Mimi sio mtaalamu wa Elimu Maalumu, hivyo sikumbuki vizuri maneno ya kitaalamu. Anachosema huyu ndugu chaweza kuwa sahihi. Kuna mataizo binafsi katika matamshi, kiasi kwamba mtu anakuwa anaongea mfululizo (kama cherehani), anaongea neno moja moja, au mafungu mafungu, watu wengi husema ni kigugumizi, wengine kuongea kwa sauti ya chini sana.
Hata mimi ni mhanga, kama yeye, kwa kulitambua hilo, sijawahi kuomba nafasi ya kuzungumza kwenye mhadhara. Hata kwa kusoma, bado napata changamoto kiasi.