Nisaidieni jamani niweze kuongea vizuri

Nisaidieni jamani niweze kuongea vizuri

Arteta_21

Member
Joined
Feb 25, 2013
Posts
12
Reaction score
2
Jamani mi ni kijana wa miaka 18 tatizo langu ni kwamba nimekuwa nikishindwa kuongea maneno kwa mtiririko nimekua nikiongea huku nikiacha maneno mengine mara naanzia kati sentensi ninazoongea hazieleweki hivyo naomba mnisaidie kama kuna tiba mbadala ili niondokane na hili tatizo ambalo limekua likinikosesha amani hasa tukiwa na vijana wenzangu
 
Hivi Tanzania kuna sehemu wanatoa "speech therapy" ? Unashindwa kuongea kwa mtiririko kama kigugumizi au unashindwa kupangilia maneno sawa lakini huna kigugumizi?

Haya ni matatizo fulani ya kuwahiwa tangu utotoni.

Wewe umeanza kuwa hivyo tangu utoto au nini kilitokea ukawa hivyo?

Vipi kusoma, unaweza kusoma vizuri?
 
Hii hali nimeigundua baada ya kufika form four mwaka jana kwenye debate. Kwa hiyo sijui kuwa ni kigugumizi au la! Na kuhusu kusoma nasoma vizuri tu.
 
siku ya debate ulichemka? au nn kilitokea hadi ikaanza ni hali ya kutokujiamini tu nipe majibu kwanza tuone
 
Hii mpya kwangu.

mkuu nadhani tatizo lake ni kutokuwa na mtiririko unaofaa wa mawazo, kupangilia maneno, kwa kawaida mtu anapozungumza lazima awe na flow inayoeleweka ndio mana unaweza ukamsikiliza mtu akitoa hotuba hadi anamaliza hujamuelewa anachanganyachanganya haeleweki nadhani huyu dogo ndo tatizo lake. suluhisho lake asiwe na papara wakati wa kuongea na na lazima akijue anachotaka kukizungumza na pia lugha anayotumia aielewe nazaidi ajiamini.
 
Mimi sio mtaalamu wa Elimu Maalumu, hivyo sikumbuki vizuri maneno ya kitaalamu. Anachosema huyu ndugu chaweza kuwa sahihi. Kuna mataizo binafsi katika matamshi, kiasi kwamba mtu anakuwa anaongea mfululizo (kama cherehani), anaongea neno moja moja, au mafungu mafungu, watu wengi husema ni kigugumizi, wengine kuongea kwa sauti ya chini sana.
Hata mimi ni mhanga, kama yeye, kwa kulitambua hilo, sijawahi kuomba nafasi ya kuzungumza kwenye mhadhara. Hata kwa kusoma, bado napata changamoto kiasi.
 
mimi sijakuelewa mdau tatizo la kuongea kivipi lugha unayoitumia huijui vizuri au tufafanulie kidogo tofauti na lugha hiyo lugha ulioizoea pia uko hivyo hivyo au
 
Back
Top Bottom