesi matukio ya utotoni na si haki mtoto kuyaona hayo (domestic women violence)
Lakini nachojaribu kutazama ni kuwa hawa hawana nia ya kuachana na kurudiana maana ndoa yao ipo ktk kundi la ndoa zisizo na mlango,,hivyo madhara ya kutengana ni chanzo cha mtoto kuishi kwa sonono.
Zaidi ni kuwa kama wanashida na ngumi wajifungie chumbani watwangane,wakichoka wapumzike pasipo mtoto kujua. Trust me Chujio ndoa zenye mtindo huu zipo nyingi
^^
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom