Nisaidieni, Hii sio Dengue jamani?

Madame B

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2012
Posts
31,155
Reaction score
35,683
Niko nyumbani siku ya tatu leo, naumwa sana. Nimeenda kupima ugonjwa hospitali kama tatu, wameniambia ni Malaria.

Dalili ninazozisikia ni:

1. Kuumwa kipanda uso, mpaka macho huwa yanatoa machozi.

2. Homa kali hasa sehemu za tumboni na kifuani.

3. Nakohoa sana.

4. Naharisha sana.

Ila hospitali wanasema ni Malaria, au hawana vipimo vya kupima huo ugonjwa?

Nisaidieni, Naogopa sana kufa.
 
Aisee kuna dr wa mwananyamala naskia kavuta jana. Nenda hospitali ya sirikali ukapimwe mndele.

natanguliza rambirambi just in case
 
Homa ya Dengue
Nitajitahidi kutafsiri kwa Kiswahili ila naomba radhi pale ambapo nitakosea
Dalili zake huanza siku 4 mpaka 10 baada ya maambukizi. Dalili zenyewe ni:
1. Homa kali naya ghafla- sudden high, fever
2. Kichwa kuuma sana- severe headache
3. Macho kuuma- pains behind the eyes
4. Maumivu makali ya misuli na joints- Severe joint and muscle pain
5. Kutapika
6. Mabaka kwenye ngozi- skin rash
7. Kutokwa damu hasa puani
8. Kichefuchefu
Tuna ambukizwaje ugojwa
Mbu ndo chanzo chake na wanasambaza virusi vya huu ugonjwa.
Tumtibu vipi mgonjwa
Kwakuwa ni virus basi hakuna dawa maalum ya kutibu ila dakari au wewe na mimi twaweza fanya yafuatayo:
1. Tumia oral yaani nunua pakti ya oral (chumvi na sukari) mpe mgonjwa anywe. Hii ni kurudishia maji yaliyopotea kwa kutapika na homa kali.
2. Mpe Panadol au paracetamol
3. USIMPE MGONJWA ASPIRINI HIYO NI HATARI KWANI ITACHOCHEA INTERNAL BLEEDING


Tiba mbadala

Nchi kama Sirilanka, India, na Malaysia wao wanaitibu kwa majani ya mpapai.
1. Chuma jani la mpapai na ulioshe
2. Saga au twanga au blend kasha kamua upate juisi yake.
3. Mpe mgonjwa vijiko 2/3 – india wanachanganya na asali kidogo

Preparation of Papaya leaf juice for curing dengue fever - YouTube
Tazama na hiyo video
 

Sasa kama umeambiwa una malaria umechukua hatua gani kwamba huitibu ama nini? ila Dengue ni malaria tu ..kunywa dawa..nimetoka kutandikwa last week mpaka kilo 3 zimenipungua maana mgongo na tumbo vili tight balaaa..acha woga Belinda!
 
Tafadhali anzisha uzi haraka juu ya hizi dalili na tiba mbadala, na tuwaombe mods waiwekee umuhim mkubwa sana ili watanzania waelewe juu ya hii dengue fever



 
Mnaonaje tukimchangia incredible afungua kizahanati,maana kasi ya dengua inatisha.
 

thanks sana maana umetufungua wengi sana, be blessed
 
Nilikuwa na mpango wa kuja Daslam ila mmh, naona itakuwa ngumu siji mpaka Dengue iishe kabisa
 
yaani nimetanguliza salamu za rambirambi kama rais wetu mpendwa. Kwani anapotumaga salamu za rambirambi kwa rais wa malawi anatuma na hela kwa mpesa?:shock:
hyo sentensi ya mwisho?unamaanisha unamtumia hela aende kwenye vipimo?
au unasubiri afe uwe wa kwanza kutuma rambi2
 
Madame B pole sana tupe update unavyoendelea na pia zingatia ushauri wa. Incredible hapo juu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…