Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante ndugu inaweza kuwa mimba imetoka?damu inatoka nyepesi sana.
Asante ndugu naelekea hospital sijui itakuwaje
Asante ndugu kwa ushauri sijui kwa nn karudi yasinge nitokea haya jamani furaha yote ya ujio wa mume wangu imeniisha kwa kweli.
Asante Mungu,asante jf
nimekwenda hospital nimepiga utra sound mimba haijatoka.nimepewa dawa na
kuelezwa cha kufanya.Asanten kwa kunitia moyo.Mungu awabariki ila
wanasema ukipata tatizo kama hilo unachotakiwa kuwahi hospital.
tehe..tehe... uko juu na kazi yako unakumbuka hata tarehe? kiukweli jamii forum ni zaidi ya familia zetu wapo watu wanaweza kujitoa kwa shida za wengine kutoka rohoni mwao gooood!19 Sept Ulitueleza kuwa mimba yako ni ya mwezi mmoja unusu, na hapa waeleza kuwa tar 6 Oct utatimiza miezi mitatu...
Mbona kama unatuzingua akili zetu we mwanamke? Tokea tar 19 hadi hiyo tar 6 huo muda hata ujumlishe vipi hauwezi tengeneza mwezi mmoja unusu ili kufanya ujauzito wako uwe wa miezi mitatu.
Anyway, mjamzito kutokwa damu si jambo la kawaida na yakupasa ufike hospitali mapema kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kuna sababu kadhaa ambazo huweza kupelekea mama mjamzito kutokwa na damu nyepesi 'spotting'.
1. Ngono 'Sex'
Wakati wa ujauzito damu nyingi huwa inakimbilia kuelekea shingo ya kizazi 'cervix'. Hivyo hupelekea ukuaji usio wa kawaida wa 'cervix' na hii kuna uwezekano ikasabisha damu ndogo kutoka wakati wa kungonoka.
2. Miscarriage au Ectopic Pregnancy
Kama kutokwa huko kwa damu kuliambatana na hali yoyote ya maumivu ya tumbo 'maumivu kama yale ya MP'...basi kuna uwezekano mimba ikawa imeharibika au mimba imetungwa nje ya mji wa mimba.
Karibia robo ya wanawake wajawazito hutokewa na hii hali na nusu ya wanawake hawa huishia kuwa na 'miscarriage'.
3. Infections
Wakati mwingine kutokwa na damu nyepesi ambayo haihusiani na hali ya ujauzito husababishwa na vaginal infections mathalani 'yeast infection', 'bacterial vaginosis' au hata magonjwa mengine ya zinaa 'STD's'.
Maambukizi haya hupelekea kuvimba au kuwa na hali ya uwasho kwa shingo ya uzazi, na kama mama mjamzito atafanya ngono kuna uwezekano wa kutokwa na damu nyepesi.
Ushauri;
Nenda hospitali wakufanyie vipimo kadha wa kadha ili kutambua ni nini haswa chanzo cha hali hiyo.
Asante Mungu,asante jf nimekwenda hospital nimepiga utra sound mimba haijatoka.nimepewa dawa na kuelezwa cha kufanya.Asanten kwa kunitia moyo.Mungu awabariki ila wanasema ukipata tatizo kama hilo unachotakiwa kuwahi hospital.
Next time jaribu kuwa makini...
Asante ndugu kwa ushauri.jamani kama nimekosea cku nisamehe kuchanganyikiwa huku kama nilisema mwezi 1 na nusu nilikosea ilikuwa miwili na nusu kwenda mitatu.sina mama jaman ndo mana kila kitu nakimbilia humu,asante.