Nisaidie ushauri wenu muhim sana kwangu

Nisaidie ushauri wenu muhim sana kwangu

Sija haja ya kukupa pole maana sioni tatizo hapa, kuwa positive sio tatizo kabisa unatakiwa kuikubali hali yako, kuna watu walio kwenye ndoa mmoja kati ya wanandoa yuko positive na mwingine yuko negative lkn wanaishi miaka mingi bila ya kumuambukiza mwingine ilimradi tu kuepuka mazingira yote hatarishi ambayo unaweza kumuambukiza mwenzi wake.

Kwa kuwa uko mjamzito hiki ni kipindi muhimu sana ktk maisha ya kijacho chako, nenda kwa wataalamu wakupe elimu ambayo itakusaidia kupata mtoto ambaye hana maambukizi ya VVU, unajua mtoto anaweza kuambukizwa akiwa tumboni, kipindi cha kujifungua na baada ya kumzaa. sasa basi nenda kapate elimu kwa kimombo inaitwa PMTCT (PREVENTION TO MOTHER CHILD TRANSMISSION) ni muhimu sana pindi unavyozidi kuchelewa kwenda klinic ndo unavyohatarisha maisha ya mwanao aliye tumboni.

Usiwe na wasiwasi dadaaa siku hizi UKIMWI sio tishio tena, kwani waweza peta for many years bila matatizo, ila unatakiwa kuikubali hali hiyo na hii utaipata zaidi utakapokwenda kwa wataamu wa VCT watakupa ushauri mzuri. Pia baada ya kujua hali yako jiunge kwenye club zinaitwa post testing club zinasaidia sana
 
nyamayao ........hakuna atakaedesa na kuja hapa kusema mumewe ana VVU na yeye ana hofu. huyu tatizo analo kweli

ushauri wangu kwako nasra ni: nendeni nyote wawili mkapime tena (katika hospitali nyengine.........kuna watu ambao wamewahi kupima Aga Khan ikakutikana kumbe ilikosewa, pia namjua mtu alipima muhimbili akaambiwa anao akenda hospitali nyengine kama tatu akaambiwa hana)

ukishakujua kama mume wako anao na wewe huna ..........hapo kaa chini omba mungu akupe nguvu za kuweza jambo hilo kwanza.

kisha onana na wataalamu watakupa namna ya kukabiliana na suala hilo

Gaijin asante sana kwa ushauri wako na nashukuru sana kwa kumuelewesha Nyamayao, hivo kweli mi naweza kudesa alafu nipitie comments za watu wote kusoma itanisaidia nn? naomba wale waelevu waelewe kuwa nina tatizo kama ulivoelewa wewe Gaijin mungu akubariki sana
 
Asante mpendwa nasubiri hiyo pm! Nawashukuru na wengine wote kwa mawazo yenu

Ushauri wangu kazana kula mchicha kwa kwa wingi glasi ya maziwa kila siku kazana kula matunda kwa wingi.
Hapa ni ushauri tu ulifanya jambo la maana kwenda kupima na ukabaini jamaa yupo + ukakokosea kumvulia huku ukijua ni + zingatia tu ushauri wa Dr. ili kiumbe kizaliwe salama salmini.
 
Mungu akutangulie!

ondoa wasiwasi nakwambia utapimwa na utaonekana ni _ve bado!! Kwa Jina la Mungu wetu mwenye upendo!
 
Back
Top Bottom