Nisaidieni jamani

Nisaidieni jamani

namdu

Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
9
Reaction score
2
Napenda sana kupika chapati lkn haziwi laini nifanyeje ziwe laini??
 
Mimi sio mpishi lakini najua dada farkhina anaweza kutusaidia.

Cha muhimu unaposukuma chapati ni lazima uzisukume katika matabaka (layers). Hii ina maana ukishasukuma chapati katika umbo la mviringo, ikate nusu halafu uiviringishe into a ball halafu sukuma tena. Fanya hivi mara mbili au tatu. Chapati zako hazitakuwa ngumu.

Bibie farkhina njoo huku utoe ushauri. Unatufanya sisi kaka zako tunamung'unya maneno hapa.
 
Tumia maji ya baridi kukandia unga....

Pia changanya samli na mafuta pamoja wakati wa kukanda na kutengeneza mviringo then wakati wa kukaanga tumia mafuta pekee na kidogo....

Hakikisha unakanda unga uwe laini vizuri na ukishazungusha mviringo acha kwa mda ili zilainike zaidi

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mimi natumia maji ambayo ni ya uvuguvugu zaidi kiasi. Lakini hakikisha unachekecha unga (inaongeza hewa), kisha pasha mafuta kiasi yawe ya moto sana (test kwa kudondosha unga kidogo utaona unachemka kwa mapovu na kupotea haraka). Hayo mafuta ya moto mimina kwenye unga huku unavuruga na kisu ama uma. Kisha rub-in (pasua vidonge vya mafuta kwa kusugua kwenye ncha za vidole, sio mkono huku ukinyanyua juu na kuacha utiririke(unaongeza hewa zaidi).

kanda unga kwa maji ya uvuguvugu zaidi na kata madonge madogo madogo. Sukuma na kupakaa mafuta kidogo kisha vuta vuta kupata mdabwada. Kamata ncha moja hewani na kuanza kuikunja mduara. Ukimaliza yote anda kusukuma na kuchoma.
 
Kikubwa unga maji ya uvugu vugu alafu ,, ukandee kwamuda pasipo tumia unga mwingiii chapat itakuwa lain kama unanawaa
 
Mimi natumia maji ambayo ni ya uvuguvugu zaidi kiasi. Lakini hakikisha unachekecha unga (inaongeza hewa), kisha pasha mafuta kiasi yawe ya moto sana (test kwa kudondosha unga kidogo utaona unachemka kwa mapovu na kupotea haraka). Hayo mafuta ya moto mimina kwenye unga huku unavuruga na kisu ama uma. Kisha rub-in (pasua vidonge vya mafuta kwa kusugua kwenye ncha za vidole, sio mkono huku ukinyanyua juu na kuacha utiririke(unaongeza hewa zaidi).

kanda unga kwa maji ya uvuguvugu zaidi na kata madonge madogo madogo. Sukuma na kupakaa mafuta kidogo kisha vuta vuta kupata mdabwada. Kamata ncha moja hewani na kuanza kuikunja mduara. Ukimaliza yote anda kusukuma na kuchoma.

Shosti hebu jaribu kukandwa kwa maji baridi then uje uniambie au hata baada ya kuzungusha ile mviringo weka katika mfuko safi then hifadhi kwa freezer next day toa wacha iyayuke then sukuma uchome utakuja kuniambia super soft chapati

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
1395651162851.jpg
 
King'asti asante mwaya. Mi huwa napika chapati zangu zenye layers nzuri ila kuna mahali nilikula chapati tamuuu. Ukila zinakuwa na ukavu fulani hivi. Leo nimepasha mafuta kama ulivyosuggest zimetoka nzuri zaidi ya siku zote. Layers na ukavu juu. Alafu nimekanda kwa maji baridi kama alivyosema farkhina . . .nadhani hivi ndio ntakuwa napika kwanzia sasa hivi.

LIKE LIKE kwenu.
 
Last edited by a moderator:

Mi nimependa hapo tuhh!

Mi nikifika home tu "we lete chapati" basi....sihitaji kujua vuguvugu au baridi!
Im so proud being a Man!
 
karibu sana wifi Lizzy, kakangu anaogopa kitambi kwa hiyo taratibu na hayo mafuta lol. That is my mom's recipe. Hata maandazi ukitaka yatoke chicha unaweka mafuta ya moto pia. sijajaribu kukanda na maji ya baridi, na mie ntajaribu soon. ila chapati za kumimina nakoroga unga kwa maji yaliyokuwa frijini.
King'asti asante mwaya. Mi huwa napika chapati zangu zenye layers nzuri ila kuna mahali nilikula chapati tamuuu. Ukila zinakuwa na ukavu fulani hivi. Leo nimepasha mafuta kama ulivyosuggest zimetoka nzuri zaidi ya siku zote. Layers na ukavu juu. Alafu nimekanda kwa maji baridi kama alivyosema farkhina . . .nadhani hivi ndio ntakuwa napika kwanzia sasa hivi.

LIKE LIKE kwenu.
 
Last edited by a moderator:
ntakandwa shosti lol.
Siwekagi kwa freezer atii, ngoja nifanye hiyo zoezi. Ila besti kimjini mjini nikikanda unga wa mwezi mzima nikauweka kwa freezer si ntaokoa muda mie? aagh maisha ya ukubwa magumu hazi nakumbuka kwa Mama Ngina!

Back
Top Bottom